Friday, June 24, 2011

TODAY NEWS

Habari za Kitaifa

Mrema- Nilipeni mafao yangu
Imeandikwa na Shadrack Sagati, Dodoma; Tarehe: 25th June 2011 @ 08:55 Imesomwa na watu: 59; Jumla ya maoni: 0


Habari Zaidi:


  • Hakimu akataa ombi la kukamata watu wa Chadema


  • Wafanyabiashara 6 maarufu mbaroni Arusha


  • Mbunge augua ghafla, aanguka bungeni


  • Mrema- Nilipeni mafao yangu


  • Mbunge- Mbona viongozi mafisadi hawakamatwi?


  • `Mionzi ya minara ya simu haina madhara’


  • Spika Zanzibar awakemea mawaziri watoro


  • Mzee akutwa na kiganja cha mtoto


  • Lowassa aunguruma bungeni


  • ‘Rushwa ya ngono sehemu za kazi bado tatizo’


  • ‘Kesi ya Magufuli’ kujulikana Julai 14


  • Zitto matatani


  • Mkurabita washinda Tuzo ya Afrika


  • Mahakama yaionya Serikali kesi ya Richmond


  • Mafisadi wa vocha za pembejeo kukiona


  • Bunge kujadili ‘chenji’ ya rada


  • Tatizo la mishahara kwa walimu kwisha mwakani


  • Jaji Mkuu aitaka Sudan ilinde mafanikio ya amani


  • Wananchi wamshambulia Muasia kwa mawe


  • SJMC waanzisha Shahada ya Uzamili

  • Habari zinazosomwa zaidi:


  • Balaa lingine kwa Chenge


  • Salama: Jasiri aliyetangaza kuishi na virusi vya Ukimwi


  • ‘Housigeli’ anataka kuniharibia ndoa


  • Dina Marius, mrithi wa Amina Chifupa


  • Kikwete achekecha wakuu wa wilaya


  • Vatican yamvua jimbo Askofu


  • Waliochaguliwa kujiunga kidato cha tano waongezeka kwa 22%


  • Orijino Komedi, Jay Dee waitwa Iringa


  • JK apigilia msumari wa mwisho Dowans


  • Interpol yatumika kusaka wenye zeutamu
  • MBUNGE wa Vunjo, Augustine Mrema ameiomba Serikali imwezeshe kwa kumlipa mafao yake ya kushikilia nafasi ya Unaibu Waziri Mkuu ili aweze kuendelea kushutumu maandamano yanayofanywa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ambayo alidai yana lengo la kuhatarisha amani ya nchi.

    Akichangia hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Mrema alisema maandamano hayo hayana nia njema, kwani kuna mifano duniani kuwa mwisho wa maandamano hayo wanayoita ya amani mwisho wake ni kuiondoa Serikali iliyoko madarakani.

    Kwa hali hiyo Mrema katika mchango wake, alisema iwapo Serikali itamlipa mafao yake walau asilimia 20 atapata nguvu ya kutetea amani ya nchi kwa kulaani maandamano hayo.

    Licha ya kuwa hakutaja chama cha siasa; lakini ni wazi kuwa alimaanisha maandamano ambayo yamekuwa yanaitishwa na Chadema.

    Alisema kwa kuwa mawaziri wakuu wastaafu wanalipwa mafao ya asilimia 80 ya mshahara wao kila mwezi ni vyema na yeye alipwe walau asilimia 20.

    Mrema alikuwa Naibu Waziri Mkuu wakati wa utawala wa awamu ya pili iliyokuwa inaongozwa na Rais Ali Hassan Mwinyi, maarufu kama Mzee Ruksa.

    Mrema alipewa mamlaka hayo wakati huo akiwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, kazi ambayo inaaminika kuwa aliifanya kwa umahiri mkubwa. Waziri Mkuu wa wakati huo alikuwa ni John Malecela.

    “Iweje Rais aanzishe cheo kisichokuwepo kikatiba alianza Dk. Salim Ahmed Salim na aliyefuatia ni mimi, sasa mnaniambia nini?

    Alihoji na kuongeza : “Mawaziri wengine wastaafu mnawalipa haki zao, sasa hii kwa kuwa inamhusu Mrema mnaona sawasawa kumnyima, nipeni,” alisema Mrema huku akisababisha baadhi ya wabunge kuangua kicheko.

    Akielezea namna ambavyo maandamano hayo ya amani yanavyoondoa Serikali nyingi duniani, Mrema alitoa mifano ya nchi za Tunisia, Misri, Madagascar na Libya kuwa ni mifano halisi namna ambavyo serikali za nchi hizo zimeondoka madarakani baada ya wananchi kuingia mitaani na kuandamana kwa amani.

    “Hivi Watanzania tunataka na sisi haya yatokee hapa kwetu? Vitendo hivi tunavyofanya tuwe makini visije vikaharibu nchi yetu wenyewe,” alisema Mrema huku akiwa ameshikilia moja ya gazeti binafsi lililokuwa na makala inayolaani maandamano ya amani.

    Alisema vyama ambavyo vinahamasisha vijana kuandamana, ni vyema wahamasishe vijana hao kwenda kupiga kura ili waiondoe Serikali kwa kutumia sanduku la kura na sio maandamano.

    Alisema suala la amani halina cha chama cha upinzani au chama tawala ni lazima wale wanaotaka kuhatarisha amani hiyo wakemewe.

    Juzi Kiongozi wa Kambi ya Upinzani, Freeman Mbowe wakati akitoa maoni ya kambi ya upinzani juu hotuba ya Waziri Mkuu, alisema watu wanaobeza maandamano yanayofanywa na Chadema wakome mara moja.

    Badala yake alikitaka kila chama kikajipime mbele ya wananchi kama wana sifa za kufanya maandamano hayo ama la na sio kuyabeza, kwani wao wapo kwa ajili ya kufanya siasa.










    :

    0

    Thursday, June 23, 2011

    ENJOY THE NEWS

    Lead story

    More Features

    • Mbowe breathes fire over lack of making bold decisions

      Mbowe breathes fire over lack of making bold decisions Leader of Official Opposition Camp in the Parliament and Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Chairman, Freeman Mbowe, yesterday hit hard at ‘coward’ Government officials and legislatures who fail to take bold moves to avoid ...0 comments
    • Petroli bei chini

      Petroli bei chini SERIKALI imepunguza tozo na kodi kwenye mafuta ya petroli na dizeli. Uamuzi huo ulitangazwa bungeni Dodoma jana na Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustapha Mkulo, alipokuwa akijhitimisha mjadala wa Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha ...0 comments
    Browse our Featured collection

    Latest News

    • Polisi wanahitaji kujipanga upya

      23 Jun 2011
      KWA mara nyingine wananchi wamevamia kituo cha polisi wakitaka wenzao waliokamatwa wakidaiwa kwa uhalifu, waachiwe huru. Wananchi hao waliokuwa na silaha za jadi walivamia kituo kikuu ...
    • Wanaouza dawa mseto bei juu kuchukuliwa hatua

      23 Jun 2011
      WIZARA ya Afya na Ustawi wa Jamii itawachukulia hatua kali za kisheria wote wanaouza dawa mseto kwa bei juu badala ya bei iliyopangwa na Serikali. Akizungumza ...
    • Rais Kikwete, Dk. Mahathir wajadili uchumi, uhusiano

      Rais Kikwete, Dk. Mahathir wajadili uchumi, uhusiano

      23 Jun 2011
      RAIS Jakaya Kikwete amekutana na waziri mkuu mstaafu wa Malaysia, Dk. Mahathir Mohammed wa Malaysia na wamejadili masuala ya uchumi na uhusiano baina ya Tanzania ...
    • Bosi wa mtandao wa mihadarati akamatwa Mexico

      23 Jun 2011
      POLISI nchini Mexico wamemkamata kiongozi wa mtandao hatari wa biashara ya dawa ya kulevya unaojulikana kama ‘La familia’, Jose Jesus Mendez. Mendez alikamatwa baada ya shambulio ...

    More News

    Advertisement

    Biashara

    • Mateja’ na biashara haramu ya kuchuja mafuta

      Mateja’ na biashara haramu ya kuchuja mafuta  Na Habakuki Urio, Dar es Salaam MOJA ya changamoto kubwa inayowakabili Watanzania wengi wakiwamo vijana, ni ukosefu wa ajira unaosababisha ugumu wa maisha. Hali hiyo imewafanya Watanzania wengi kushindwa kukabiliana na changamoto za maisha. 0 comments

    More in Biashara

    World News

    More in World News

    Makala na Uchambuzi

    • Abebwaye hukitazama kisogo cha ambebaye

      NI kweli duniani ubebaji watoto upo wa aina nyingi. Tumepata kuwaona wanaowabebea watoto ubavuni na wengine juu ya tumbo na kadhalika. Yote sawa. Lakini, kwa ujumla wake, ubebaji mtoto uliozoeleka sehemu nyingi za Afrika, Tanzania ikiwamo, ...0 comments

    More in Makala na Uchambuzi

    Burudani na Michezo

    • WOTE WABABE

      WOTE WABABE Bondi daniel Wanyonyi Kulia akitunishiana misuli na Francis Cheka wa Tanzania wakati wa mkutano wa waandishi wa habari Dar es salaam, jana kuhusu mpambano wao unaotarajia kufanyika Jumamosi kwenye uwanja wa Jamhuri Morogoro.Katikati ni ...0 comments

    More in Burudani na Michezo

    Monday, June 20, 2011

    POSHO ZA WABUNGE TANZANIA

    Sakata la Posho:Chadema wamkaba koo Waziri Mkuu  Send to a friend
    Sunday, 19 June 2011 21:04
    Waziri MKuu Mizengo Pinda
    Waandishi Wetu, Dodoma na Dar
    SUALA la kufutwa kwa posho za wabunge na watumishi wengine wa umma bado ni mwiba kwa Serikali, baada ya Chadema kuzidi kumbana Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na safari hii wakimtaka afute kauli yake kwamba posho hizo zipo kisheria kwa kuwa si kweli vinginevyo watachukua hatua kali zaidi.Chama hicho pia kimemtaka Waziri Mkuu,  kuueleza umma kwamba kauli yake ya kuwa Wabunge wa Chadema wanazimezea mate posho hizo, si kweli kwani msimamo wa kuzipinga upo kwenye Ilani ya chama hicho ya mwaka 2010.

    Katibu wa  Wabunge wa Chadema na Kambi ya Upinzani  bungeni, John Mnyika aliwaambia waandishi wa habari jana mjini Dodoma kuwa Pinda anapaswa kufanya hivyo kabla ya mwisho wa mkutano huo wa bajeti, vinginevyo wabunge wa chama hicho watakaa na kujadili cha kufanya.

    Alisema  kauli ya kuhalalisha posho za wabunge kwa hoja ya kwamba zinahitajika kwa ajili ya kuwapa watu wanaoomba fedha nje ya Ukumbi wa Bunge siyo sahihi kwani ni kinyume na misingi ya Bunge na maadili yake.

    “Waziri Mkuu, Pinda anapaswa kufuta kauli yake kwani inapotosha majukumu ya Bunge na wabunge wake yaliyotajwa kwenye ibara ya 63 kifungu cha (2) na (3) ya kuisimamia Serikali, kuwakilisha wananchi, kupitisha mipango na kutunga sheria,” alisema na kuongeza:

    “Kauli ya Waziri Mkuu Pinda inahamasisha siasa za fadhila katika taifa, ambazo zimetumika na CCM kupandikiza mbegu za rushwa katika uchaguzi kwa kisingizio cha takrima."

    Mnyika alisema kauli hiyo ya Pinda inadhihirisha kuwa hana dhamira ya dhati kutekeleza kwa ukamilifu na kwa haraka maagizo ya Rais Jakaya Kikwete kinyume na Katiba ibara ya 52 (3) inayomtaka atekeleze au asababishe utekelezaji wa jambo lolote ambalo Rais ataagiza kwamba litekelezwe.

    Alisema akiwa Katibu wa wabunge wa Chadema anamtaka Waziri Mkuu, Pinda kuelewa kuwa suala la kutaka mabadiliko ya mfumo wa posho ni la pamoja kwa Chadema na hivyo kumtaka Waziri Mkuu huyo kusoma ilani ya chama hicho kupata msingi wa msimamo huo.

    “Kama sehemu ya kuimarisha uchumi kwa kuondoa ubadhirifu ilani ya Chadema ya Agosti 2010 kifungu cha 5.5.1 kipengele cha 5 imeeleza bayana kuwa Serikali ya CCM imekuwa ikitenga kiwango kikubwa cha fedha kwa ajili ya posho,” alisema Mnyika huku akitolea mfano wa posho za Ofisi ya Rais na Bunge kwa mwaka 2009/10

    Aliendelea, "Kipengele cha 6 kwenye ilani ya Chadema ya mwaka 2010 kimeeleza bayana kwamba Serikali ya Chadema itaweka utaratibu ili semina, warsha, mafunzo na vikao katika taasisi mbalimbali za umma zifanyike kama sehemu ya kazi bila uwepo wa posho maalumu za vikao kwa siku.”

    Zitto asema Pinda anapingana na Mpango wa Taifa wa Maendeleo

    Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe amemtaka Pinda ajiuzulu au afukuzwe kazi mara moja kutokana na kutetea posho hizo kuwa zipo kwa mujibu wa sheria zilizoanishwa kikatiba na kudai  wapo Wabunge wa Chadema wanaozimezea mate.

    Akizungumza na gazeti hili jana, Zitto  alisema, " Mimi nina mambo mawili kwa Waziri Mkuu, anapaswa kuchukua uamuzi ama ku resign (kujiuzulu) au afukuzwe kazi mara moja kwa kutetea posho."

    Akitetea hoja yake, Zitto alisema kitendo cha Pinda kutetea posho kimemfanya ashindwe kutekeleza uamuzi wa kisera wa Baraza la Mawaziri ambao pia ulipitishwa na Bunge, hivyo anapaswa kujiuzulu.

    "Kwanza, nasikitika kuwa Waziri Mkuu amerejesha suala la posho za vikao kwenye mjadala ilhali lilimalizwa baada ya Bunge kupitisha Mpango wa Maendeleo wa miaka mitano. Kitendo cha Waziri Mkuu kulilia posho kinaonyesha jinsi asivyo  tayari kusimamia na kutetea sera za Serikali yake anayoiongoza," alisema na kuongeza:

    "Anapaswa kuchukua hatua mbili, ama afukuzwe kazi mara moja kwa kwenda kinyume na maamuzi ya kisera ya Serikali yaliyopitishwa na Baraza la Mawaziri kisha Bunge au, ajiuzulu. Hatuwezi kuvumilia viongozi wanaokwenda kinyume na sera za Serikali." 

    Zitto alisema uamuzi huo wa Baraza la Mawaziri ambao ni wa Serikali uliomo katika Mpango wa Taifa wa Maendeleo kwa miaka mitano, umeanisha maeneo ya vipaumbele na namna ya Serikali kudhibiti matumizi yakiwamo kukata posho na kupunguza misafara ya safari za viongozi.

    Naibu Kiongozi huyo wa upinzani bungeni alifafanua kwamba, baada ya uamuzi huo kujadiliwa ulipitishwa na wawakilishi hao na kuonyeshwa kushangazwa na kauli hiyo ya Waziri Mkuu.

    "Kauli ya Waziri Mkuu haiwezi kupita hivi hivi bila kuhojiwa. Waziri Lukuvi (Sera, Uratibu na Bunge), alisema kuondolewa kwa posho za vikao ni msimamo wa Serikali katika Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano. Then (kisha ukaletwa na Serikali na Bunge likaujadili na kuupitisha," alisema Zitto na kuongeza,

    "Sasa leo hii, wiki moja baada ya kupitishwa na Bunge, Waziri Mkuu anakuja kusema posho ni suala la kikatiba, hivyo anakwenda kinyume na uamuzi wa kisera wa Serikali, kimsingi, anapaswa ku resign ua kufukuzwa."

    Aliongeza kwamba, tayari uamuzi huo uliotokana na Baraza la Mawaziri na kisha kupitishwa na Bunge umeanishwa katika mpango huo ukurasa wa  17, hivyo kitendo cha mkuu huyo wa shughuli za kiserikali bungeni ni kuupingana nao.

    Zitto alisema akiwa waziri Kivuli wa Fedha, leo anatarajia kuwasilisha hoja bungeni akimtaka Waziri Mkuu ajiuzulu kutokana na mapungufu hayo ya kiutendaji.

    "Natarajia kuwasilisha hoja hiyo bungeni kutaka Waziri Mkuu ajiuzulu wakati nikichangia. Haiwezekani Waziri Mkuu apingane na maamuzi ya kisera ya Serikali ambayo pia yamepitishwa na Bunge." 

    Mapema mwezi huu Zitto alimwandikia Spika wa bunge barua akielezea kusudio lake la kukataa posho ya vikao vya wabunge bungeni, akijenga hoja kwamba hiyo ni sehemu ya kazi yake, hivyo kulipwa ni makosa akitaka fedha hizo zielekezwe jimboni kwake.

    Hata hivyo, hoja hiyo ambayo imetekwa na chama chake cha Chadema inaonekana kuitikisa nchi huku viongozi wa dini, wasomi na watu wa kada tofauti wakijadili kwa mitazamo tofauti.

    Askofu awalipua wabunge kuhusu posho

    Askofu wa Dayosisi ya Kaskazini ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk Martin Shao juzi alitema cheche akiwataka wabunge kuacha kutanguliza ubinafsi katika kung’ang’ania kulipwa posho za vikao vya Bunge.

    Badala yake, Dk Shao alisema posho hizo na zile wanazolipwa watumishi wa umma waliofikia ngazi ya menejimenti zielekezwe kuboresha maslahi ya watumishi wa umma wanaofanya kazi katika mazingira magumu vijijini.

    Kauli hiyo ya Askofu Shao imekuja siku chache baada ya Waziri Mkuu, Pinda kutetea malipo hayo ya posho ambayo yamezua malumbano makubwa bungeni kati Wabunge wa Upinzani , CCM na Spika, Anne Makinda.

    “Nchi hii kuna uozo huko kwa wakubwa kutanguliza mambo binafsi…mimi kwanza…na hili limesumbua sana kwenye Bunge wiki hii, wakubwa kwanza, waheshimiwa wabunge kwanza,”alisema Dk Shao.

    Askofu Shao alisema yeye anaungana na wale wanaopinga kulipwa kwa posho hizo akisisitiza kuwa si haki wabunge kutanguliza umimi na kuwataka wabunge na vigogo serikalini wasiingie katika dhambi ya umimi.

    "Posho hizo ziende zikaboreshe  matabibu vijijini, ziende kwa walimu wetu wanaofundisha katika mazingira magumu, kutanguliza umimi siyo haki, tunaomba sana wabunge msiangalie mambo yenu wenyewe,"alisisitiza Askofu Shao.

    Dk Shao alisema ni vyema Serikali ikawa na mpango mahsusi wa kuendesha sekta ya afya kwa kushirikiana na mashirika ya dini, ili kuhakikisha hospitali na zahanati vijijini zinakuwa na madaktari na wauguzi mahiri.

    Habari hii imeandikwa na Daniel Mjema, Hai, Kizitto Noya na Masoud Masasi, Dodoma, Ramadhan Semtawa, Dar.

    Saturday, June 18, 2011

    The death Of Chiluba

    Chiluba dies

    Former Zambian President Frederick Chiluba (Feb 2008) Frederick Chiluba developed an authoritarian approach to his critics during his presidency

    Related Stories

    Frederick Chiluba, Zambia's first democratically elected president, has died at home at the age of 68.
    Mr Chiluba was hailed as Zambia's "liberator" by his supporters when he came to office in 1991 after 27 years of single party Socialist rule.
    He won praise for his economic and political reforms but was later accused of embezzlement and turning a blind eye to corruption.
    The cause of his death is not known but he was known to have heart problems.
    Under Mr Chiluba, Zambia was considered to be a model of African democracy and his presidency was welcomed in the West.
    The former trade union leader and son of a copper miner introduced many reforms which dismantled the restrictive policies of former President Kenneth Kaunda.
    But he was dogged by corruption allegations and was accused of taking an authoritarian approach to his political opponents, firing critical colleagues and jailing outspoken journalists.
    He attempted to alter the constitution to allow him to run for a third term in office in 2001, but stood down after huge public protests.
    Mr Chiluba was prosecuted for alleged embezzlement in 2002 but acquitted after a six-year trial.
    In 2007, he was convicted of fraud by a London court and ordered to repay $58m in embezzled funds, but the ruling was never carried out by Zambia.
    He spent his final years at his resident in Lusaka, confined by ill health and the confiscation of his passport by the authorities.