Saturday, August 18, 2012

Familia zatafuta jamaa zao kwenye mgodi


Familia zatafuta jamaa zao kwenye mgodi

 18 Agosti, 2012 - Saa 08:54 GMT
Familia za wachimba migodi waliouliwa na polisi wa Afrika Kusini, wakati wa mgomo wa Alhamisi, zimekuwa zikipita mahospitali kuwatafuta jamaa zao.
Wanawake na watoto wakienda kutafuta habari za waume zao kwenye mgomo huko Rustenburg, Afrika Kusini
Wake wa wachimba migodi wanasema polisi na mameneja wa kampuni ya mgodi hawakuwapa orodha ya wachimba migodi 34 waliouwawa na wengine wengi waliojeruhiwa kwenye mapambano hayo.
Polisi wanasema sasa wanashirikiana na mameneja wa mgodi kutoa orodha kuu, lakini haiwezi kufichua majina ya wachimba migodi zaidi ya 200 waliokamatwa.
Rais Jacob Zuma ametangaza kuwa ataunda tume ya kuchunguza mauaji hayo.
Rais wa chama cha wafanyakzi kisichokuwa rasmi, ameiambia BBC kwamba wanataka tume ya kimataifa na iliyo huru.
Polisi wanasema watu thelathini na wanne waliuwawa katika tukio hilo.
Rais wa chama cha wafanyakazi ambacho siyo rasmi, Joseph Mathunjwa, wa Association of Mineworkers and Construction Union, aliiambia BBC kuwa wanataka tume huru ya kimataifa kuchunguza mauaji hayo kwa sababu chama chake tayari kinalaumiwa kwa ghasia hizo.
Kampuni inayomiliki migodi hiyo, Lonmin, imeahidi kusaidia familia za walioathirika, lakini inashikilia kuwa mgomo huo haukuwa halali.
Chama hicho kinataka nyongeza ya mshahara wa zaidi ya dola 1,000 kwa mwezi.
Watu kumi wakiwemo polisi wawili waliuwawa kabla ya tukio la siku ya Alhamisi.

No comments:

Post a Comment