Saturday, June 18, 2011

The death Of Chiluba

Chiluba dies

Former Zambian President Frederick Chiluba (Feb 2008) Frederick Chiluba developed an authoritarian approach to his critics during his presidency

Related Stories

Frederick Chiluba, Zambia's first democratically elected president, has died at home at the age of 68.
Mr Chiluba was hailed as Zambia's "liberator" by his supporters when he came to office in 1991 after 27 years of single party Socialist rule.
He won praise for his economic and political reforms but was later accused of embezzlement and turning a blind eye to corruption.
The cause of his death is not known but he was known to have heart problems.
Under Mr Chiluba, Zambia was considered to be a model of African democracy and his presidency was welcomed in the West.
The former trade union leader and son of a copper miner introduced many reforms which dismantled the restrictive policies of former President Kenneth Kaunda.
But he was dogged by corruption allegations and was accused of taking an authoritarian approach to his political opponents, firing critical colleagues and jailing outspoken journalists.
He attempted to alter the constitution to allow him to run for a third term in office in 2001, but stood down after huge public protests.
Mr Chiluba was prosecuted for alleged embezzlement in 2002 but acquitted after a six-year trial.
In 2007, he was convicted of fraud by a London court and ordered to repay $58m in embezzled funds, but the ruling was never carried out by Zambia.
He spent his final years at his resident in Lusaka, confined by ill health and the confiscation of his passport by the authorities.


3 comments:

  1. Katimu Mkuu CCM akiri Serikali ilikosea Send to a friend
    Sunday, 19 June 2011 08:04
    0digg
    Habel Chidawali,Dodoma
    KATIBU Mkuu wa CCM, Wilson Mukama, amesema Serikali ilikosea kutowapeleka katika mazoezi ya vitendo wanafunzi wa vyuo vikuu, kwa kuwa hiyo ni haki yao ya msingi.

    Mukama aliwaomba radhi wanafunzi hao kwa upungufu huo na kuwataka waipe Serikali mwaka mmoja ili ibadili mfumo unaotumika sasa.
    Mukama alitoa kauli hiyo jana wakati akizungumza kwenye sherehe ya Umoja wa Wanafunzi wa Vyuo vikuu ambao ni wanachama wa CCM walioko mjini Dodoma.

    “Nawaomba radhi sana kwa kutokuwapeleka katika mazoezi ya elimu ya vitendo, lakini nawaahidi kuwa kazi hiyo tutaimaliza na haitajirudia mwakani, hivyo kuweni na amani sasa,’’alisema Mukama.

    Alisema kuwa suala la kulilia elimu kwa vitendo walilokuwa wakilitafuta wanavyuo hao ni haki yao ya msingi.
    Kuhusu suala la ajira kwa vijana wanaomaliza masomo, Mukama alisema katika ofisi na maeneo mengi wasomi wamekuwa wakiogopwa na baadhi ya viongozi wa sehemu hizo kwa hofu ya kunyang’anywa nafasi zao.

    Mkama alikiri kuwa wasomi wengi hawatumiki ipasavyo katika jamii, ikiwamo ndani ya CCM na serikalini kutokana na hofu ya walioko madarakani kupoteza nafasi zao.

    Alisema katika maeneo mengi kuna ukiritimba unaotokana na woga na hofu ya baadhi ya viongozi kwa wasomi kuwa wakiapa ajira vibarua vyao vitaota majani.
    “Katika jambo kama hilo lazima tuwe makini kwani walioko ofisini wanakuwa na woga kutokana na elimu yenu kuwa wanaweza kupoteza ajira.

    Akizungumzia kampeni ya Kujivua Gamba ndani ya CCM, Mukama alisema ipo na halikwepeki baada ya kugundulika kuwa baadhi ya viongozi wa chama hicho tawala wamekuwa wakitumia nafasi zao kwa masilahi yao binafsi.
    Mukama alisema; “hakuna jambo litakalopingwa juu ya mageuzi ndani ya chama. Nakawataka mtumie (wasomi wa vyuo vikuu) elimu yenu kufanya mageuzi wanakokwenda baada ya kuhimu.

    Katika sherehe hizo, Mukama aliwafahamisha wanafunzi hao kuwa katika ya vyuo vikuu vilivyopo mjini Dodoma kuna jumla ya wanafunzi 9,200 ambao baadhi yao wanahitimu katika kipindi kifupi na watakwenda kulitumikia taifa na chama

    Add this page to your favorite Social Bookmarking websites

    ReplyDelete
  2. Rais wa zamani Ujerumani atoa tahadhari sarafu moja EAC Send to a friend
    Friday, 17 June 2011 21:17
    0digg
    Peter Saramba, Arusha
    RAIS wa zamani wa Ujerumani, Profesa Horst Kohler ameonyesha wasiwasi na mpango wa haraka wa umoja sarafu unakusudiwa kutekelezwa na nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki(EAC), ifikapo 2012.

    Akizungumza katika hafla maalumu ya kuangalia matarajio na uhalisia wa EAC katika ulimwengu wa utandawazi mjini Arusha juzi, Profesa Kohler alisema kuharakisha mpango huo kunaweza kuleta mkanganyiko wa mambo siku zijazo kwani baadhi ya masuala ya
    msingi yanaweza kurukwa bila kujadiliwa na kupata makubaliano ya pamoja kwa maslahi ya wote.

    “Kwanini haraka katika jambo la msingi na muhimu kama hili. Siamini na haiwezekani kutekeleza mpango wa kuwa na sarafu moja 2012 kama ilivyokubaliwa katika makubaliano ya EAC. Jambo hili lazima lijadiliwe
    kwa makini na tahadhari kubwa,” alisema Profesa Kohler.

    Aliwaambia wajumbe waliohudhuria hafla hiyo iliyoandaliwa kwa pamoja na Sekretarieti ya Afrika Mashariki na taasisi ya Kijerumani ya Konrad
    Adenauer Stiftung kuwa baadhi mambo yanayohusu sarafu moja hugusa utaifa wa watu ambao uzoefu unaonyesha ni kitu muhimu kuliko vyote kwa
    jamii yoyote.

    Alitolea mfano wa mpango wa sarafu moja kwa nchi za Jumuiya ya Ulaya aliochukua muda wa zaidi ya miaka 10 tangu mwanzo wa mjadala ulioanza mwaka 1991 hadi mkataba uliposainiwa mwaka 1999 kabla ya utekelezaji
    rasmi kuanza mwaka 2002 ulipozinduliwa sarafu na noti ya kwanza ya jumuiya hiyo (EURO)

    “Kwa sababu hiyo, lazima yote yanayokusudiwa katika ushirikiano wa EAC upate kibali na uungwaji mkono kutoka kwa wananchi…ushirikiano usiwe mawazo na msukumo kutoka kwa viongozi wa kisiasa, lazima
    uzingatie mahitaji na maslahi ya wananchi,” alisema Rais huyo wa zamani.

    Kuhusu mfumo wa soko huria, Rais huyo wa zamani ambaye jana alitembelea nchi ya Rwanda
    alisema lazima ziwepo sera na mfumo unaojali na kuzingatia faida na manufaa kwa wote msukumo mkubwa ukiwekwa katika maslahi ya jamii.

    Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa EAC, Dk. Richard Sezibera alimhakikishia mgeni huyo nia thabiti ya kukamilisha na kutekeleza mipango yote inayokusudiwa katika ushirikiano wa nchi za ukanda huu wa Afrika Mashariki na kuongeza kuwa viongozi wote waliopo wameweka mbele nia na umuhimu wa mipango hiyo.

    Dk Sezibera alisema pamoja na mambo mengine ushirikiano huo unapanua soko kubwa na la uhakika kwa bidhaa zinazozalishwa katika ukanda huo wenye jumla ya wakazi zaidi ya milioni 130 na tayari mipango ya
    kuboresha miundombinu ya barabara, reli, anga na maji kurahisisha mawasiliano na kusarishaji wa watu na bidhaa za biashara umeanza kutekelezwa.

    ReplyDelete
  3. Kukamilika kwa ujenzi makao makuu EAC wahitaji Sh7 bil Send to a friend
    Friday, 17 June 2011 20:34
    0digg

    Peter Saramba, Arusha


    MATUMIZI ya ofisi za makao makuu ya Jumuiya ya Afrika
Mashariki (EAC), unaotarajiwa kukamilika Agosti mwaka huu, huenda ukakwama kutokana na upungufu wa zaidi ya Sh7.2 bilioni zinazohitajika kukamilisha ujenzi.
Mratibu wa ujenzi huo ulioanza mwaka jana, Phil Klerruu, alisema fedha hizo ni ziada ya zile za awali ambazo ni Sh33.6 bilioni, zilizotolewa na Serikali ya Ujerumani ambao ndiyo wadhamini wakuu wa ujenzi huo.

    Klerruu ambaye ni Maneja Mwandamizi wa Majengo EAC, alikuwa akitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi huo kwa Rais wa zamani wa Ujerumani, Profesa Horst Kohler, alisema fedha hizo zitatumika kujenga uzio wa kisasa kuzunguka ofisi hizo zilizojengwa pembeni mwa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC).


    “Pia, fedha hizi zitatumika kununua na kufunga vifaa vya kisasa vya
mawasiliano (IT equipments), kununua vyombo na vifaa vya kisasa vya
jikoni kwa ajili ya mghahawa utakaokuwapo katika ofisi hizi,” alisema
Klerruu.

    wajumbe wa baraza la mashuriano kuhusu nia na hali halisi
ya EAC, alisema fedhahizo pia zitatumika kukarabati majengo mawili ya kihistoria yaliyotumiwa na viongozi wa zamani wa jumuiya iliyovunjika mwaka 1977, ili yawe katika mazingira ya kisasa na yaendelee kutumika.


    Moja kati ya majengo yanayokusudiwa kukarabatiwa, ni lile lililokuwa
likitumika kama Ikulu ndogo kabla na baada ya uhuru, ambayo miaka ya karibuni ilikuwa makazi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha kabla ya
kukabidhiwa EAC na Serikali ya Tanzania.
Ujenzi wa ofisi za EAC umekamilika kwa asilimia 63 kufikia sasa na
utakuwa na majengo matatu yenye ghorofa nne, kwa ajili ya ofisi za
sekretarieti, Bunge na Mahakama ya Afrika Mashariki.

    Klerruu aliahidi kuwa watakamilisha mradi huo kwa muda uliopangwa bila gharama za ziada za ujenzi.
Profesa Kohler hakutoa ahadi ya moja kwa moja, lakini akasema nchi yake inafuatilia changamoto zinazokabili mradi huo na kwamba, wako tayari kusikiliza maombi rasmi yatakayowasilishwa.

    Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
    Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP

    Add comment
    Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!

    Name (required)

    E-mail

    ReplyDelete