Saturday, October 18, 2014

HABARI KWA UFUPI KUTOKA BBC SWAHILI

Mwizi wa mapenzi akamatwa Austria

Polisi nchini Austria wanawahoji wanawake ambao wamehadaiwa na mwanamume mwenye mazoea ya kuwapenda wanawake wengi tu.

Wengi wafariki onyesho la bendi Seoul

Watu wapatao 16 wamekufa na wengine 11 kujeruhiwa katika tamasha la muziki mjini Seongnam, kusini mwa Seoul

Je,elimu ya juu yawanufaisha Wahitimu?

Haba na Haba inajadiliana na wadau nchini Tanzania kuhusu mfumo wa elimu ya juu nchini humo

Boko Haram kuwaachilia wanafunzi

Serikali ya Nigeria inasema kuwa imefikia makubaliano na kundi la wapiganaji wa Boko Haram kuwaachilia wasichana walitekwa nyara

Al-Shabaab waendeleza biashara ya mkaa

Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa imekishutumu kikundi cha Somalia cha Al Shabaab kwa kuendelea na biahara ya mkaa.

Makasisi wanaounga mkono ushoga

Askofu na kadinali wa Chile ,Ricardo Ezzati, alituma ujumbe wa siri akilalamikia Vatican kuwahusu makasisi hao wanaotetea ushoga

Ebola:Ahadi za mataifa hazijatimizwa

Shirika la MSF linasema kuwa ahadi za mataifa kutoa msaada na kupeleka wahudumu kupambana na Ebola havijakuwa na mafanikio

Mgonjwa atibiwa Uraibu wa Internet

Wanasayansi wamemtibu mwanamume mmoja mwenye umri wa miaka 31 nchini Marekani kwa wanachokisema kuwa uraibu wa kutumia mtandao wa Interne

Wanariadha watumia sana madawa Kenya

Ripoti kuhusu utumizi wa madawa haramu ya kusisimua misuli michezoni, Kenya, imebaini kuwa wanariadha wengi wa wanatumia madawa hayo

IS:Wapiganaji wafunzwa urubani

Marubani walioasi jeshi la Iraq na kujiunga na kundi la wapiganaji wa Islamic State wameanza kutoa mafunzo ya urubani kwa wapiganaji wa IS

Kigoma:Mmea ambao ni siri ya wanaume

Hata hivyo, alipozungumza na wenyeji wa eneo hilo linalojulikana kama Kabwe, akaelezwa mmea huo unaitwa Mlemela.

Wakili asema Pistorius 'amefilisika'

Mahakama inayosikiliza kesi ya mwanariadha mlemavu wa Afrika Kusini, Oscar Pistorius imeambiwa kuwa mwanariadha huyo hana pesa

Ebola:Annan akosoa mataifa ya Magharibi

Katibu mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan amekosoa ambavyo mataifa ya magharibi yameshughulikia janga la Ebola.

Bendi ya The Good Ones kutoka Rwanda

Wakati mwimbaji mkuu wa bendi hiyo na mtunzi wa nyimbo, Adrien Kazigira alipoamua kuanzisha bendi hiyo, alikuwa anawatafuta “the good ones”,

Upinzani wakataa matokeo Msumbiji

Kulingana na matokeo chama tawala kimeshinda uchaguzi huo ingawa upinzani Renamo umekataa matokeo hayo ya uchaguzi uliofanyika Jumatano.

Virusi hatari kwa viumbe vyagunduliwa

Watafiti wa masuala ya viume vya ardhini na majini, wamegundua virusi vipya vinavyoangamiza kizazi kizazi hicho.

Jeshi la Marekani kupambana na Ebola

Rais wa Marekani Barack Obama amethibitisha kulitumia jeshi la nchi hiyo na wale wa akiba kupambana na wa ugonjwa wa Ebola Afrika magharibi.

Michezo kwa ufupi

Kunea kwa ugonjwa wa Ebola umefanya fainali za Kombe la mataifa ya Afrika kuwa mashakani.

Ukeketaji watua England

Kwa mara ya kwanza tabia ya ukeketaji wa wanawake imegunduliwa England

Renamo-hatutambui matokeo

Chama cha kikuu cha upinzani nchini Msumbiji cha RENAMO,kimetoa yake ya moyoni kuwa hawatayakubali matokeo yajayo.


No comments:

Post a Comment