Friday, June 8, 2012

Kocha afariki saa 24 baada ya mkataba

Kocha afariki saa 24 baada ya mkataba.

 7 Juni, 2012 - Saa 12:03 GMT
Manuel Preciado
Manuel Preciado
Kocha mpya aliyeteuliwa juzi Manuel Preciado amefariki saa 24 baada ya kutangazwa kama Kocha wa klabu ya Uhispania, Villarreal.
Kocha huyo ambaye hapo zamani alikua kocha wa Sporting Gijon alifariki kutokana na mshtuko wa moyo akiwa na umri wa miaka 54.
Kifo chake kimetokea saa 24 baada ya kukubali mkataba wa kuiongoza klabu ya Villareal iliyoshuka daraja, ambapo mkataba wake ulikua wa kuanza msimu wa mwaka 2012 hadi 2013.
Preciado alifutwa kazi na Sporting Gijon mnamo mwezi Januari licha ya kuiwezesha klabu hio kupanda daraja mara mbili kuingia Ligi kuu ya Uhispania, La Liga.
Mnamo mwezi Aprili mwaka 2011, klabu yake ya Sporting Gijon iliikwamisha klabu maarufu ya Real Madrid kwa kuvunja rekodi yake ya miaka tisa bila kupoteza kwenye uwanja wa nyumbani safari hii ikiwa chini ya Jose Mourinho.
Wakati wake wa uchezaji soka Preciado alicheza kama beki aliyeanzia uchezaji wake katika klabu ya Racing Santander na pia kushiriki mechi za vilabu kama Linares, Mallorca, Alaves, Ourense na Gimnastica.
Baada ya kustaafu kama mchezaji mwaka 1992, akaanza shughuli za ukufunzi akianzia klabu ya Gimnastica na pia kuifunza Racing B, Racing Santander, Levante na Murcia kabla ya kujiunga na Sporting Gijon mwaka 2006.
Baadaye aliiwezesha klabu hio kupanda daraja hadi Ligi kuu ya Uhispania katika msimu wake wa pili na kukaa na klabu hio kwa kipindi cha miaka sita.
Kocha mpya aliyeteuliwa juzi Manuel Preciado amefariki saa 24 baada ya kutangazwa kama Kocha wa klabu ya Uhispania, Villarreal.
Kocha huyo ambaye hapo zamani alikua kocha wa Sporting Gijon alifariki kutokana na mshtuko wa moyo akiwa na umri wa miaka 54.
Kifo chake kimetokea saa 24 baada ya kukubali mkataba wa kuiongoza klabu ya Villareal iliyoshuka daraja, ambapo mkataba wake ulikua wa kuanza msimu wa mwaka 2012 hadi 2013.
Preciado alifutwa kazi na Sporting Gijon mnamo mwezi Januari licha ya kuiwezesha klabu hio kupanda daraja mara mbili kuingia Ligi kuu ya Uhispania, La Liga.
Mnamo mwezi Aprili mwaka 2011, klabu yake ya Sporting Gijon iliikwamisha klabu maarufu ya Real Madrid kwa kuvunja rekodi yake ya miaka tisa bila kupoteza kwenye uwanja wa nyumbani safari hii ikiwa chini ya Jose Mourinho.
Wakati wake wa uchezaji soka Preciado alicheza kama beki aliyeanzia uchezaji wake katika klabu ya Racing Santander na pia kushiriki mechi za vilabu kama Linares, Mallorca, Alaves, Ourense na Gimnastica.
Baada ya kustaafu kama mchezaji mwaka 1992, akaanza shughuli za ukufunzi akianzia klabu ya Gimnastica na pia kuifunza Racing B, Racing Santander, Levante na Murcia kabla ya kujiunga na Sporting Gijon mwaka 2006.
Baadaye aliiwezesha klabu hio kupanda daraja hadi Ligi kuu ya Uhispania katika msimu wake wa pili na kukaa na klabu hio kwa kipindi cha miaka sita.

Bajeti gani inakuja Tanzania?

Ni bajeti gani inakuja?

editor's picture
Na editor - Imechapwa 06 June 2012
Printer-friendly versionSend to friend
Maoni ya Mhariri
HIVI serikali imeandaa bajeti gani kwa ajili ya Watanzania katika mwaka wa fedha unaoanzia mwezi ujao? Ina vipaumbele vichache vya kuzingatia au utitiri kama ilivyokuwa bajeti inayomalizika?
Imetenga fedha za kutosha kushughulikia tatizo kubwa la nishati ya umeme; au inakuja tena na porojo na mikakati isiyotekelezeka?
Hatuamini serikalini bado hawajaelewa umuhimu wa kulipa eneo hili mtizamo mpya, badala ya ule wa mazoea – kuongeza miradi ya kutumia mitambo ya kukodi ili kuzalisha umeme. Hii ni miradi ulaji.
Tuseme wakuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinachoongoza, wanadhani bado ipo nafasi ya kutumia fedha za Watanzania, kutajirisha kampuni za kikabaila na mawakala wao waliopo nchini?
Iwapo serikali ingalipo hapohapo, tutaamini kumbe wanatenda mzaha na hatutaishia hapo. Tutashikamana na wananchi kupinga kwa nguvu maana ni mpango butu ambao haukufaa juzi wala jana na hautofaa leo hata kesho.
Tunataka viongozi wasikie kilio hiki na waheshimu wanataaluma wa Shirika la Umeme nchini (TANESCO) wanaohitaji kusaidiwa fedha ili kutekeleza miradi ya maendeleo waliyoibuni. Wakisaidiwa, angalau wataacha kulalamika chinichini kuwa nguvu zao zinabezwa.
Tunalisemea sana hili tukiamini umeme ndiyo injini ya maendeleo. Bila umeme, tena wenye uhakika, hatuwezi kuota maendeleo.
Hakutakuwa na uzalishaji wenye tija, si maofisini, viwandani, mashambani wala majumbani.
Tusipokuwa na uzalishaji maeneo hayo, tumefunga fursa za kukuza uchumi wa taifa na wa familia. Uchumi hukua kwa nchi kuuza bidhaa nyingi nje, na kuzalisha chakula cha kutosha.
Nchi ikiuza zaidi bidhaa nje kuliko inavyonunua, inahifadhi fedha zake za kigeni kwa matumizi ya maendeleo ikiwemo ununuzi wa mafuta, injini nyingine kwa maendeleo.
Uzalishaji chakula husaidia sana kupunguza mfumuko wa bei za bidhaa. Takwimu za eneo hili zinasikitisha na zinahitaji kufutwa ili ziende na hali halisi ya uwezo wa wananchi.
Tungependa fedha nyingi zaidi zitengwe kutekeleza miradi ya maendeleo itakayoongeza ajira na kupunguza pengo la wenye nacho na wasionacho nchini.
Tukitanua wigo wa kodi, na kusimamia ukusanyaji wake, ikiwemo kufuta misamaha holela, tutapata mapato zaidi na kujenga uwezo wa serikali kuhudumia madeni ambayo yameanza kuwa mzigo mzito.
Sasa tuone serikali kweli viongozi wake wanasikia au wataendeleza jeuri na hivyo kujiandaa kupata fedheha kama watu walioshindwa kuongoza?

HABARI ZA VICHEKESHO


Kisa na Mkasa na Salim Kikeke

 31 Mei, 2012 - Saa 19:45 GMT

Media Player

Mikasa na vituko duniani wiki hii
Unahitaji toleo sahihi la Flash Player kucheza sauti/video

Nzi wawili tu

Mamlaka nchini Uchina zimeanzisha sheria mpya ya vyoo vya umma.
Sheria hiyo inakataza choo kuwa na zaidi ya nzi wawili kwa wakati mmoja.Sheria hiyo iliyowekwa na halmashauri ya mannispaa ya jiji la Beijing inalenga kuhakikisha hali ya usafi katika vyoo vinavyotumiwa na jamii.
Hata hivyo haijawekwa wazi ni hatua gani zitachukuliwa iwapo nzi wa watu atakutwa chooni.
Sheria nyingine ni kuhakikisha vyoo vinasafishwa kila mara na matumizi ya vifaa vyakisasa na mafunzo ya kutosha kwa watu wanaovitazama vyoo hivyo.
Mwandishi wa BBC mjini Beijing amesema sheria hizi mpya ni mahsusi kusaidia watu wengi mjini humo ambao hawana vyoo majumbani mwao na wanategemea vyoo vya umma. Bila shaka watakuwa wakitazama huko na huko kutafuta nzi wa tatu yuko wapi..

Tembo kuwa pweza

Tembo mmoja nchini Poland anatarajiwa kuchukua nafasi ya Pweza Paul kwa kutabiri matokeo ya michuano ya maataifa ya Ulaya yanayoanza hivi karibuni.
Tembo huyo anayejulikana kama Citta mwenye umri wa miaka thelathini na mitatu atakuwa akitumia mkonga wake kubashiri timu itakayoshinda.
Habari kutoka Warsaw zinasema ubashiri wa kwanza utafanywa tarehe sita mwezi Juni, siku mbili kabla ya kuanza kwa michuano hiyo. Tembo huyo alifanya kituko wakati akitambulishwa kwa waandishi wa habari, baada ya kuumeza mpira wa miguu uliokuwepo mezani.
Mkurugenzi wa hifadhi ya wanyama ya mjini Warsaw Teresa Grega amesema tembo huyo alitabiri ushindi wa Chelsea dhidi ya bayern Munich katika fainali ya Klabu Bingwa Ulaya hivi karibuni. Tembo huyo atatabiri mshindi kati ya Poland watakaopambana na Ugiriki Juni nane.
Atapewa matunda matatu, mawili yakiwa na majina ya timu hizo mbili, na tunda la tatu kwa ajili ya kutabiri sare. Tembo huyo alizaliwa India, akaishi Ujerumani kabla ya kwenda Austria, halafu Uhispania na hatimaye kuhamia Poland. Bi Gregga amesema tembo huyo anapenda sana kutazama soka.

Noti taka

Bwana mmoja nchini Marekani ameingia matatani baada yakudondosha noti ya dola moja barabarani.
Bwana huyo, John davis wa Cleveland, amesema alikuwa akijaribu kutoa sadaka kwa mtu aliyekuwa barabarani.
Davis ambaye alikuwa ndani ya gari yake, alifungua dirisha na kutoa noti kadhaa za fedha ili kumpa mtu aliyekuwa akiomba msaada.
Kwa bahati mbaya, moja kati ya noti alizokuwa akizitoa ilipeperushwa na upepo. Muda si mrefu, alitoea polisi na kumkamata bwana Davis kwa kosa la kurusha taka barabarani.
"Nimekuona ukitupa karatasi" amekaririwa polisi huyo akimwambia bwana Davis. Msamaria mwema huyo amepigwa faini pamoja na gharama za mahakama zinazofika dola mia tano.

Atoroka na gari la wagonjwa

Mwanamama mmoja aliyekuwa amelazwa hospitali, alichoshwa na maisha ya hospitalini na kuamua kuiba gari la wagonjwa na kutoroka nalo.
Mwanamama huyo Heather Sullivan wa Buffalo, New York, alikataliwa kwenda nyumbani kwa kuwa hali yake haikuwa njema sana kiafya, ingawa mwenyewe alikuwa akitaka kuondoka.
Taarifa zinasema mwanamama huyo alinyata na kuiba gari la kubebea wagonjwa la hospitali ya Erie County, na kuondoka kwa kasi kubwa. Alianza kufukuzwa na polisi.
Mwanamama huyo alikuta gari la kubebea wagonjwa likiwa limeegeshwa nje ya hospitali huku fungua za gari hilo zikinin'ginia kwenye kiwashio.
Polisi wa Buffalo wamesema mwanamke huyo aliokuwa akiendesha gari hilo kwa mwendo wa kasi na wa hatari, huku akikosa kosa kugonga wapita njia. Hatimaye gari hilo lilipoteza mwelekeo na kupunduka, na mwanamama huyo kukamatwa.
Ameshtakiwa kwa kuhatarisha maisha ya watu, na kuiba gari. Hasara aliyosababisha imefika dola laki moja.

Faini kwa mluzi

Mwanamama mmoja nchini Ujerumani amepigwa faini, baada ya kupiga mluzi kwenye simu yake na kusababisha maumivu kwa mtu aliyekuwa akizungumza naye.
Mwanamama huyo mwenye umri wa miaka sitini na moja, alikuwa amechoshwa kupigiwa simu na kampuni zilizokuwa zikimshawishi anunue bidhaa mbalimbali.
Mwanamama huyo wa Pirmasens, katika eneo la Rhineland amesema alikuwa amechoshwa na bughudha za wauza bidhaa waliokuwa wakimpigia simu kila mara kumshawishi anunue bidhaa zao. Siku ya siku alipopigiwa simu, aliamua kupiga mluzi kwa nguvu kwa mtu aliyempigia simu kiasi cha kumsababishia maumivu ya masikio. Mwanamama huyo amepigwa fani ya karibu dola mia tisa.
Alipofikishwa mahakamani alimwambia jaji kuwa alikuwa amechukizwa mno na simu za wafanyabiashara.
Na kwa taarifa yako.........Fani kongwe zaidi duniani ni ukunga na uganga wa kienyeji

Miili ya watu 14 imepatikana Mexico

Miili ya watu 14 imepatikana Mexico

 8 Juni, 2012 - Saa 07:26 GMT
Milli ya watu iliyokatakatwa nchini Mexico
Milli ya watu iliyokatakatwa nchini Mexico
Serikali ya Mexico imesema kuwa imapata miili ya watu 14 ambayo imekatakatwa ndani ya lori iliokuwa imeegezwa nje ya ofisi ya meya wa mji wa Ciudad Mante, Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo.
Ripoti zinasema kuwa ujumbe ulioandikwa na kundi moja la kigaidi limepatikana ndani ya blanketi iliyotumika kufunika miili ya watu hao.
Miongoni mwa walioauawa ni wanaume kumi na mmoja na wanawake watatu.
Mauaji hayo yametokea siku moja baada mgombea anayeongoza katika kinyanganyiro cha kuwania kiti cha urais, Enrique Pena Nieto, kuzuru jimbo hilo na kuhaidi kuwa atapunguza viwango vya mauaji ikiwa atachaguliwa kuwa rais wa taifa hilo.
Tangu mwaka wa 2006 Mexico imeshuhudia misururu ya ghasia zinazohusiana na ulanguzi wa madawa ya kulevya baada ya rais wa nchi hiyo Felipe Calderon, kutoa amri kwa jeshi la nchi hiyo kuyasaka makundi ya walanguzi wa mihadarati.

Annan ataka dunia iungane dhidi ya Syria

Annan ataka dunia iungane dhidi ya Syria

 8 Juni, 2012 - Saa 06:52 GMT
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon na Kofi Annan
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon na Kofi Annan
Ujumbe maalumu wa Bwana Koffi Annan kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ulikuwa kwamba Baraza hilo ni sharti liungane katika hatua ya kushinikiza Serikali ya Syria kutekeleza mpango wake, au sio hali hiyo itasababisha hali kuwa mbovu zaidi.
Bwana Annan, ambaye ni balozi maalumu wa maswala ya Syria, kwa mara ya kwanza aligusia uwezekano wa kutumia vikwazo, akisisitiza kuwa lazima kuwepo na adhabu ya aina fulani kwa ye yote anayekataa kufuatilia kikamilifu mpango huo wa amani.
Katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kulikuwepo mapatano ya kauli moja kuwa lazima hatua muhimu ichukuliwe lakini, ingawa haikubainika hatua ipi inapaswa kuchukuliwa.
Mataifa kadhaa ya Magharibi yalipendekeza vikwazo lakini Urusi ililipa wazo hilo kisogo na kutoa kauli kuwa makundi ya upinzano yenye silaha yasiposhinikizwa pia hakuna haja ye yote kwa Serikali kukubali mapendekezo ya jamii ya kimataifa.
Wakati huohuo Bwana Annan alikiri kuwa mashauriano yameanza juu ya uwezakano wa kuanzisha jopo la eneo na viongozi wa kimataifa ili kushawishi Serikali ya Syria kupunguza uhasama kati yao.

Chadema watisha mawaziri

Moto wa Chadema watisha mawaziri  Send to a friend
Thursday, 07 June 2012 19:58
0digg
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa akihutubia wakazi wa Lindi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Michezo wa Ilulu, juzi. Chama hicho kipo katika ziara ya mikoa ya kusini katika ziara ya ‘Operesheni okoa Kusini’. Picha na Emmanuel Herman
MKUCHIKA, GHASIA, CHIKAWE NA MEMBE WAENDA KUUZIMA, CCM KUJIPIMA NGUVU JANGWANI KESHO
Geofrey Nyang’oro, Mchinga
VUGUVUGU la Mabadiliko (M4C) linaloendeshwa na Chadema katika mikoa ya Lindi na Mtwara, limewatisha mawaziri wanne wanaotoka katika mikoa hiyo, ambao wamelazimika kurejea majimboni mwao kusafisha hali ya hewa.

Mawaziri waliorejea majimboni kufanya kilichoelezwa ni shughuli za kiserikali ni pamoja Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Hawa Ghasia, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora), George Mkuchika, Waziri wa Sheria na Katiba, Mathias Chikawe na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe.

Kwa wiki takribani ya pili sasa, Chadema kimekuwa kikiendesha operesheni hiyo ya vuguvugu la mabadiliko katika mikoa hiyo ya kusini mwa nchi.

Jana, taarifa zilizopatikana mkoani Lindi zilisema Ghasia alifanya mkutano katika jimbo lake la Mtwara Vijijini akiwa katika harakati za kufuta nyayo za Chadema.
Oparesheni hiyo ya Chadema jana na leo ilitarajiwa kuingia jimbo la Mtama ambalo linaongozwa na Membe.

Vuguvugu hilo linaongozwa na viongozi wa ngazi za juu wa Chadema, ambao ni Katibu Mkuu Dk Willibrod Slaa na Mwenyekiti wa Chama hicho, Freeman Mbowe ambao wanatarajia kuhutubia mikutano yao katika kata aliyozaliwa Membe.

Mkuchika alithibitisha jana kuwa yuko jimboni kwake Newala, na alipoulizwa kama lengo lake ni kufuta nyayo za Chadema, aling’aka, “Kwani kila siku nikija nyumbani kwangu huwa mnaniuliza, mimi nimekuja nyumbani kwangu bwana. Niacheni nipumzike nyumbani kwangu.”

Membe alipotafutwa kuzungumzia taarifa hiyo simu yake haikuwa hewani, lakini Msemaji wa wizara hiyo, Assah Mwambene alipoulizwa alipo bosi wake alithibitisha kwamba yuko jimboni kwake.

Jana, vuguvugu hilo lilikuwa katika Jimbo la Mchinga mkoani Lindi, lakini lilikumbana na upepo mzito wa kisiasa baada ya bendera mpya za CCM kuonekana kupamba kona mbalimbali za jimbo hilo.
Waziri Ghasia na Chikawe pia hawakupatikana kupitia kwa simu zao kuzungumzia taarifa hizo.

Msigwa ashambulia mawaziri
Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa  aliwashambulia mawaziri hao wanaotoka majimbo ya mikoa ya Kusini ya Lindi na Mtwara, akihoji ni kwanini wanaikumbatia CCM.
Msigwa alisema CCM imeshindwa kuwasaidia kuleta maendeleo katika mikoa hiyo ya kusini mwa Tanzania, ndiyo sababu, watu wanaishi katika hali ya umasikini wa kutisha.

“Mimi ninawashangaa   wabunge wa majimbo ya Lindi na Mtwara wakiwamo mawaziri Hawa Ghasia,  Mkuchika na Bernard Membe ni kwa nini wanakiunga mkono CCM wakati majimbo yao yamekithiri kwa umaskini,” alisema Msigwa na kuongeza;

“Nashangaa Membe, Hawa Ghasia na Mkuchika sijui kiburi wanakipata wapi. Ndiyo sababu wamehama majimbo yao na kuishi Dar es Slaam, haiwezekani leo mikoa wanayotoka, wilaya na hata majimbo yakawa na sura kama ilivyo sasa. Nitakwenda kuwabana bungeni,’’ alisema Msigwa.

 Msigwa alitamba kuwa yeye na wabunge wote wa Chadema wanaishi kwenye majimbo yao, ndiyo sababu wamekuwa wakifanikiwa katika mikakati yao ya kutetea na kuwaletea maendeleo wananchi wao.

Sugu alia umaskini
Katika mkutano huo, Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi (Sugu) alisema ukarimu wa wakazi wa Lindi na Mtwara kwa CCM ndio uliosababisha mikoa hiyo kuwa katika lindi la umaskini.
 Mbilinyi alisema wabunge kupitia chama hicho hawana uwezo wa kuwaletea wananchi maendeleo kutokana na mfumo wa chama hicho kukumbatia matajiri na kuachana na maskini.

Alisema ndani ya CCM, watu wa kipato cha chini hawawezi kupata ubunge, akitoa mfano kwamba fomu ya ubunge ya CCM inachukuliwa kwa Sh100, 000 ilihali ya Chadema ni  Sh50,000.

“Nawasihi vijana wenzagu kuungana na kuwa na ujasiri wa kuamua katika masuala ya kimaendeleo. Mimi nilikuwa mitaani na muziki wangu, lakini nikatokea Chadema na kunipa nafasi ya kugombea ubunge ,lakini ningekwenda CCM wasingenipa nafasi ya kugombea kwa sababu ya umaskini wangu,” alisema Mbilinyi na kuongeza:

 “Hivyo, basi wazee na vijana nawasii kuachana na CCM kwa sababu chama hicho kimekosa mwelekeo tangu alipofariki  Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, CCM iliyobaki ni ya wanjanja sio wewe ulioko kijijini.”

CCM kujipima nguvu Jangwani
Wakati Chadema ikizidi kuwasha moto wa vuguvugu la mabadiliko, Chama tawala CCM kesho kitafanya mkutano wa hadhara katika viwanja vya Jangwani jijini Dar es Salaam,  kutoa msimamo wake kuhusu mambo  muhimu yanayogusa taifa.

Mkutano huo unafanyika ikiwa zimepita takribani wiki mbili tangu Chadema wafanye mkutano mkubwa katika viwanja hivyo uliohudhuriwa na mamia ya watu, na kuzindua kampeni yake ya M4C’, yenye lengo la kushika dola mwaka 2015.

Kwa mujibu wa taarifa iliyopatikana katika mtandao wa chama hicho tawala jana, iliyotolewa na Katibu wa Siasa na Uenezi wa mkoa huo, Juma Simba ilieleza kwamba mkutano huo utaanza saa 8 mchana.

Simba alisema katika taarifa hiyo kwamba, chama hicho kitatumia mkutano huo kuwaeleza Watanzania msimamo wake kuhusu hatma ya maisha yao.

“Utaeleza hatma ya maisha ya Watanzania katika suala la ajira, miundombinu ya barabara, reli, bandari na anga, bei za bidhaa mbalimbali, umeme na rasilimali za taifa,” alisema Simba.

Alifafanua kwamba jambo jingine litakaloelezwa katika mkutano huo, ni msimamo wa chama hicho kuhusu mchakato wa Katiba Mpya pamoja na vurugu za Zanzibar.

Katika mkutano huo watakuwapo viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali na kutoa ufafanuzi juu ya masuala hayo, yaliyoainishwa kama msimamo wa chama hicho.

Mwakyembe: Nimemng’oa bosi ATCL kwa ufisadi

Mwakyembe: Nimemng’oa bosi ATCL kwa ufisadi  Send to a friend
Thursday, 07 June 2012 19:54
0digg
Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe akizungumza katika mkutano na na wafanyakazi wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) uliofanyika Dar es Salaam jana. Katikati ni Kaimu Mkurugenzi mpya wa ATCL, Milton Lazaro na Mkurugenzi Rasilimali Watu, Judith Ndaba. Picha na Rafael Lubava
ASEMA WANAOUNUNG’UNIKA WAKO HURU KUJIONDOKA
Fidelis Butahe
SIKU nne baada ya kung’olewa aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), Paul Chizi, Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe ameamua kuanika tuhuma za ufisadi zinazodaiwa kufanywa na kigogo huyo.Miongoni mwa tuhuma hizo ni kuingia mkataba wa kununua ndege bila kumhusisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali(AG) na kununua sare 15 za watumishi wa ndege kwa dola 50,000 za Marekani.

Juni 5, Dk Mwakyembe alitengua uteuzi wa Chizi na kumteua rubani wa muda mrefu, Kapteni Lusajo Lazaro kukaimu nafasi hiyo, akisema uteuzi ulikiuka Sheria za Utumishi wa Umma.

Mbali na kutengua uteuzi huo, pia alitangaza kuwasimamisha kazi vigogo wengine wanne wa shirika hilo, hatua ambayo ilianza kuibua malalamiko kutoka kwa baadhi ya wafanyakazi kwamba hatua hiyo ilitokana na majungu na ukabila.

Waliosimamishwa kazi na Dk Mwakyembe ni Kaimu Mkurungenzi wa Uhandisi, Jonh Ringo, Mwanasheria  ,Amini Mziray, Kaimu Mkurugenzi wa Fedha, Justus Bashara na Josephat Kagirwa ambaye alikuwa Kaimu Mkurugenzi wa Biashara.

Jana, waziri huyo wa uchukuzi aliamua kufafanua tuhuma moja hadi nyingine zinazomhusu kigogo huyo na wenzake na kusema, mbali ya tuhuma za Chizi, wakurugenzi wawili wa shirika hilo walikwenda kushonesha sare 15 za wahudumu wa ndege nchini China kwa gharama ya dola 50,000 za Marekani (karibu Sh80 milioni).

Akizungumza na wafanyakazi wa shirika hilo katika Uwanja wa Ndege wa zamani (Terminal One) jijini Dar es Salaam, Dk Mwakyembe alisema kutokana na hali hiyo, ameagiza kujazwa kwa nafasi zilizo wazi na kuwaonya watakaozichukua, kuhakikisha wanachapa kazi ili ATCL ipige hatua na kama wakishindwa watakuwa wamejiondoa wenyewe.

Dk Mwakyembe alitoa miezi mitatu kwa shirika hilo kuanza kujiendesha kwa faida, ikiwa ni pamoja na kupata fedha za kuwalipa wafanyakazi wake.

“Kwa kasi niliyoanza nayo watu kama Chizi ni lazima wakae pembeni, ni mtaalam katika masuala haya, lakini tatizo lake hakuwa muwazi,” alisema Dk Mwakyembe.Chizi hakupatikana jana kuzungumzia tuhuma hizo, wakati wote Mwananchi ilipompigia simu yake ya kiganjani, ilikuwa imezimwa.

Waziri huyo ambaye pia ni Mbunge wa Kyela, alitumia Saa 1:17 kuzungumza na wafanyakazi hao na kufafanua kwamba Serikali imechoka kutoa fedha za kuliendesha shirika hilo, akihoji iweje mashirika mengine ya ndege yaweze kusimama yenyewe, lakini  ATCL iishindwe.

“Tunaipenda ATCL iendelee na tunachukua hatua za kila aina ila tukiona tunashindwa tutaachana nalo ili, fedha zinazotumika hivi sasa zipelekwe kufanyia mambo mengine ya maendeleo,” alisema Dk Mwakyembe.

Tuhuma
Akichambua tuhuma moja hadi nyingine za ukiukwaji wa sheria na taratibu, Dk Mwakyembe alianza kwa kutolea mfano mkataba tata baina ya shirika hilo na Air Bus ambao umeifanya nchi kudaiwa Sh69 bilioni na kusisitiza kuwa, kutokana na hali hiyo Serikali haikuwa tayari kufumbia macho mambo mengine ya ovyo yaendelea katika shirika hilo.

Alisema wafanyakazi wote wa ATCL ambao wananung’unika baada ya kutengua uteuzi wa Chizi wako huru kuondoka katika shirika hilo, huku akionya atawatimua wengi watakaofanya mambo kinyume.

“Nilipoteuliwa kuwa waziri wa uchukuzi siku chache baadaye nilisikia ATCL wanaleta ndege mpya, nilimwita Katibu Mkuu wa wizara anipe ufafanuzi wa jambo hilo, lakini, akaniambia hafahamu lolote,” alisema Dk Mwakyembe.

Aliongeza, “Ndege hiyo ilikodishwa na kutua nchini kwa mara ya kwanza mwezi uliopita kutokana na iliyokuwapo kuanguka mkoani Kigoma. Ndege hiyo aina ya Boeing 737-500 imekodishwa kutoka Kampuni ya Aero Vista ya Dubai.”

Dk Mwakyembe kwa sauti ya ukali alisema, “Niliamua kuwaita wakurugenzi wa ATCL ofisini kwangu saa 3 asubuhi, lakini wakaja saa nne na nusu, pamoja na hayo walinieleza kuwa jambo hilo liko safi na limeshafika kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali.”

Alisema baada ya siku moja, alipata taarifa kutoka ofisi ya AG ikieleza kwamba hawana mkataba huo.

“Nikaona jambo zito kidogo, nikaamua kukutana na wale wawekezaji ambao walinionyesha mkataba ule ambao ulipitishwa bila wizara kujua, jambo hilo nililihoji pia…, nawambia ukweli mkataba huu niliuona upande wa pili sio kwa viongozi wa shirika,” alisema Dk Mwakyembe.

Alisema hivi sasa mchakato wa kuchunguza mikataba hiyo umeshaanza na kusisitiza kuwa, hiyo ndio ilikuwa moja ya sababu ya kumng’oa Chizi.


Dk Mwakyembe alisema, “nchi haiwezi kuendelea kwa kukiukwa kwa sheria za ununuzi na ajira. Hata Kapteni Lazaro naye ameponea chupu chupu maana kabla ya kuwang’oa wakurugenzi tulipitia mafaili yao.”

“Msitegemee kubebwa ndugu zangu, nawaomba mchape kazi, mishahara yenu sio mizuri, lakini mkiweza kusimama mtakuwa na uwezo wa kujipangia hata mishahara,” alisema Dk Mwakyembe.

Alisema kwa kutambua mchango wa ATCL, Serikali imepata Sh4.9 bilioni kwa ajili ya matengenezo ya ndege ya shirika hilo na kuwataka kuzitumia kwa ufanisi fedha za shirika hilo.“Hivi sasa inatakiwa kila baada ya miezi mitatu tunakutana na kuzungumza,” alisema Dk Mwakyembe.

Kapteni Lazaro aahidi ushirikiano
Kwa upande wake, Kapteni Lazaro aliahidi kuyazingatia yote yaliyozungumzwa na waziri huyo, huku akiomba shirika hilo kuongezewa muda zaidi kwa kuwa miezi mitatu ni michache ili liweze kujitegemea.


Kupanda/kushuka  ATCL
ATCL ni kampuni iliyoanzishwa baada ya Shirika la Ndege la Tanzania ATC kuingia ubia na Shirika la Ndege la Afrika Kusini (SAA) mnamo mwaka 2002.

ATCl ni moja ya mashirika ya ndege yaliyoonyesha kukua kwa kasi miaka ya 1980 na 1990, lakini lilianza kuyumba kutokana na uendeshaji mbovu na hali ikawa mbaya zaidi baada ya kuingia ubia na SAA.

Serikali iliingia mkataba wa ubia na SAA mwaka 2002 kwa matumaini kwamba itakua na kuwa moja ya mashirika makubwa ya ndege Afrika, lakini hali ikawa kinyume chake.

Kwenye mkataba huo, Serikali ikibakia na hisa 49 huku SAA ikiwa nazo 51, ambazo zilimfanya mbia huyo kuwa na nguvu ya kuamua mambo mengi.

Serikali ilivunja mkataba na SAA Septemba 2006, baada ya kubaini kuwa ATCL inazidi kudidimia kiuchumi huku madeni yakiwa yanaongezeka kadri muda ulivyokuwa unaenda.

Miili ya watu 14 imepatikana Mexico

Miili ya watu 14 imepatikana Mexico

BBCSwahili.com | Mwanzo - 4 hours ago
Miili ya watu 14 ambayo imekatakatwa imepatikana ndani ya lori mjini Ciudad Mante, Kaskazini Mashariki mwa Mexico

Kamati ya katiba kuteuliwa Misri

BBCSwahili.com | Mwanzo - 4 hours ago
Ripoti zinasema kuwa mzozo uliokuwa umeibuka kuhusu jopo maalum la kuandika katiba mpya nchini Misri hatimaye imetatuliwa

Annan ataka dunia iungane dhidi ya Syria

BBCSwahili.com | Mwanzo - 5 hours ago
Ujumbe maalumu wa Koffi Annan kwa Baraza la Usalama la UN ulikuwa kwamba dunia liungane kushinikiza Serikali ya Syria.

KULWA NA DOTO MAMA YAO NI MMOJA!

Shadaka at Shaffih Dauda in Sports. - 12 hours ago
Kikubwa zaidi ninachojaribu kukiangalia ni jinsi ambavyo viongozi wa vilabu vya SIMBA na YANGA wasivyopenda kufuata taratibu na kanuni zilizowekwa, mwenyekiti wa SIMBA ameongelea kwa jazba kubwa sakata la beki wa timu yake Kelvin Yondani kusajiliwa na Yanga, si ajabu kesho tu tukasikia viongozi wa YANGA nao wakilijibu hili kwa mbwembwe. Lakini mwisho wa siku ni lazima tukubali kuwa viongozi wote hawa wa simba na yanga wana mapungufu makubwa sana katika utendaji wao wa Kazi, na namna wanavyoendesha vilabu vyao na mpira wa Tanzania kwa ujumla. Viongozi hawa wa SIMBA na YANGA W... more »

Euro 2012: UBAO WA TAKWIMU ZA WACHEZAJI!

Shadaka at Shaffih Dauda in Sports. - 14 hours ago
[image: Euro 2012 Focus: Player Stats Leaderboards] [image: Euro 2012 Focus: Player Stats Leaderboards] [image: Euro 2012 Focus: Player Stats Leaderboards] [image: Euro 2012 Focus: Player Stats Leaderboards] [image: Euro 2012 Focus: Player Stats Leaderboards]

TETESI : JUMA NYOSO HUYOO YANGA

Shadaka at Shaffih Dauda in Sports. - 16 hours ago
TAARIFA NILIZOZIPATA HIVI PUNDE BEKI WA SIMBA JUMA NYOSSO MUDA WOWOTE KUANZIA HIVI SASA HUENDA NAYE AKASINI KWA AJILI YA KUJIUNGA NA YANGA. TAARIFA NILIZOZIPATA KUTOKA KWENYE CHANZO CHA KUAMINIKA KIKOSI KAZI CHA YANGA TAYARI KIPO KWENYE KAMBI YA TIMU YA TAIFA KWA AJILI YA KUMALIZANA NA BEKI HUYO .

IMF kurejesha ufadhili kwa Malawi

BBCSwahili.com | Mwanzo - 17 hours ago
Dola milioni 157 kama mkopo kwa Malawi ili kuuchepua uchumi wake ambao umedorora

Bia yaidhinishwa Brazil Kombe la Dunia

BBCSwahili.com | Mwanzo - 17 hours ago
Rais Dilma Rousseff wa Brazil amwaga wino kuidhinisha kuwa sheria bia kuuzwa wakati wa mechi za Kombe la Dunia mwaka 2014

Katika teknolojia wiki hii

BBCSwahili.com | Mwanzo - 17 hours ago
Teknolojia mpya ya Microsoft yazinduliwa

Nyota wa soka waafrika kwenye Euro 2012 kwa picha

BBCSwahili.com | Mwanzo - 18 hours ago
Kutana na wachezaji soka wenye mizizi yao barani Afrika ingawa wanachezea mataifa ya kigeni. Je watangara au?

Mamilioni kwa watakaowafichua al-shabaab

BBCSwahili.com | Mwanzo - 18 hours ago
Serikali ya Marekani imetenga dola milioni 33 kwa watakaotoa taarifa zitakazopelekea kukamatwa kwa viongozi saba wa kundi la al-shabab nchini Somalia. Marekani na wachambuzi wengine wa masuala ya usalama wamehusisha kundi hilo na lile la al Qaeda.

Mshirika wa Gbagbo akamatwa.

BBCSwahili.com | Mwanzo - 18 hours ago
Moise Lida Kouassi ni wa kwanza kati ya washirika wa Bwana Gbagbo kukamatwa baada ya uchaguzi wa mwaka 2010.

Ufaransa haitutishi!

BBCSwahili.com | Mwanzo - 18 hours ago
Timu ya England yajipiga moyo konde

EURO 2012: ITALIA NA SAFU YA USHAMBULIAJI YA WENDAWAZIMU CASSANO NA BALOTELLI.

Shadaka at Shaffih Dauda in Sports. - 20 hours ago
*Maneno ya Cesare Prandelli alipomrithi Marcello Lippi kama kocha wa timu ya taifa baada ya kombe la dunia mwaka 2010 ni kwamba ataifanya Azzuri ivutiwa kwa kucheza soka zuri la kushambulia. Kwa hakika amejitahidi sana huku akitambulisha utaratibu wa 'ethical code' (wachezaji wanaokuwa wamesimamishwa kwa makosa ya kinidhamu hawatoitwa timu ya taifa) na kusisitiza katika kuwapa nafasi zaidi viungo wenye ufundi zaidi katika timu yake. Wazo ni kuifanya Italia kucheza kwa staili yake ya mfumo wa tiki-taka, staili inayopendelewa zaidi na Wahispania. Akiuacha mfumo wa siku nyingi wa kuj... more »

Chris Hughton meneja mpya Norwich City

BBCSwahili.com | Mwanzo - 20 hours ago
Achukua nafasi iliyoachwa wazi na Paul Lambert

Treetops

BBCSwahili.com | Mwanzo - 22 hours ago
Hoteli alimokuwa Malkia Elizabeth alipofahamishwa kifo cha babake 1952

COPA COCA-COLA TAIFA KUANZA KUTIMUA VUMBI JUNI 24

Shadaka at Shaffih Dauda in Sports. - 22 hours ago
Michuano ya Copa Coca-Cola ngazi ya Taifa inaanza kutimua vumbi Juni 24 mwaka huu kwenye mikoa ya Dar es Salaam na Pwani huku pambano la ufunguzi likiwa kati ya Kigoma na Lindi litakalofanyika kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam. Upangaji ratiba (draw) umefanyika leo (Juni 7 mwaka huu) kwenye ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na kushuhudiwa na waandishi wa habari, makocha wa timu za mikoa za Copa Coca-Cola na wadhamini kampuni ya vinywaji baridi ya Coca-Cola. Makocha 35 wa timu za Copa Coca-Cola kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwa... more »

SAKATA HILI LA YONDANI KWA UPANDE MWINGINE LIMECHANGIWA NA SERA MBOVU YA USAJILI YA SIMBA!

Shadaka at Shaffih Dauda in Sports. - 22 hours ago
Sakata la usajili wa Kelvin Yondani limetokea kuteka hisia za wengi katika kipindi cha masaa 48. Taarifa ambazo zimetapakaa kwenye vyombo ya habari zinasema kuwa Dar es salaam Young Africans imekamilisha usajili wa Yondani huku nakala ya mkataba wake alioingia na klabu hiyo ukionyesha kuwa amesaini kuichezea Yanga kwa miaka miwili huku akitia kibindoni kiasi cha Milioni 30 huku mshahara wake ukiwa laki nane kwa mwezi. Upande wa pili wa sinema hii ambao ni klabu anayodaiwa kutoka Yondani ya Simba Sports unadai kuwa Yondani aliongeza mkataba wake wa awali na klabu hiyo kabla hata y... more »

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Shadaka at Shaffih Dauda in Sports. - 1 day ago
SIMBA SPORTS CLUB P.O.BOX 15318 | TEL+255 222183330 |FAX +255 222183330 |MSIMBAZI/MCHIKICHI STREET | DAR ES SALAAM | TANZANIA | EMAIL simbasportsclub@yahoo.com|WEBSITE www.simba.co.tz| AFFILIATED TO TFF, DRFA and IDFA Simba Sports club imesikitishwa na kitendo cha Young Africans kuvunja taratibu za usajili kwa kumrubuni mchezaji wake Kelvin Patrick Yondani kwa kuzungumza naye na baadae kwa ushahidi wa picha kuonekana wakimuandikisha makaratasi ambayo baadae imeripotiwa na vyombo vya Habari kwamba alikuwa akisaini mkataba wa kui... more »