Majaji katika mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai na uhalifu wa kivita huko The Hague wametupilia mbali ombi la raisi wa zamani wa Ivory Coast kwenda kuhudhuria katika maziko ya mamake mzazi.
Mahakama hiyo ilikua inaangalia zaidi suala la usalama wa huko aendako,na hivyo kumzuia kwenda kwao Laurent Gbagbo kwa muda wa siku tatu.Gbabo anakabiliwa na makosa ya uhalifu wa kibinaadamu kufuatia uchaguzi ulofanyika mwaka 2010,ambapo inakadiriwa watu elfu tatu waliuawa.
No comments:
Post a Comment