Saturday, August 18, 2012

Mafuriko yasababisha vifo Nigeria


Mafuriko yasababisha vifo Nigeria

 15 Agosti, 2012 - Saa 09:59 GMT
Mafuriko katika eneo la Jos
Mafuriko katika eneo la Jos
Takriban watu 33 wameuawa kufuatia mafuriko makubwa kati kati mwa jimbo la Plateau nchini Nigeria.
Afisa mmoja wa shirika la kutoa misaada, Abdussalam Muhammad ameiambia BBC, kuwa maelfu ya watu wameachwa bila makao baada ya makaazi yao kusombwa na maji.
Amesema usafiri umetatizika baada ya barabara kadhaa na daraja kusombwa na maji na hivyo kuvuruga shughuli za kutoa misaaada.
Zaidi ya watu elfu kumi na mbili wameathiriwa na mafuriko hayo yaliyokumba wilaya sita ikiwemo wilaya ya Shendam.
Mwezi uliopita watu thelathini na tisa waliuawa karibu na makao makuu ya jimbo hilo Jos.
Maafisa wa serikali wamewaonya raia katika maeneo hayo kuwa huenda kukatokea mafuriko zaidi katika siku za hivi karibuni.
Msimu wa mvua nchini Nigeria huanza mwezi Machi hadi Septemba Kila mwaka.
Bwana Muhammad, ambaye ni mshirikishi wa kutoa misaada ya dharurua wa shirika la kitaifa la kukabiliana na majanga katika eneo la kati nchini Nigeria, amesema waathiriwa hao wanahitaji misaada ya vyakula, maji, mavazi, blanketi na dawa.
Wilaya ya Shendam ni miongoni mwa sehemu zilizoathiriwa pakubwa na mafuriko nchini Nigeria.
Sehemu zingine ni pamoja na wilaya za Wase na Kanam.

Waziri Mkuu Uganda adukuliwa

Waziri Mkuu Uganda adukuliwa

 17 Agosti, 2012 - Saa 13:26 GMT
Mtandao wa Waziri Mkuu wa Uganda
Afisa mmoja wa serikali ya Uganda amethibitisha kwamba mtandao wa Waziri Mkuu wa nchi hiyo umeshambuliwa na wadukuzi.
Sasa mtandao huo unaonyesha picha na ujumbe kutoka kwa wanaharakati wa watu wanaofanya mapenzi ya jinsia moja.
Katika moja wapo ya ujumbe huyo, wadukuzu wameweka ujumbe kuonyesha kuwa Waziri Mkuu wa Uganda anaomba mashoga radhi kwamba eti sasa anaunga mkono maandamano ya watu hao wanaofanya mapenzi ya jinsia moja.
Mapenzi ya jinsi moja ni hatia nchini Uganda na wengi ya wanaoshukiwa kuwa miongoni mwao wamekuwa wakishambuliwa na hata kutelekezwa na jamii.
Mapema mwaka huu , hoja ya kutaka sheria ibadilishwe na kuongoze adhabu kwa watu wanaofanya mapenzi ya jinsia moja kutoka miaka 14 hadi kifungo cha maisha iliwasilishwa kwa mara nyegine bungeni.
Awali sheria iliyopendekezwa ilikuwa inasema kwamba yeyote atakaye patikana na hatia ya kufanya mapenzi ya jinsia moja na mtoto au mlemavu au mtu anayefanya hivyo akiwa na ukimwi ,basi adhabu yake ni kunyongwa.
Mtandao wa kitengo cha sheria na uadilifu nchini Uganda pia unasemekana wiki hii ulidukuliwa.
Lakini kamishena wa habari na Teknolojia Bwana Ambrose Ruyooka,aliambia BBC kuwa tatizo hilo limerekebishwa.
Serikali ya Uganda imenzisha sheria kali ya tovuti na mtandano ilikukabiliana na ufalifu wa mtandao.
Inandaiwa kuwa mwanaharakati ajayejiita @DramaSett3r katika Twitter, ndiye anayehusika na udukuzi huo.

Familia zatafuta jamaa zao kwenye mgodi


Familia zatafuta jamaa zao kwenye mgodi

 18 Agosti, 2012 - Saa 08:54 GMT
Familia za wachimba migodi waliouliwa na polisi wa Afrika Kusini, wakati wa mgomo wa Alhamisi, zimekuwa zikipita mahospitali kuwatafuta jamaa zao.
Wanawake na watoto wakienda kutafuta habari za waume zao kwenye mgomo huko Rustenburg, Afrika Kusini
Wake wa wachimba migodi wanasema polisi na mameneja wa kampuni ya mgodi hawakuwapa orodha ya wachimba migodi 34 waliouwawa na wengine wengi waliojeruhiwa kwenye mapambano hayo.
Polisi wanasema sasa wanashirikiana na mameneja wa mgodi kutoa orodha kuu, lakini haiwezi kufichua majina ya wachimba migodi zaidi ya 200 waliokamatwa.
Rais Jacob Zuma ametangaza kuwa ataunda tume ya kuchunguza mauaji hayo.
Rais wa chama cha wafanyakzi kisichokuwa rasmi, ameiambia BBC kwamba wanataka tume ya kimataifa na iliyo huru.
Polisi wanasema watu thelathini na wanne waliuwawa katika tukio hilo.
Rais wa chama cha wafanyakazi ambacho siyo rasmi, Joseph Mathunjwa, wa Association of Mineworkers and Construction Union, aliiambia BBC kuwa wanataka tume huru ya kimataifa kuchunguza mauaji hayo kwa sababu chama chake tayari kinalaumiwa kwa ghasia hizo.
Kampuni inayomiliki migodi hiyo, Lonmin, imeahidi kusaidia familia za walioathirika, lakini inashikilia kuwa mgomo huo haukuwa halali.
Chama hicho kinataka nyongeza ya mshahara wa zaidi ya dola 1,000 kwa mwezi.
Watu kumi wakiwemo polisi wawili waliuwawa kabla ya tukio la siku ya Alhamisi.

HABARI MICHEZO NA BURUDANI

Familia zatafuta jamaa zao kwenye mgodi

BBCSwahili.com | Mwanzo - 4 hours ago
Mauaji ya wachimba migodi 34 Afrika Kusini yatachunguzwa na tume, asema Rais Zuma, huku wake wasema hawajui waume zao waliko

MABADILIKO YA UONGOZI YANGA YALIVYOCHELEWESHA MCHAKATO WA KAMPUNI YA LIGI KUU (TPL)

Shadaka at Shaffih Dauda in Sports. - 15 hours ago
Wakati ligi kuu ya Tanzaia bara ikiwa imepangwa kuanza ndani ya wiki mbili zijazo, kumekuwepo hakuna taarifa yoyote rasmi juu ya muendeshaji wa ligi hiyo kampuni (Tanzania Premium League -TPL) ambayo itakuwa ikiundwa na vilabu vishiriki vya ligi kwa pamoja na TFF kama wenye hisa. Kama itakumbukwa wakati wa ligi ya msimu uliopita ikiwa imefikia katikati, vilabu vya ligi kuu kwa kushirikiana na wadau tofauti walianzisha harakati za kutaka ligi kuu ya msimu uliopita ngwe ya pili iendeshwe na kampuni ya vilabu vyenyewe na sio TFF kama ilivyo kwenye ligi kuu za Kenya, EPL na nyingi... more »

GWIJI LA ARSENAL IAN WRIGHT ASEMA: "VAN PERSIE AMEFANYA CHAGUO SAHIHI KUJIUNGA NA MAN UNITED.

Shadaka at Shaffih Dauda in Sports. - 20 hours ago
*Ian Wright na Van Persie* Robin Van Persie amejiunga na Manchester United kutokea Arsenal, na kwanza kabisa naomba nikiri sidhani kama ameondoka kwa sababu ya fedha. Mholanzi huyo ambaye alikuwa nahodha wetu ameenda Old Trafford kwa sababu anaamini kuichezea United kutampa nafasi nzuri zaidi ya kushinda makombe. Na hili linatuumiza mashabiki wa Arsenal. Van Persie alijiunga na Gunners mwezi May 2004, muda mchache baada ya klabu yangu ya zamani kumaliza msimu bila kufungwa katika ligi kuu ya England. Hii ilikuwa timu bora kabisa ya Arsenal. Ilikuwa na uwezo wa kuendelea kutawala... more »

KUELEKEA FAINALI YA BANCABC SUPER8 HAPO KESHO: HIKI NDICHO ALICHOKI-POST KOCHA WA SIMBA SELEMANI MATOLA KWENYE FACEBOOK

Shadaka at Shaffih Dauda in Sports. - 22 hours ago
WANAGU HAPA NIKAMA MWAKA MMOJA NUSU ULIOPITA. TUOMBE MUNGU WANA CMBA KESHO IWE KAMA HIVI

JOHN BOCCO AENDELEA VIZURI SUPERSPORTS UTD.

Shadaka at Shaffih Dauda in Sports. - 22 hours ago
Baada ya majaribio ya siku 7 Super Sport United imewapunguza wachezaji sita kati ya 9 waliokuwa wakifanya majaribio, waliopunguzwa wanatoka Congo, Senegal, Nigeria na Mali. wachezaji waliobaki ni JB19 toka Tanzania, Mnigeria ambaye alikuwa Petro Athletico ya Angola na Raia wa Chad. nafasi ni moja tuu. Bocco ameongezewa siku sita nyingine za majaribio hadi Alhamisi Ijayo....All The Best JB19 [image: Photo: Baada ya majaribio ya siku 7 Super Sport United imewapunguza wachezaji sita kati ya 9 waliokuwa wakifanya majaribio, waliopunguzwa wanatoka Congo, Senegal, Nigeria na Mali. wac... more »

Ferdinand atozwa faini

BBCSwahili.com | Mwanzo - 22 hours ago
Kumtukana Ashley Cole

Waziri Mkuu Uganda adukuliwa

BBCSwahili.com | Mwanzo - 23 hours ago
Wadukuzu wameweka ujumbe kwamba Waziri Mkuu anaomba mashoga radhi eti anawaunga mkono

Wachimba migodi 30 wapigwa risasi

Polisi walifyatua risasi baada ya kushindwa kuwatawanya wachimba migodi walijihami

PICHA ZA SIKU: ROBIN VAN PERSIE AKUTANISHWA NA WACHEZAJI WENZIE WA MAN U - AANZA MAZOEZI

Shadaka at Shaffih Dauda in Sports. - 1 day ago
*Karibu kijana hapa ndio Carrington - Sir Alex Ferguson akimkaribisha RVP katika uwanja wa mazoezi* *"Jisikie upo nyumbani"* *Wayne Rooney na Robin Van Persie* *Karibu sana kijana - Nani akimkaribisha Van Persie* *RVP akisalimiana na Darren Fletcher*

HIVI NDIVYO WASHABIKI WA ARSENAL WALIVYOUMIZWA NA VAN PERSIE KWENDA MAN UNITED

Shadaka at Shaffih Dauda in Sports. - 1 day ago
Jana nilitoa nafasi kwa mashabiki wa Arsenal kuweza kutoa maoni yao juu ya suala la uhamisho wa mshambuliaji Robin Van Persie kwenda Manchester United, mamilioni ya washabiki wa Arsenal duniani walianza kuitumia kila nafasi wanayoipata kutoa maoni juu ya uhamisho huo, wengine walimtakia kheri, wengine walimkashifu na kumpa majina ya ajabu ajabu huku wengine wakijaribu hata kuchoma hata jezi zake. Kutokana na hilo nilijaribu kutoa nafasi kwa washabiki wa Arsenal ambao ni wadau wa mtandao huu kutoa maoni yao juu ya uhamisho wa Robin Van Persie. Na haya ni baadhi ya yale niliyot... more »

DEAL DONE!

Shadaka at Shaffih Dauda in Sports. - 1 day ago
Robin van Persie said: “It’s an honour to sign for Manchester United. I am looking forward to following in the footsteps of so many great strikers, bringing my experience and playing my part to help the team compete for the biggest trophies in the game. I can’t wait to get started.”

OFFICIAL: ROBIN VAN PERSIE ATAMBULISHWA RASMI MANCHESTER UNITED ASAINI MIAKA MINNE

Shadaka at Shaffih Dauda in Sports. - 1 day ago
*Robin van Persie akisaini mkataba wake wa miaka minne wa kujiunga na Manchester United mbele manager wa klabu hiyo Sir Alex Ferguson mchana huu makao makuu ya klabu hiyo jijini Manchester.*

DEBATE: KITENDO CHA ARSENAL KUMUUZA VAN PERSIE KWENDA MAN UTD,JE NDIO MWISHO WA UPINZANI NA UHASAMA BAINA YA HIVI VILABU VIWILI ?

Shadaka at Shaffih Dauda in Sports. - 1 day ago
ROBIN VAN PERSIE akiwasili kwenye hospitali ya bridgewater tayari kufanyiwa vipimo vya afya ili kumalizia taratibu za kujiunga na MAN UTD.

RAISI JAKAYA MRISHO MRISHO KIKWETE ASEMA AHADI YAKE YA KUILETA REAL MADRID IPO PALE PALE

Shadaka at Shaffih Dauda in Sports. - 1 day ago
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa bado ni dhamira ya Serikali yake kuileta moja ya timu za Ligi Kuu ya Soka ya Hispania (La Liga) kutembelea Tanzania na amemtaka Balozi mpya wa Hispania katika Tanzania kusaidia kufanikisha dhamira hiyo. Aidha, Rais Kikwete ameipongeza Hispania kwa kutetea ubingwa wa Kombe la Mataifa ya Ulaya (Euro) 2012 katika mashindano yaliyomalizika mwezi uliopita nchini Poland na Ukraine. Akizungumza na Balozi mpya wa Hispania, Mheshimiwa Luis Manuel Cuesta Civis mara baada ya kupokea hati yake ya utambulis... more »

IKIWA UNAMTAKA CRISTIANO RONALDO ITAKUBIDI KULIPA €1 BILLION

Shadaka at Shaffih Dauda in Sports. - 1 day ago
Kila mchezaji anayo bei yake, ingawa vilabu vimekuwa vikijaribu kila njia kuweza kukaa na wachezaji wao muhimu, lakini siku zote inakuwa ngumu jambo lililopelekea kuwa zinawawekea vipengele vya beighali ikiwa kuna klabu itakuja kuwataka kuwanunua wakiwa bado kwenye mkataba husika. Kupitia utafiti mdogo uliofanyika tumeweza kugundua na kupata kujua ni wachezaji gani wanaongoza kwa kuwekewa vipengele vya kuuzwa fedha nyingi kuliko wenigne. *Cristiano Ronaldo* *€1bn* *Lionel Messi* *€250m* *Fernando Torres*

Friday, June 8, 2012

Kocha afariki saa 24 baada ya mkataba

Kocha afariki saa 24 baada ya mkataba.

 7 Juni, 2012 - Saa 12:03 GMT
Manuel Preciado
Manuel Preciado
Kocha mpya aliyeteuliwa juzi Manuel Preciado amefariki saa 24 baada ya kutangazwa kama Kocha wa klabu ya Uhispania, Villarreal.
Kocha huyo ambaye hapo zamani alikua kocha wa Sporting Gijon alifariki kutokana na mshtuko wa moyo akiwa na umri wa miaka 54.
Kifo chake kimetokea saa 24 baada ya kukubali mkataba wa kuiongoza klabu ya Villareal iliyoshuka daraja, ambapo mkataba wake ulikua wa kuanza msimu wa mwaka 2012 hadi 2013.
Preciado alifutwa kazi na Sporting Gijon mnamo mwezi Januari licha ya kuiwezesha klabu hio kupanda daraja mara mbili kuingia Ligi kuu ya Uhispania, La Liga.
Mnamo mwezi Aprili mwaka 2011, klabu yake ya Sporting Gijon iliikwamisha klabu maarufu ya Real Madrid kwa kuvunja rekodi yake ya miaka tisa bila kupoteza kwenye uwanja wa nyumbani safari hii ikiwa chini ya Jose Mourinho.
Wakati wake wa uchezaji soka Preciado alicheza kama beki aliyeanzia uchezaji wake katika klabu ya Racing Santander na pia kushiriki mechi za vilabu kama Linares, Mallorca, Alaves, Ourense na Gimnastica.
Baada ya kustaafu kama mchezaji mwaka 1992, akaanza shughuli za ukufunzi akianzia klabu ya Gimnastica na pia kuifunza Racing B, Racing Santander, Levante na Murcia kabla ya kujiunga na Sporting Gijon mwaka 2006.
Baadaye aliiwezesha klabu hio kupanda daraja hadi Ligi kuu ya Uhispania katika msimu wake wa pili na kukaa na klabu hio kwa kipindi cha miaka sita.
Kocha mpya aliyeteuliwa juzi Manuel Preciado amefariki saa 24 baada ya kutangazwa kama Kocha wa klabu ya Uhispania, Villarreal.
Kocha huyo ambaye hapo zamani alikua kocha wa Sporting Gijon alifariki kutokana na mshtuko wa moyo akiwa na umri wa miaka 54.
Kifo chake kimetokea saa 24 baada ya kukubali mkataba wa kuiongoza klabu ya Villareal iliyoshuka daraja, ambapo mkataba wake ulikua wa kuanza msimu wa mwaka 2012 hadi 2013.
Preciado alifutwa kazi na Sporting Gijon mnamo mwezi Januari licha ya kuiwezesha klabu hio kupanda daraja mara mbili kuingia Ligi kuu ya Uhispania, La Liga.
Mnamo mwezi Aprili mwaka 2011, klabu yake ya Sporting Gijon iliikwamisha klabu maarufu ya Real Madrid kwa kuvunja rekodi yake ya miaka tisa bila kupoteza kwenye uwanja wa nyumbani safari hii ikiwa chini ya Jose Mourinho.
Wakati wake wa uchezaji soka Preciado alicheza kama beki aliyeanzia uchezaji wake katika klabu ya Racing Santander na pia kushiriki mechi za vilabu kama Linares, Mallorca, Alaves, Ourense na Gimnastica.
Baada ya kustaafu kama mchezaji mwaka 1992, akaanza shughuli za ukufunzi akianzia klabu ya Gimnastica na pia kuifunza Racing B, Racing Santander, Levante na Murcia kabla ya kujiunga na Sporting Gijon mwaka 2006.
Baadaye aliiwezesha klabu hio kupanda daraja hadi Ligi kuu ya Uhispania katika msimu wake wa pili na kukaa na klabu hio kwa kipindi cha miaka sita.

Bajeti gani inakuja Tanzania?

Ni bajeti gani inakuja?

editor's picture
Na editor - Imechapwa 06 June 2012
Printer-friendly versionSend to friend
Maoni ya Mhariri
HIVI serikali imeandaa bajeti gani kwa ajili ya Watanzania katika mwaka wa fedha unaoanzia mwezi ujao? Ina vipaumbele vichache vya kuzingatia au utitiri kama ilivyokuwa bajeti inayomalizika?
Imetenga fedha za kutosha kushughulikia tatizo kubwa la nishati ya umeme; au inakuja tena na porojo na mikakati isiyotekelezeka?
Hatuamini serikalini bado hawajaelewa umuhimu wa kulipa eneo hili mtizamo mpya, badala ya ule wa mazoea – kuongeza miradi ya kutumia mitambo ya kukodi ili kuzalisha umeme. Hii ni miradi ulaji.
Tuseme wakuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinachoongoza, wanadhani bado ipo nafasi ya kutumia fedha za Watanzania, kutajirisha kampuni za kikabaila na mawakala wao waliopo nchini?
Iwapo serikali ingalipo hapohapo, tutaamini kumbe wanatenda mzaha na hatutaishia hapo. Tutashikamana na wananchi kupinga kwa nguvu maana ni mpango butu ambao haukufaa juzi wala jana na hautofaa leo hata kesho.
Tunataka viongozi wasikie kilio hiki na waheshimu wanataaluma wa Shirika la Umeme nchini (TANESCO) wanaohitaji kusaidiwa fedha ili kutekeleza miradi ya maendeleo waliyoibuni. Wakisaidiwa, angalau wataacha kulalamika chinichini kuwa nguvu zao zinabezwa.
Tunalisemea sana hili tukiamini umeme ndiyo injini ya maendeleo. Bila umeme, tena wenye uhakika, hatuwezi kuota maendeleo.
Hakutakuwa na uzalishaji wenye tija, si maofisini, viwandani, mashambani wala majumbani.
Tusipokuwa na uzalishaji maeneo hayo, tumefunga fursa za kukuza uchumi wa taifa na wa familia. Uchumi hukua kwa nchi kuuza bidhaa nyingi nje, na kuzalisha chakula cha kutosha.
Nchi ikiuza zaidi bidhaa nje kuliko inavyonunua, inahifadhi fedha zake za kigeni kwa matumizi ya maendeleo ikiwemo ununuzi wa mafuta, injini nyingine kwa maendeleo.
Uzalishaji chakula husaidia sana kupunguza mfumuko wa bei za bidhaa. Takwimu za eneo hili zinasikitisha na zinahitaji kufutwa ili ziende na hali halisi ya uwezo wa wananchi.
Tungependa fedha nyingi zaidi zitengwe kutekeleza miradi ya maendeleo itakayoongeza ajira na kupunguza pengo la wenye nacho na wasionacho nchini.
Tukitanua wigo wa kodi, na kusimamia ukusanyaji wake, ikiwemo kufuta misamaha holela, tutapata mapato zaidi na kujenga uwezo wa serikali kuhudumia madeni ambayo yameanza kuwa mzigo mzito.
Sasa tuone serikali kweli viongozi wake wanasikia au wataendeleza jeuri na hivyo kujiandaa kupata fedheha kama watu walioshindwa kuongoza?

HABARI ZA VICHEKESHO


Kisa na Mkasa na Salim Kikeke

 31 Mei, 2012 - Saa 19:45 GMT

Media Player

Mikasa na vituko duniani wiki hii
Unahitaji toleo sahihi la Flash Player kucheza sauti/video

Nzi wawili tu

Mamlaka nchini Uchina zimeanzisha sheria mpya ya vyoo vya umma.
Sheria hiyo inakataza choo kuwa na zaidi ya nzi wawili kwa wakati mmoja.Sheria hiyo iliyowekwa na halmashauri ya mannispaa ya jiji la Beijing inalenga kuhakikisha hali ya usafi katika vyoo vinavyotumiwa na jamii.
Hata hivyo haijawekwa wazi ni hatua gani zitachukuliwa iwapo nzi wa watu atakutwa chooni.
Sheria nyingine ni kuhakikisha vyoo vinasafishwa kila mara na matumizi ya vifaa vyakisasa na mafunzo ya kutosha kwa watu wanaovitazama vyoo hivyo.
Mwandishi wa BBC mjini Beijing amesema sheria hizi mpya ni mahsusi kusaidia watu wengi mjini humo ambao hawana vyoo majumbani mwao na wanategemea vyoo vya umma. Bila shaka watakuwa wakitazama huko na huko kutafuta nzi wa tatu yuko wapi..

Tembo kuwa pweza

Tembo mmoja nchini Poland anatarajiwa kuchukua nafasi ya Pweza Paul kwa kutabiri matokeo ya michuano ya maataifa ya Ulaya yanayoanza hivi karibuni.
Tembo huyo anayejulikana kama Citta mwenye umri wa miaka thelathini na mitatu atakuwa akitumia mkonga wake kubashiri timu itakayoshinda.
Habari kutoka Warsaw zinasema ubashiri wa kwanza utafanywa tarehe sita mwezi Juni, siku mbili kabla ya kuanza kwa michuano hiyo. Tembo huyo alifanya kituko wakati akitambulishwa kwa waandishi wa habari, baada ya kuumeza mpira wa miguu uliokuwepo mezani.
Mkurugenzi wa hifadhi ya wanyama ya mjini Warsaw Teresa Grega amesema tembo huyo alitabiri ushindi wa Chelsea dhidi ya bayern Munich katika fainali ya Klabu Bingwa Ulaya hivi karibuni. Tembo huyo atatabiri mshindi kati ya Poland watakaopambana na Ugiriki Juni nane.
Atapewa matunda matatu, mawili yakiwa na majina ya timu hizo mbili, na tunda la tatu kwa ajili ya kutabiri sare. Tembo huyo alizaliwa India, akaishi Ujerumani kabla ya kwenda Austria, halafu Uhispania na hatimaye kuhamia Poland. Bi Gregga amesema tembo huyo anapenda sana kutazama soka.

Noti taka

Bwana mmoja nchini Marekani ameingia matatani baada yakudondosha noti ya dola moja barabarani.
Bwana huyo, John davis wa Cleveland, amesema alikuwa akijaribu kutoa sadaka kwa mtu aliyekuwa barabarani.
Davis ambaye alikuwa ndani ya gari yake, alifungua dirisha na kutoa noti kadhaa za fedha ili kumpa mtu aliyekuwa akiomba msaada.
Kwa bahati mbaya, moja kati ya noti alizokuwa akizitoa ilipeperushwa na upepo. Muda si mrefu, alitoea polisi na kumkamata bwana Davis kwa kosa la kurusha taka barabarani.
"Nimekuona ukitupa karatasi" amekaririwa polisi huyo akimwambia bwana Davis. Msamaria mwema huyo amepigwa faini pamoja na gharama za mahakama zinazofika dola mia tano.

Atoroka na gari la wagonjwa

Mwanamama mmoja aliyekuwa amelazwa hospitali, alichoshwa na maisha ya hospitalini na kuamua kuiba gari la wagonjwa na kutoroka nalo.
Mwanamama huyo Heather Sullivan wa Buffalo, New York, alikataliwa kwenda nyumbani kwa kuwa hali yake haikuwa njema sana kiafya, ingawa mwenyewe alikuwa akitaka kuondoka.
Taarifa zinasema mwanamama huyo alinyata na kuiba gari la kubebea wagonjwa la hospitali ya Erie County, na kuondoka kwa kasi kubwa. Alianza kufukuzwa na polisi.
Mwanamama huyo alikuta gari la kubebea wagonjwa likiwa limeegeshwa nje ya hospitali huku fungua za gari hilo zikinin'ginia kwenye kiwashio.
Polisi wa Buffalo wamesema mwanamke huyo aliokuwa akiendesha gari hilo kwa mwendo wa kasi na wa hatari, huku akikosa kosa kugonga wapita njia. Hatimaye gari hilo lilipoteza mwelekeo na kupunduka, na mwanamama huyo kukamatwa.
Ameshtakiwa kwa kuhatarisha maisha ya watu, na kuiba gari. Hasara aliyosababisha imefika dola laki moja.

Faini kwa mluzi

Mwanamama mmoja nchini Ujerumani amepigwa faini, baada ya kupiga mluzi kwenye simu yake na kusababisha maumivu kwa mtu aliyekuwa akizungumza naye.
Mwanamama huyo mwenye umri wa miaka sitini na moja, alikuwa amechoshwa kupigiwa simu na kampuni zilizokuwa zikimshawishi anunue bidhaa mbalimbali.
Mwanamama huyo wa Pirmasens, katika eneo la Rhineland amesema alikuwa amechoshwa na bughudha za wauza bidhaa waliokuwa wakimpigia simu kila mara kumshawishi anunue bidhaa zao. Siku ya siku alipopigiwa simu, aliamua kupiga mluzi kwa nguvu kwa mtu aliyempigia simu kiasi cha kumsababishia maumivu ya masikio. Mwanamama huyo amepigwa fani ya karibu dola mia tisa.
Alipofikishwa mahakamani alimwambia jaji kuwa alikuwa amechukizwa mno na simu za wafanyabiashara.
Na kwa taarifa yako.........Fani kongwe zaidi duniani ni ukunga na uganga wa kienyeji