Thursday, December 12, 2013


Siku ya pili heshima mwili wa Mandela

 12 Disemba, 2013 - Saa 07:14 GMT
Jeneza lenye mwili wa Hayati Nelson Mandela
Waombolezaji nchini Afrika Kusini wanaingia siku ya pili katika zoezi la kutoa heshima za mwisho kwenye mwili wa Rais wa kwanza mweusi nchini Afrika Kusini Hayati Nelson Mandela.
Maelfu ya watu wamejipanga kwenye mistari wakisubiri kutoa heshima zao za mwisho kwenye mwili huo uliolazwa katika ikulu kwenye jengo la Muungano mjini Pretoria.
Mjane wa Marehemu Graca Machel na Rais wa sasa wa Afrika Kusini Jacob Zuma, viongozi wa serikali na wanafamilia walikuwa ni miongoni mwa waliotoa heshima zao za mwisho kwenye mwili wa Marehemu Mandela siku ya jumatano.
Viongozi mbali mbali pamoja na raia wa Afrika Kusini walianza kutoa heshima zao za mwisho kuanzia jumatano
Kabla ya kuwekwa katika jengo la ikulu awali mwili huo ulichukuliwa katika msafara kutoka chumba cha maiti cha hosptali hadi kwenye jengo la Muungano.
Msafara wenye jeneza la Marehemu uliondoka mjini katika Hosptali ya jeshi muda mfupi siku ya jumatano. Jeneza lilibebwa kwenye gari maalum na kufunikwa bendera ya Afrika Kusini.
Wananchi walijipanga kando kando ya barabara lilipopitishwa jeneza kama ishara ya kutoa heshma za mwisho kwa mwili wa marehemu.
Msafara ulipita katika mitaa huku baadhi ya raia wakikimbia pembeni kwenye mstari wa askari wa wanajeshi Mwandishi BBC's Joseph Winter katika mji wa Pretoria amesema.
Wanajeshi waliobeba jeneza hilo walisonga hatua kwa hatua hadi katika Majengo ya Muungano eneo alikoapishwa kuwa rais wa kwanza mzalendo wa Afrika kusini 1994.
Marehemu Mandela atazikwa nyumbani kwake katika kijiji Qunu katika jimbo la Cape Mashariki siku ya jumapili.

No comments:

Post a Comment