Waziri Mkuu Uganda adukuliwa
17 Agosti, 2012 - Saa 13:26 GMT
Afisa mmoja wa serikali ya Uganda amethibitisha kwamba mtandao wa Waziri Mkuu wa nchi hiyo umeshambuliwa na wadukuzi.
Sasa mtandao huo unaonyesha picha na ujumbe kutoka kwa wanaharakati wa watu wanaofanya mapenzi ya jinsia moja.Mapenzi ya jinsi moja ni hatia nchini Uganda na wengi ya wanaoshukiwa kuwa miongoni mwao wamekuwa wakishambuliwa na hata kutelekezwa na jamii.
Mapema mwaka huu , hoja ya kutaka sheria ibadilishwe na kuongoze adhabu kwa watu wanaofanya mapenzi ya jinsia moja kutoka miaka 14 hadi kifungo cha maisha iliwasilishwa kwa mara nyegine bungeni.
Awali sheria iliyopendekezwa ilikuwa inasema kwamba yeyote atakaye patikana na hatia ya kufanya mapenzi ya jinsia moja na mtoto au mlemavu au mtu anayefanya hivyo akiwa na ukimwi ,basi adhabu yake ni kunyongwa.
Mtandao wa kitengo cha sheria na uadilifu nchini Uganda pia unasemekana wiki hii ulidukuliwa.
Lakini kamishena wa habari na Teknolojia Bwana Ambrose Ruyooka,aliambia BBC kuwa tatizo hilo limerekebishwa.
Serikali ya Uganda imenzisha sheria kali ya tovuti na mtandano ilikukabiliana na ufalifu wa mtandao.
Inandaiwa kuwa mwanaharakati ajayejiita @DramaSett3r katika Twitter, ndiye anayehusika na udukuzi huo.
No comments:
Post a Comment