Friday, June 24, 2011

TODAY NEWS

Habari za Kitaifa

Mrema- Nilipeni mafao yangu
Imeandikwa na Shadrack Sagati, Dodoma; Tarehe: 25th June 2011 @ 08:55 Imesomwa na watu: 59; Jumla ya maoni: 0


Habari Zaidi:


  • Hakimu akataa ombi la kukamata watu wa Chadema


  • Wafanyabiashara 6 maarufu mbaroni Arusha


  • Mbunge augua ghafla, aanguka bungeni


  • Mrema- Nilipeni mafao yangu


  • Mbunge- Mbona viongozi mafisadi hawakamatwi?


  • `Mionzi ya minara ya simu haina madhara’


  • Spika Zanzibar awakemea mawaziri watoro


  • Mzee akutwa na kiganja cha mtoto


  • Lowassa aunguruma bungeni


  • ‘Rushwa ya ngono sehemu za kazi bado tatizo’


  • ‘Kesi ya Magufuli’ kujulikana Julai 14


  • Zitto matatani


  • Mkurabita washinda Tuzo ya Afrika


  • Mahakama yaionya Serikali kesi ya Richmond


  • Mafisadi wa vocha za pembejeo kukiona


  • Bunge kujadili ‘chenji’ ya rada


  • Tatizo la mishahara kwa walimu kwisha mwakani


  • Jaji Mkuu aitaka Sudan ilinde mafanikio ya amani


  • Wananchi wamshambulia Muasia kwa mawe


  • SJMC waanzisha Shahada ya Uzamili

  • Habari zinazosomwa zaidi:


  • Balaa lingine kwa Chenge


  • Salama: Jasiri aliyetangaza kuishi na virusi vya Ukimwi


  • ‘Housigeli’ anataka kuniharibia ndoa


  • Dina Marius, mrithi wa Amina Chifupa


  • Kikwete achekecha wakuu wa wilaya


  • Vatican yamvua jimbo Askofu


  • Waliochaguliwa kujiunga kidato cha tano waongezeka kwa 22%


  • Orijino Komedi, Jay Dee waitwa Iringa


  • JK apigilia msumari wa mwisho Dowans


  • Interpol yatumika kusaka wenye zeutamu
  • MBUNGE wa Vunjo, Augustine Mrema ameiomba Serikali imwezeshe kwa kumlipa mafao yake ya kushikilia nafasi ya Unaibu Waziri Mkuu ili aweze kuendelea kushutumu maandamano yanayofanywa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ambayo alidai yana lengo la kuhatarisha amani ya nchi.

    Akichangia hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Mrema alisema maandamano hayo hayana nia njema, kwani kuna mifano duniani kuwa mwisho wa maandamano hayo wanayoita ya amani mwisho wake ni kuiondoa Serikali iliyoko madarakani.

    Kwa hali hiyo Mrema katika mchango wake, alisema iwapo Serikali itamlipa mafao yake walau asilimia 20 atapata nguvu ya kutetea amani ya nchi kwa kulaani maandamano hayo.

    Licha ya kuwa hakutaja chama cha siasa; lakini ni wazi kuwa alimaanisha maandamano ambayo yamekuwa yanaitishwa na Chadema.

    Alisema kwa kuwa mawaziri wakuu wastaafu wanalipwa mafao ya asilimia 80 ya mshahara wao kila mwezi ni vyema na yeye alipwe walau asilimia 20.

    Mrema alikuwa Naibu Waziri Mkuu wakati wa utawala wa awamu ya pili iliyokuwa inaongozwa na Rais Ali Hassan Mwinyi, maarufu kama Mzee Ruksa.

    Mrema alipewa mamlaka hayo wakati huo akiwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, kazi ambayo inaaminika kuwa aliifanya kwa umahiri mkubwa. Waziri Mkuu wa wakati huo alikuwa ni John Malecela.

    “Iweje Rais aanzishe cheo kisichokuwepo kikatiba alianza Dk. Salim Ahmed Salim na aliyefuatia ni mimi, sasa mnaniambia nini?

    Alihoji na kuongeza : “Mawaziri wengine wastaafu mnawalipa haki zao, sasa hii kwa kuwa inamhusu Mrema mnaona sawasawa kumnyima, nipeni,” alisema Mrema huku akisababisha baadhi ya wabunge kuangua kicheko.

    Akielezea namna ambavyo maandamano hayo ya amani yanavyoondoa Serikali nyingi duniani, Mrema alitoa mifano ya nchi za Tunisia, Misri, Madagascar na Libya kuwa ni mifano halisi namna ambavyo serikali za nchi hizo zimeondoka madarakani baada ya wananchi kuingia mitaani na kuandamana kwa amani.

    “Hivi Watanzania tunataka na sisi haya yatokee hapa kwetu? Vitendo hivi tunavyofanya tuwe makini visije vikaharibu nchi yetu wenyewe,” alisema Mrema huku akiwa ameshikilia moja ya gazeti binafsi lililokuwa na makala inayolaani maandamano ya amani.

    Alisema vyama ambavyo vinahamasisha vijana kuandamana, ni vyema wahamasishe vijana hao kwenda kupiga kura ili waiondoe Serikali kwa kutumia sanduku la kura na sio maandamano.

    Alisema suala la amani halina cha chama cha upinzani au chama tawala ni lazima wale wanaotaka kuhatarisha amani hiyo wakemewe.

    Juzi Kiongozi wa Kambi ya Upinzani, Freeman Mbowe wakati akitoa maoni ya kambi ya upinzani juu hotuba ya Waziri Mkuu, alisema watu wanaobeza maandamano yanayofanywa na Chadema wakome mara moja.

    Badala yake alikitaka kila chama kikajipime mbele ya wananchi kama wana sifa za kufanya maandamano hayo ama la na sio kuyabeza, kwani wao wapo kwa ajili ya kufanya siasa.










    :

    0

    2 comments:

    1. Mukama-Mafisadi CCM lazima wavue gamba

      KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilson Mukama, amesema yeye ni sawa na mtu aliyeteuliwa kufanya kazi ya kunyonga mkosaji aliyehukumiwa adhabu hiyo na Mahakama, hivyo hawezi kuogopa kutekeleza hukumu hiyo. Akifafanua kauli hiyo jana
      Soma Zaidi | Maoni | HabariPicha


      HABARI ZAIDI
      Mbunge - Mawaziri wengi mno, wapunguzwe
      Lema apinga mwafaka wa CCM, Chadema
      Mukama-Mafisadi CCM lazima wavue gamba
      Aliyekunywa kikombe Samunge ampa Babu gari
      Tao agoma kujiuzulu, amtaka Mrema ang'oke


      TAHARIRI
      Ushauri huu usipewe nafasi
      SOMA | HIFADHI





      Image
      Mkazi wa Dar es Salaam akichota maji ya chemichem huku watoto wakisubiri zamu yao katika eneo la Tandika. Licha ya maji hayo kupatikana mita chache tu toka ardhini wakazi wengi hawamudu gharama za kuchimba visima. (Picha na Robert Okanda).


      HABARI ZA BUNGE
      Kagasheki awatahadharisha wabunge
      Mbunge amtuhumu Waziri Mkuu
      Bilioni 512 zahusishwa na uzembe, wizi, ubadhirifu
      Dawa mseto ya malaria kupunguzwa bei


      UCHAMBUZI

      Image

      Ushindi wa Mkurabita UN uongeze tija kwa Watanzania

      SOMA | HIFADHI


      SAFU

      Image

      Hata hicho kidogo wananyang’anywa

      SOMA | HIFADHI


      NYOTA WA WIKI
      Image

      Wazee waoana kwa hofu ya mauti

      SOMA | HIFADHI



      MICHEZO NA BURUDANI Habari Zaidi Habari Zinazosomwa Zaidi
      Ocean View safi Kagame
      ZANZIBAR Ocean View imejiweka katika mazingira mazuri zaidi ya kufuzu robo fainali ya michuano ya Kombe Kagame baada ya kuifunga Red Sea ya Eritrea Mshambuliaji wa timu ya Ocean View ya Zanzibar, Mohamed Hamdun (kulia) akitafuta mbinu ya kumtoka beki wa Red Sea ya Eritrea, Temesgen Asefaw katika mchezo wa Kombe la Kagame uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam. Ocean View ilishinda mabao 2-0. (Picha na Yusuf Badi).

      Nsajigwa aachana na Nje Cup
      Ocean View safi Kagame
      APR yashangaa bingwa kupangwa Moro
      Bunge laelezwa sababu za kuboronga michezoni
      Watanzania waalikwa gofu Malawi

      Nsajigwa aachana na Nje Cup

      MAKALA Habari Zaidi Habari Zinazosomwa Zaidi
      JK: CCM kujivua gamba pekee hakutoshi
      MIAKA mitatu kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi wa mwaka 1995 (karibu miaka 20 iliyopita sasa), nikiwa na fikra nzito juu ya Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama (kulia) akiwa na Waziri Mkuu wa zamani, Cleopa Msuya.

      JK: CCM kujivua gamba pekee hakutoshi
      Ushabiki wa vyama wawapofusha wabunge
      Rungwe hajakata tamaa ya urais
      Wapinzani na kokoro la bajeti – 3
      KUELEKEA MCHAKATO WA KATIBA MPYA:Wanahabari wapaswa kujua wajibu wao


      BIASHARA NA UCHUMI Habari Zaidi Habari Zinazosomwa Zaidi
      Wakusanya mapato Norway kuifunda TRA
      SERIKALI ya Tanzania kupitia Mamlaka ya Mapato (TRA), imeingia mkataba wa miaka minne na Serikali ya Norway kupitia Mamlaka ya Mapato ya nchi hiyo

      Wakusanya mapato Norway kuifunda TRA
      Watakiwa kuuza mazao kwenye masoko maalumu
      Waziri-Uwanja wa Songwe ukamilike Desemba
      TATOA wapongeza mafuta ya taa kuongezwa kodi
      Kampuni zilizoboronga Arusha zaibukia Morogoro

      ReplyDelete
    2. kweli duniani kuna mambo. Mwanamume wa India, Kailash Singh mwenye umri wa miaka 65, huenda akashika chati ya watu wanaotoa harufu mbaya za mwili na nywele, kwani kwa miaka 37 hajaoga wala kukata nywele na ndevu zake.

      Sababu kubwa ya Singh kushindwa kufanya hivyo na nadhiri aliyokuwa ameiweka kwamba, ataoga, kukata nywele na kunyoa ndevu endapo atabahatika kupata mtoto wa kiume.

      Kwa mara ya mwisho alikutana na maji kwa maana ya kuoga ilikuwa kabla ya sherehe ya harusi ya kumuoa mkewe, Kalavari Devi mwaka 1974.

      Singh anaelezea sababu ya msimamo wake huo kuwa ni sharti la utabiri aliopewa na mmoja wa kiongozi wa dini ya Hindu kuwa atakapopata mtoto wa kiume, basi mtoto huyo atakuwa mwenye mafanikio makubwa sana kwenye maisha yake na atakuwa tajiri sana.

      Ni miaka 37 imepita, lakini Singh anaendelea na msimamo wake wa kutooga mpaka pale atakapofanikiwa kupata mtoto wa kiume.

      Sing ana jumla ya watoto saba wa kike, lakini juhudi zake zote za kupata mtoto wa kiume bado hazijazaa matunda.

      Mkewe ambaye sasa ana umri wa miaka 60, alishawahi kujaribu kuweka mgomo wa kutoa unyumba mpaka Singh atakapooga, lakini mgomo huo uligonga mwamba kwani Singh hakujali chochote na matokeo yake mgomo huo uliisha.

      Majirani na watoto wamekuwa wakimtania na kumtupia maneno ya kejeli mzee Singh ambaye amekuwa akipuuza kila anachoambiwa mpaka pale ndoto yake ya kuwa na mtoto wa kiume itakapotimia.

      Familia yake nayo imewahi kujaribu kutumia nguvu kumuogesha Singh katika mto Ganges, lakini alifanikiwa kuwazidi nguvu na kukimbia akisema kuwa ni heri kufa kuliko kuvunja sharti litakalomwezesha kupata mtoto wa kiume.

      Kinachomfanya Singh awe anatoa harufu kali ni kazi yake ya ufugaji ambayo huifanya akizunguka kuwalisha majani ng'ombe wake kwenye kijiji chake cha Chatav ambapo hali ya hewa yake ni ya joto kali na wakati mwingine kufikia joto la nyuzi 47.

      Mbali ya kutooga, Singh hajazikata ndevu zake na wala kuzinyoa nywele zake ambazo hivi sasa zimefikia urefu wa mita 1.9. Ili kuusafisha mwili wake, Singh huota moto kila siku jioni huku akisali kumuomba Mungu wake wa Kihindu, Shiva.

      Mzee huyo anayevuta pia bangi, anasema kwa kuuweka mwili wake karibu na moto kila jioni humsaidia kutoa jasho analolifuta na hivyo kupunguza uchafu mwilini na pia anaamini joto la moto husaidia kuua bakteria.

      “Wakati ninapoendesha baiskeli kwenda kwenye shughuli zangu, watoto wamekuwa wakinitania na kunipigia kelele kuwa siogi, hawaelewi kwanini nafanya hivi sitabadili uamuzi wangu mpaka nitakapopata mtoto wa kiume," anasisitiza Singh.

      Kwa Singh, maji kwake yana kazi mbili tu, kunywa na kunawa mikono. Hajui hata maana ya kupiga mswaki. Na mara nyingi anapoona dalili za mvua anajihadhari kwa kujifungia nyumbani kwake au kwa kujifunika na kitu maalumu.

      Mmoja wa majirani wa Singh, Madhusudan, anasema imani ya kupata mtoto wa kiume ndiyo inayomponza jirani yake ambaye kwa sasa anakimbiwa na watu wengi kutokana na kutoa harufu mbaya. Jirani huyo anafichua kwamba, kitendo cha Singh kupata watoto wengi wa kike anakichukulia kama laana, kwa kuwa kwa mila za makabila mengi ya India, wanawake ndio wanaotoa

      ReplyDelete