Wednesday, January 4, 2012

Rwanda waliwaua raia 26 mashariki mwa KONGO


Jamhuri ya kidemokrasia yaCongo
Jamhuri ya kidemokrasia yaCongo
Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo linadai kuwa wapiganaji kutoka Rwanda waliwaua raia 26 mashariki mwa nchi hiyo.
Jeshi hilo la Congo limesema mashambulio hayo yalitekelezwa na waasi wa kundi la FDLR, mapema wiki hii.
Mauaji hayo yanawakilisha baadhi ya mapigano makali zaidi kutekelezwa na kundi hilo kwa miezi sasa.
Jeshi la Congo limesema litaimarisha ulinzi katika eneo hilo.
Miongoni mwa maeneo yaliyoshambuliwa ni Bamuguma Sid, mkoa wa kivu ya kusini.
Mbali na kuwauwa watu, wapiganaji wa FDLR inadaiwa kupora mali wakaazi wa eneo hilo.
Walionusurika shambulio hilo wameripotiwa wakisema kuwa walilengwa kwa sababu jamii kutoka eneo hilo linadhaniwa kuunga mkono kundi la wanamgambo katika eneo hilo, na kwamba walikuwa wanaadhibiwa kwa hilo.
Wapiganaji wa FDLR wamelaumiwa kwa kutekeleza ubakaji na mauaji , licha ya kuwepo kwa wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa katika eneo hilo.

Ndugai amshukia Frederick Sumaye

Ndugai amshukia Frederick Sumaye  Send to a friend
Wednesday, 04 January 2012 21:09
0digg
Naibu Spika wa Bunge,Job Ndugai
ASEMA HANA USAFI WA KUBEZA NYONGEZA YA POSHO
Fredy Azzah
NAIBU Spika wa Bunge, Job Ndugai amemjia juu Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye kuhusu kauli yake ya posho za wabunge, akisema hakupaswa kuitoa kwani aliwahi kufanikisha kupitishwa sheria ya malipo kwa viongozi wakuu wastaafu ili kujinufaisha akistaafu.Juzi, Sumaye pamoja na mambo mengine, alizungumzia mwelekeo wa taifa kwa sasa na kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2015 huku akisema mpango wa ongezeko la posho za wabunge unapaswa kuachwa kwani unaweza kufanya makundi mengine ya utumishi wa umma kudai nyongeza.

Kauli hiyo ilijibiwa vikali jana na Ndugai ambaye aliwatahadharisha viongozi wastaafu kuwa makini na kauli wanazotoa na kuwataka wale ambao wanataka urais wa 2015 ikiwa ni pamoja na Sumaye waseme sasa badala ya kuwababaisha Watanzania kwa kuzungumza mambo mbalimbali ili wawapende.

Alisema wakati Sumaye anazungumzia posho za wabunge, sheria ya kuwalipa viongozi wastaafu mafao ilipitishwa wakati akiwa kiongozi wa shughuli za Serikali bungeni na hakuipinga kwa kuwa alikuwa anajiandalia mazingira ya kustaafu.
“Kwa sasa analipwa asilimia 80 ya mshahara wa waziri mkuu aliyepo madarakani, ni fedha nyingi kuliko hata mshahara wa Naibu Spika (Ndugai kwa sasa), wakati sheria hii inapitishwa alikuwa kiongozi wa shughuli za Serikali bungeni (Waziri Mkuu), alikuwa anajiandalia mazingira ya kustaafu,” alisema Ndugai na kuongeza:

 “Sitaki kuendelea kusema sana jinsi ambavyo ananufaika, lakini ninachosema viongozi wastaafu duniani kote inatakiwa wawe makini na kauli zao. Wakianza kwenda kwenye vyombo vya habari na kusema maneno haya haipendezi.”
Alifafanua kwamba badala ya kuzungumzia posho za wabunge pekee ni vyema pia likazungumziwa suala la posho kwa viongozi wote wa umma.

“Kwa watu wanaotaka kugombea urais mwaka 2015 ni bora waseme sasa. Waache kutubabaisha Watanzania… nasema viongozi wastaafu lazima wawe makini kwa kauli zao, mimi Sumaye ninamheshimu sana na ninatambua haki yake ya kikatiba ya kujieleza,” alisema na kumshauri kuwa makini na kauli zake anapozungumza juu ya Bunge kwa sababu yeye pia alikuwa sehemu ya mhimili huo.

“Yeye ni kama mchezaji mstaafu wa timu hii (Bunge), inatakiwa awe makini sana hawezi kuizungumzia hii timu kama mshabiki mwingine,” alisema Ndugai.

Ndugai alisema posho zilikuwepo tangu enzi za Sumaye akiwa mbunge, naibu waziri na hatimaye waziri mkuu na kwamba kama hoja ni kiasi cha fedha... “Aseme ni kiasi gani wabunge wanapaswa kulipwa.”
Sumaye aliingia bungeni kwa mara ya kwanza mwaka 1985 baada ya kushinda ubunge katika Jimbo la Hanang na mwaka 1987, aliteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Kilimo na Maendeleo ya Mifugo hadi mwaka 1994 alipoteuliwa kuwa waziri kamili katika wizara hiyo.

“Mimi nakwambia kitu ambacho nakijua na wakati huo nilikuwa bungeni kama mbunge na Sumaye alikuwa akizipokea hizi posho, Rais (Ali Hassan) Mwinyi aliwahi kusema kila zama na kitabu chake, hebu na yeye (Sumaye) atuache na sisi tuandike kitabu chetu,” alisema Ndugai.

Dk Bana abeza
Akizungumzia kauli ya Sumaye, Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Benson Bana alisema mambo aliyozungumza si mapya na huku akimtaka kutazama kila neno linalotoka mdomoni mwake.

Dk Bana alisema kauli ya Sumaye kuhusu matumizi ya taasisi ya urais, inaweza kutafsiriwa kwamba inatokana na yeye kuwa na uchungu wa kuikosa alipogombea na Rais Jakaya Kikwete katika uchaguzi wa ndani wa CCM.

Sumaye katika kinyang’anyiro cha kupenya kura za maoni kwa ajili ya kupeperusha bendera ya CCM baada ya Mkapa, alishika nafasi ya tano na kushindwa kuingia hata tatu bora ambayo waliingia Rais Kikwete, Dk Salim Ahmed Salim na Profesa Mark Mwandosya.

“Kwanza anavyozungumzia taasisi ya urais hatujui kama ni hii au ni zilizopita, lakini ikumbukwe kuwa aligombea nafasi hiyo akaikosa kwa hiyo kuna uwezekano kuwa ni roho inamuuma,” alisema Bana.

Kuhusu suala la rushwa katika uchaguzi alisema: “Suala hili lilikuwepo kwa muda mrefu na limepigiwa sana kelele, yeye hakuweza kumshauri Rais (Benjamin) Mkapa kuwa watunge sheria ya kupambana na hali hii, lakini sasa hivi Serikali imejaribu inatakiwa aipongeze kwa hilo,” alisema Dk Bana.

Alisema hata baada ya kuundwa kwa sheria hiyo, viongozi wengi wakubwa ikiwa ni pamoja na wale wastaafu hawaonekani kuipigia debe.

Dk Bana alisema kuundwa kwa sheria ni jambo moja na kinachotakiwa sasa ni utekelezaji wake kufanyiwa kazi.
Alisema pia ingekuwa jambo jema endapo viongozi wastaafu wangeunda taasisi yao ili waweze kushauri Serikali ili busara zao ziweze kutumika vyema huko... “Yeye ana nafasi kubwa sana ya kuzungumza haya mambo ndani ya chama na pia hata kumshauri Rais moja kwa moja.”

Kuhusu suala la posho kwa wabunge, alisema Sumaye alilizungumza vizuri na inatakiwa aungwe mkono na watu wengine.

Alichosema Sumaye
Akizungumza kupitia kipindi cha dakika 45 kinachorushwa na Kituo cha Televisheni cha ITV, Sumaye alisema ongezeko la posho za wabunge linaweza kuchochea makundi mengine kama wanajeshi, polisi, Mahakama na walimu nao kutaka nyongeza, hivyo kumweka Rais katika wakati mgumu kufanya uamuzi.

“Mwanasiasa mzuri akifanya jambo akiona limewaudhi wananchi anatakiwa aliache, lakini pia kwenye hili huu mkanganyiko wa Spika na Katibu wake na huu ukimya wa Ikulu ni tatizo, tungependa waseme ili umma ujue hali ikoje?” alisema Sumaye.

Alisema hatua ya Bunge kujipandishia posho ya kikao kutoka Sh70,000 hadi Sh200,000 kwa siku haliingii akilini na kwamba, inakiuka utaratibu uliowekwa na Serikali katika kulipa gharama kwa maofisa wake ikiwa ni pamoja na gharama hizo za fedha za kujikimu.

“Siyo kwamba napinga posho, wabunge wanastahili posho, lakini kwa kweli kujiongezea kutoka Sh70,000 hadi Sh200,000 siyo sahihi,” alisema Sumaye.

Alisema wakati alipoteuliwa na Rais Benjamin Mkapa kwa Awamu ya Pili kushika wadhifa wa Waziri Mkuu, aligoma kwa sababu alikuwa amekwaruzana na wabunge kuhusu nyongeza ya posho.

“Nilimwambia wabunge watanikataa kwa sababu nimegombana nao sana juu ya suala la posho lakini akasema lazima uwe na mimi ndipo nikakubali, lazima hili suala liangaliwe mara mbilimbili… leo wabunge mmejiongezea kesho jeshi, polisi na walimu nao watataka, tutafanyaje tusifanye mambo ambayo yatamuweka Rais pabaya,” alisema Sumaye.

Alisema posho ni jambo ambalo kwa sasa limekuwa tatizo kwa serikali na kwamba imefika wakati ofisi za Serikali zimehamia hotelini, lengo likiwa ni watumishi wa umma kutafuta mwanya wa kulipana posho.

Hamad Rashid ang'olewa CUF


Hamad Rashid ang'olewa CUF  Send to a friend
Wednesday, 04 January 2012 21:01
0digg
Mbunge wa Wazi Zanzibar Hamad Rashid Mohamed (katikati),akiwa na wanachama wenzake katika kikao cha Baraza Kuu la Chama Cha Wananchi (CUF)mjini Zanzibar jana, kabla ya kuanza kwa kikao cha kuamua hatma yao ndani ya Chama hicho, ambapo anatuhumiwa yeye na wenzake 13 kukisaliti Chama. Picha na Jackson Odoyo
Aziza Masoud na Talib Ussi, Zanzibar
HATIMAYE Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid Mohamed na wenzake watatu wamefukuzwa uanachama wa CUF kuanzia jana. Hatua hiyo ilichukuliwa na zaidi ya robo tatu ya wajumbe wa Baraza Kuu la chama hicho katika kikao chake kilichofanyika hapa.

Uamuzi huo umekata mzizi wa fitina wa hatma ya Hamad na washirika wake hao kisiasa ndani ya chama hicho, baada ya kuibuka mvutano wa muda mrefu kati yake na uongozi wa juu.

Mvutano huo uliochomoza zaidi baada ya Hamad kutangaza kuwania nafasi ya Katibu Mkuu inayoshikiliwa na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharrif Hamad.

Hata hivyo, hatua hiyo imepingwa na Hamad ambaye ameiita kuwa ni ya kihuni kwani imekiuka amri ya Mahakama iliyotangaza kusitishwa kwa kikao kilichochukua uamuzi huo.

Naibu Katibu Mkuu wa CUF (Bara), Julius Mtatiro alithibitisha kuvuliwa uanachama kwa Hamad na kuwataja wengine walioondolewa pia kuwa ni Mjumbe wa Baraza Kuu (Tanga), Doyo Hassan Doyo, Mjumbe wa Baraza Kuu (Pemba), Shoka Khamis Juma, Mjumbe wa Baraza Kuu Unguja, Juma Saanane na Mjumbe wa Baraza Kuu (Mbeya), Yassin Mrotwa.

“Kwa mujibu wa katiba ya chama, wasioridhika na uamuzi huo wanaweza kukata rufaa kwenye mkutano mkuu wa taifa,” alisema.

Naibu Katibu Mkuu CUF Zanzibar, Ismail Jussa akizungumza jana jioni na Idhaa ya Kiswahili ya Redio Ujerumani (DW), alisema haoni kama hatua hiyo ya kuwafukuza wanachama hao akiwamo Hamad ambaye aliwahi kuwa Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni kunaweza kuhatarisha mustakabali wa chama hicho.

“Ni kweli Hamad ametoa mchangao mkubwa ndani ya chama. Lakini wakati mwingine unapima faida na hasara sasa hivi Hamad alikuwa anaelekea kuvuruga chama,” alisema Jussa

Hamad: Ni uamuzi wa kihuni

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kikao hicho, Hamad alisema anashangazwa na kiongozi wa nchi (Maalim Seif), kushindwa kuheshimu amri ya Mahakama na kuendelea na kikao ambacho ilikuwa imeamuru kisitishwe.

“Kiongozi wa nchi anakaidi uamuzi wa mahakama... uamuzi huu mimi nauita ni uamuzi wa kihuni, nimekwenda kwenye kikao naulizwa maswali ambayo wao wamejipanga na mashahidi wao mimi sijajipanga, sina shahidi nawaambia wanipe maswali ili nipate muda wa kuyajibu na kuandaa mashahidi kama wao hawataki, sasa demokrasia ipo wapi hapo?” alisema Hamad.

Hamad alisema hati ya kusimamishwa kwa kikao hicho ilifika ukumbini hapo saa 6:10 mchana, lakini wajumbe wa kikao hicho walionekana kuipuuza na kuendelea nacho na hati iliyopelekwa makao makuu ya Dar es Salaam saa 2:00 jana ilikatiliwa kupokewa akidai kwamba ni kwa agizo kutoka kwa viongozi wakuu.

Alisema hati ya mahakama inaonyesha kwamba wanatakiwa kwenda mahakamani Februari 14, mwaka huu na kusema kwamba uamuzi wa kuaminika utatolewa huko kwani katika chama hicho wanachama wengine wanaonekana hawana nguvu kama katibu mkuu.

Alisema wanachama wote wa CUF wanapaswa kufurahi kwani hajaumizwa na uamuzi kwa kuwa viongozi wake wamekuwa wakionekana kuhubiri haki sawa huku wakienda tofauti na msimamo wa chama.

“Maalim Seif kila siku anaonekana anahubiri haki sawa kumbe hana lolote, anakandamiza tu watu kwa kuharibu chama na kutoa maamuzi kibabe. Mimi sipo tayari kuburuzwa, wakitaka tuelewane haki wanayoihubiri iwe inatendeka kweli,” alisema Hamad.

Kwa upande wake, Shoka Khamis ambaye alikuwa Mbunge wa Micheweni, Kaskazini Pemba katika Bunge la Tisa, alisema kwa mujibu wa katiba ya CUF hamjui aliyemtuhumu kwani haiwezekani mtu asomewe shtaka bila kujua anayemtuhumu.

“Nimejifundisha mengi sana CUF mazuri na mabaya, lakini leo kwa sababu wamenifukuza ngoja niseme mabaya, CUF sisi ni CCM B kama wanavyosema wenzetu. Chama kina sifa mbaya ya kufukuza watu, lakini anayefukuza wenzake, Seif Sharif Hamad yeye anajiona kama mungu hafanyi makosa,” alisema Shoka.

Alisema hawapo tayari kujiunga na chama chochote cha siasa kama maneno yanavyosambazwa kuwa watahamia Chadema. Alisema watafufua Chama Cha Wananchi (CCW) ambacho kiliungana n Kamahuru na kuipata CUF.

“Tuna mpango wa kuanzisha chama kingine kwani CUF kwa sasa kimeshakuwa chama cha mtu ambaye ni Seif na siyo cha wananchi kama kinavyojulikana katika siasa za nchi hii,” alisema Shoka.

Hamad na hujuma

Desemba 27, mwaka jana Hamad aligoma kuhojiwa na Kamati ya Maadili na Nidhamu, akitoa sababu tano huku akiibua tuhuma nzito za kunasa waraka wa mawasiliano uliotumwa kwa barua pepe na Maalim Seif kwenda kwa Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba ukionyesha mpango wa kumshughulikia.

Sababu ya pili, alisema baadhi ya walioteuliwa katika kamati hiyo ya Nidhamu na Maadili walikwisha mtuhumu hadharani na kumtia hatiani hivyo, kikao hicho kisingeweza kumtendea  haki.

Alitaja sababu nyingine ya kukataa kuhojiwa kuwa ni kutoelezwa tuhuma zake hasa vifungu vya Katiba alivyodaiwa kuvikiuka.

Pia alitaka apewe hadidu za rejea za kikao kilichounda Kamati ya Nidhamu na Maadili kwa sababu haipo kikatiba, hakuna chombo kama hicho. Aligoma pia kuhudhuria kikao hicho kwa kuwa tayari alibaini njama za kumshughulikia zilizosukwa na Maalim Seif na Lipumba.

Hamad Rashid alijikuta kwenye mgogoro huo baada ya kutangaza dhamira yake hiyo ya kugombea nafasi ya katibu mkuu mwaka 2014.

Kuanzia hapo akajikuta ameingia kwenye mgogoro na chama hicho kiasi cha kunusurika kushambuliwa na watu wasiojulikana wakati akigawa misaada katika matawi ya chama hicho, Kata ya Manzese.

SIKU 75 BAADA YA KIFO CHA GADDAFI




Mwandishi Wetu na Intaneti
Ilishaonywa kuwa Libya haiwezi kuwa na amani baada ya kifo cha aliyekuwa kiongozi wao, Muammar Gaddafi na sasa hali ya hatari imeanza kujionesha kutokana na hasira kali walizonazo wananchi.
Siku 75 zimepita tangu Gaddafi alipokamatwa, kuteswa na kuuawa kabla ya kuzikwa kwa siri, lakini sasa imeibuka hali ya hatari kutokana na wananchi wa Libya kuanza kudai damu ya kiongozi huyo aliyeitawala nchi hiyo kwa miaka 42.
Mwandishi wa Habari wa Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), Wyre Davies, aliandika ripoti ya uchunguzi wake nchini Libya baada ya kifo cha Gaddafi kuwa Jiji la Sirte, limetanda giza ya chuki dhidi ya Serikali ya Baraza la Mpito (NTC).
Katika ripoti yake, iliyohusisha mahojiano na wananchi waliokuwa tayari kwa mapambano, wakazi wa Sirte wametoa agizo kwenda NTC kuwa ni lazima waoneshe kaburi la Gaddafi pamoja na la mwanaye, Muttasim ambaye alizikwa naye siku moja.
Ripoti hiyo ilieleza pia kuwa wananchi wanataka damu ya Gaddafi ifidiwe, vinginevyo Libya haitakalika abadan!
 Mwandishi huyo aliandika kuwa chuki ya wananchi wa Sirte ni kubwa kwa NTC kutokana na maelezo wanayotoa kwamba Gaddafi alikuwa anapambana kuwalinda, wakati waasi wakisaidiwa na vikosi vya Jeshi la Kujihami la Nchi za Magharibi (Nato), waliendesha mauaji ya raia bila tahadhari.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Sirte, Dk. Ahmed Hassan, amezungumza ndani ya ripoti hiyo kuwa maisha ya Walibya yameharibika kwa kiasi kikubwa.
Alisema, enzi za Gaddafi alisaidia maeneo mengi ya kimaisha kwa wananchi wa Libya lakini sasa hivi imekuwa tofauti.
“Gaddafi alitusaidia makazi, wao NTC wameyaharibu. Gaddafi alitulinda raia wa Libya, NTC wameua raia, hawafai hata kidogo,” alisema Dk. Hassan ambaye yeye na familia yake yenye mke na watoto watano, wanaishi kwenye hema baada ya nyumba yao kuharibiwa na milipuko ya mabomu.
Alihoji: “Nitazame, mimi ni mhadhiri wa chuo kikuu hapa. Nilifanya kosa gani mpaka nikastahili maisha haya mabovu?”
Dk. Hassan alifafanua kuwa Walibya walikuwa wanaishi kwa amani, matumaini, furaha na upendo lakini NTC wamevuruga misingi yote bora iliyowekwa na Gaddafi.
“Kwa sasa mimi sijali. Tutaona kitakachotokea. Sioni kitu kinachoweza kunishawishi kuamini kwamba NTC wataifanya Libya kuwa mpya yenye matumaini,” alisema.
Katika ripoti hiyo, mwandishi huyo wa BBC ameeleza kwamba hasira za wananchi na mgawanyiko uliopo, vinafanya amani na umoja wa kitaifa wa Libya viwe ni ndoto kupatikana.
Imezidi kuelezwa kwenye ripoti hiyo kwamba wananchi wao kwa wao wamegeukana, wale waliokuwa wanaunga mkono NTC wanachakazwa na wengi ambao hawakukubaliana na hatua zilizochukuliwa dhidi ya Gaddafi.
Inaelezwa kuwa NTC kwa kulitambua hilo, imekuwa ikiingilia kati na kuwadhibiti wananchi waliokuwa wanaamini katika huduma ya Gaddafi.
Inabainishwa kuwa wananchi 30,000 wanaoishi kwenye mji wa kaskazini ya Jiji la Mistrata, wametimuliwa kwenye makazi yao, hivyo hawana makazi kwa sasa.
Msichana, Najia Waks, mkazi wa jiji hilo la tatu kwa ukubwa Libya, alisema kuwa wapiganaji wa NTC wamewafanyia udhalilishaji wa hali ya juu, kwa hiyo hawatawasamehe hata kidogo.
“Hawawezi kujirudi na hawawezi kuja tena. Wametufanyia mambo mengi ya kuumiza. Ni mambo ya kutisha mno.
“Wamebaka wanawake, vijana walichukuliwa usiku na mpaka sasa hawajulikani walipo,” alisema Najia, mwenye asili yake kwenye Mji wa Tawergha, Mistrata.
Mwanamke, Umm Saber, akiwa kwenye Kambi ya Wakimbizi ya Ghost, alisema, Libya hakuna amani na hali iyopo sasa hivi, nchi haina msimamizi sahihi.
“Tunanyanyasika tu na kuteswa. Wanawake tunageuzwa watumwa wa ngono na wapiganaji wa NTC kwa sababu hawana maadili. Ona maisha yalivyokuwa magumu na bei za vitu zimepanda, wakati Gaddafi alirahisisha bei za bidhaa.
“Alilipa marupurupu na mishahara hata kwa wasio na kazi. NTC hatuoni hayo. Tunaambiwa inajengwa Libya mpya yenye umoja na amani, hayo mbona hayatekelezwi, badala yake tunashuhudia ukandamizaji na utesaji wa wananchi?
“Ikijulikana kuna sehemu watu walikuwa wanamuunga mkono Gaddafi wanauawa, tunakwenda wapi? Bila shaka NTC ni wahalifu wa kivita. Mimi nitaungana na wanaharakati watakaojitoa kudai damu ya Gaddafi, tutapambana usiku na mchana,” alisema Umm.
Gaddafi, aliuawa Oktoba 20, 2011 baada ya kukamatwa na wapiganaji (waasi) wa NTC kwa kushirikiana na Nato.
Kukamatwa kwa Gaddafi kulikuja baada ya mapigano ya muda mrefu kati ya waasi wakisaidiwa na Nato dhidi ya kiongozi huyo aliyekuwa amegoma kuachia madaraka.

Sumaye atema cheche


Sumaye atema cheche  Send to a friend
Tuesday, 03 January 2012 20:13
Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye
APONDA POSHO MPYA ZA WABUNGE, ASEMA KUJIVUA GAMBA NI KITANZI KWA CCM UCHAGUZI MKUU 2015
Waandishi Wetu
WAZIRI Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye amezungumzia mwelekeo wa taifa huku akionya kuwa nyongeza za posho zisizofuata utaratibu kwa watumishi wa umma ni hatari na ni utawala mbaya kwa nchi.Alisema suala la posho ni jambo ambalo sasa limekuwa tatizo kwa Serikali na kuwa imefika wakati ofisi za Serikali zimehamia hotelini lengo likiwa ni watumishi wa umma kutafuta mwanya wa kulipana posho.

“Ndiyo maana watu wa TRA (Mamlaka ya Mapato Tanzania) wanakusanya fedha nyingi, lakini ni fedha kidogo sana zinazokwenda kwenye huduma za jamii. Nadhani hili ni tatizo na ni utawala mbaya kabisa, lazima kuwepo mabadiliko kama kweli tunataka kuisaidia nchi yetu,” alisema Sumaye.Kuhusu posho za wabunge, Sumaye alisema ni jambo la hatari kwani ikiwa wabunge watalipwa viwango vya posho vilivyotangazwa, linaweza kuvuruga amani ya nchi.

Sumaye alisema hayo katika kipindi cha dakika 45 kinachotushwa na Kituo cha Televisheni cha ITV. Alisema ongezeko la posho za wabunge linaweza kuchochea makundi mengine kudai akitolea mfano wa wanajeshi, polisi, Mahakama na walimu jambo ambalo alisema litamweka Rais katika wakati mgumu kufanya uamuzi.

“Mwanasiasa mzuri akifanya jambo akiona limewaudhi wananchi anatakiwa aliache, lakini pia kwenye hili, huu mkanganyiko wa Spika na Katibu wake na huu ukimya wa Ikulu ni tatizo. Tungependa waseme ili umma ujue hali ikoje,” alisema Sumaye.  Alisema hatua ya Bunge kujipandishia posho ya kikao kutoka Sh70,000 hadi Sh200,000 kwa siku haliingii akilini na kwamba linakiuka utaratibu uliowekwa na Serikali katika kulipa gharama kwa maofisa wake ikiwa gharama hizo ni zaidi ya kiwango cha fedha za kujikimu zilizowekwa.

“Siyo kwamba napinga posho. Wabunge wanastahili posho, lakini kwa kweli kujiongezea kutoka Sh70,000 hadi Sh200,000 siyo sahihi,” alisema Sumaye.Alisema wakati alipoteuliwa na Rais Benjamin Mkapa kwa Awamu ya Pili kushika wadhifa wa Waziri Mkuu, aligoma kwa sababu alikuwa amekwaruzana na wabunge kuhusu nyongeza ya posho.

“Nilimwambia wabunge watanikataa kwa sababu nimegombana nao sana juu ya suala la posho lakini akasema lazima uwe na mimi ndipo nikakubali. Lazima hili suala liangaliwe mara mbilimbili, leo wabunge mmejiongezea kesho jeshi, polisi na walimu nao watataka, tutafanyaje? Tusifanye mambo ambayo yatamuweka Rais pabaya,” alisema.

Kitanzi cha Gamba Akizungumzia Uchaguzi Mkuu ujao wa 2015, alikitahadharisha chama chake cha CCM akikitaka kutekeleza kwa vitendo mkakati wake wa kujivua gamba, la sivyo utageuka na kuwa kitanzi kwake kwenye uchaguzi huo.
Alisema kama CCM kina nia ya dhati katika kupambana na kuhakikisha kinatokomeza rushwa na ufisadi unaoonekana kuwa kikwazo katika maendeleo ya taifa, lazima kiwavue gamba walioshindwa kujivua wenyewe... “Wasipojivua hilo koti, itabidi watu wengine wawasaidie kulivua,” alisema Sumaye.

Alisema hivi sasa suala hilo limeonekana kama vita dhidi ya pande mbili ndani ya chama hicho, ingawa upande unaotetea ufisadi, hautoki moja kwa moja na kujionyesha. “Lakini ukiangalia sana suala la rushwa utaona kuwa hatujapambana nalo vya kutosha, kinachomfanya mtu awe mla ruswa ni cheo, ukimtoa kwenye hiyo nafasi pamoja na fedha zake hatoweza kufanya chochote,” alisema Sumaye.

Alisema chama hicho ni lazima kihakikishe kinatokomeza rushwa wakati wa uchaguzi wake wa ndani, vinginevyo alisema wananchi watakiangusha.  Matumizi mabaya ya urais Sumaye alisema rushwa, ufisadi na matumizi mabaya ya urais, ni moja ya sababu inayofanya nchi nyingi za Afrika zizidi kuwa masikini.

Alisema hali hiyo haipo kwa viongozi wa sasa pekee, bali hata kwa wale waliowatangulia isipokuwa wale tu waliogombea uhuru wa mataifa hayo. “Matumizi mabaya ya taasisi ya urais ni tatizo, mtu akiwa Rais anafanya taasisi hiyo inakuwa mali yake alikuwa ni mtu wa kawaida lakini ghafla anakuwa tajiri anataka na watoto wake pia wawe matajiri,” alisema na kuongeza:

 “Urais siyo mali ya mtu na familia yake, dhamana hiyo unapewa na wananchi na inatakiwa uwatumikie wao, viongozi kama Nyerere, Kenyatta, Mandela mitizamo yao ilikuwa tofauti sana na viongozi wa sasa,” alisema. Alitoa mfano wa Rais wa Misri aliyepinduliwa Hussein Mubarak ambaye alikuwa na utajiri wa zaidi ya Dola 70bilioni na mtoto wake akiwa na fedha maradufu ya hizo. “Nimesema haya kwa ujumla jinsi nchi nyingi za Afrika zilivyo lakini haya ni matatizo ambayo hata hapa kwetu yapo, Rais Kikwete ameyakuta, atakuja mwingine atayakuta, tusipopiga vita rushwa na ufisadi, hatutakwenda popote,” alisema Sumaye.

Maelezo hayo ya Sumaye, yalitokana na swali aliloulizwa kwamba, kwa nini baadhi ya nchi ikiwemo Korea Kusini miaka ya 1960 zilikuwa karibu sawa kimaendeleo na nchi nyingi za Afrika lakini kwa sasa nchi hizo zimeendelea maradufu huku Afrika ikizidi kuwa masikini.

Rushwa na uchaguzi Sumaye alisema: “Kama tunataka viongozi bora wa kuliongoza taifa hili, lazima tupambane na rushwa katika uchaguzi... Nasema fedha za kuhonga zilizowekwa kwenye bahasha lazima tuhakikishe zinatokomezwa, tusipofanya hivyo tutaondolewa, nadhani ni wakati wa kurudi kwenye enzi za Tanu na ile CCM ya zamani, mtu unazungumza watu wanakuchagua bila kutoa hongo, tusipofanya hivyo wananchi watafanya uamuzi tofauti.”
Alisema watu wanaotaka madaraka kwa kuwanunua wapiga kura lazima wadhibitiwe kwani hali hiyo ikiachwa nchi itaangamia kwa ubinafsi.

Sumaye alilalamika kuwa kuna tatizo ndani ya CCM na Serikali yake ya kupambana na wanaopambana na rushwa badala ya kuwaunga mkono... “Hilo ndilo tatizo kubwa, wale wanaopambana na ufisadi na rushwa sasa wanageuzwa kuwa kambi fulani inayotaka kuiondoa kambi nyingine madarakani. Huo ni ujinga wote tunatakiwa kupambana tukiwa kitu kimoja. Inaonyesha kuna mapambano ya kudhoofisha wale wanaopambana na ufisadi.”

 Alikinyooshea kidole CCM akisema kuwa chaguzi zake nyingi zimejaa rushwa huku wala rushwa wakiachwa bila kukamatwa.   “Wakati wa uchaguzi fedha zinagawanywa lakini kuna watu wanakamatwa na wengine hawakamatiki. Lazima kama Taifa tupambane. Rushwa ikiendelea kuwepo tutakuwa na nchi isiyo na maendeleo,” alisema.

Sumaye aliongeza kuwa, vyama vya siasa vipambane na watu wanaotaka madaraka kwa njia ya fedha kwani kama wataingia madarakani wataanza kujineemesha wao badala ya kuwatumikia wananchi.

 Urais 2015 Kuhusu wanaotaka kugombea urais mwaka 2015 Sumaye alisema alimradi hatafuti nafasi ya kumuondoa Rais aliyepo madarakani wala haleti vurugu, haoni shida kwa mtu yeyote kuota au kutangaza kwamba mwaka 2015 atagombea nafasi hiyo. Alisema kibaya ni endapo mtu huyo atafanya hivyo huku akiwachafua wenzake, jambo ambalo amesema kwa kiasi fulani sasa linajitokeza.

“Tatizo ni pale watu wanapojaribu kuchafua watu, hilo ndiyo tatizo, nafikiri lipo... mimi bado sijatangaza na bado sijaamua nikiamua nitasema. Kuna tatizo kwamba ukisema chochote wanasema huyu anautaka urais sasa ina maana kwamba wanaotaka urais wanyamaze, au wasipumue hata kidogo?”

 Uongozi wa Mkapa Akizungumzia changamoto za uongozi wa Serikali ya Awamu ya Tatu ya Mkapa, alisema walifanya kazi kubwa ya kuinua uchumi wa nchi kwani walipoanza kazi nchi ilikuwa katika hali mbaya.

“Wakati Rais Mkapa anaingia madarakani ilikuwa ngumu sana. Pili marafiki wa nje, taasisi za fedha zilitukataa kama nchi. Hata mishahara ilikuwa ngumu kupata wakati huo kima cha chini kilikuwa ni Sh17,000,” alisema na kuongeza:    “Hatukuweza kuingia kwenye janga la kuchapisha fedha. Kuchapisha fedha ni janga la kiuchumi. Ukiona nchi inachapisha fedha ujue imeporomoka kiuchumi na ndiyo maana sisi tulihakikisha kuwa hatuingii kwenye kuchapisha fedha,” alisema.

Kuhusu mchango wa viongozi wastaafu katika kuleta maendeleo ya nchi, Sumaye alisema Serikali imewatenga viongozi wastaafu japo wapo wanaotumiwa.

“Kama utakumbuka Mzee Mkapa wakati wa World Economic Forum pale Mlimani City alilalamika akisema tatizo kubwa la Afrika ni kutotumia hazina ya viongozi wa Afrika. Akasema hamtutumii lakini wenzenu wa nje wanatutumia sana na wanatufaidi sana.

“Hilo ni tatizo la Afrika na ni tatizo la Tanzania kwa sababu tunayo hazina kubwa ya viongozi ambao tungeweza kuwatumia vizuri sana. Lakini hawatumiki. Ili niweze kusaidia, lazima awepo mtu wa kukwambia hebu fulani njoo hapa au wewe useme hebu nimwone fulani lakini bila ya hivyo hakuna namna ya kusaidia.”  

Wawili Hatiani kwa mauwaji


Wawili Hatiani kwa mauwaji

 3 Januari, 2012 - Saa 16:02 GMT
Baada ya miaka 18 ya upelelezi na kuendesha kesi kuhusu mauwaji ya kijana mweusi mjini London, Stephen Lawrence, wanaume wawili wamepatikana na hatia.
Gary Dobson na David Norris
Gary Dobson na David Norris
Gary Dobson na David Norris wamepatikana na hatia na jopo la mahakama baada ya kesi hio kutegemea ushahidi wa kitaalamu.
Wataalamu wa uchunguzi wa damu na alama kama hizo waligundua alama ya damu kwenye koti la Dobson ambalo bila shaka halingepatikana bila kumkaribia marehemu.
Wakati akiondolewa mahakamani, aliliambia jopo kua wamemhukumu mtu asiye na hatia. Hukumu itasomwa siku ya jumatano.
Stephen Lawrence
Stephen Lawrence
Wazazi wa marehemu Stephen, Doreen na Neville, waliangua kiliyo jopo lilipotangaza kua watuhumiwa wamepatikana na hatia. Duwayne Brooks, rafiki mkubwa wa Stephen Lawrence aliyekua naye waliposhambuliwa, alituma ujumbe kupitia mtandao wa Tweeter akisema, hatimaye, sheria imetendeka'
Mamake Dobson, Bi.Gary Dobson, aliyeiambia mahakama kua mwanawe alikua nyumbani wakati wa mauwaji, aliangua kilio mahakamani kufuatia tangazo la watuhumiwa kupatikana na hatia.
Upelelezi wa kwanza uliofanywa na polisi ulishindwa na kupelekea Polisi ya mji wa London kutuhumiwa kama Idara inayoendesha ubaguzi wa rangi.
Stephen Lawrence alikua mwenye umri wa miaka 18 alipouawa kwa kisu akiwa karibu na kituo cha basi cha Eltham, London ya kusini mnamo mwezi April mwaka 1993. Polisi walitambua watu watatu ambao baadaye walitajwa katika ripoti ya uchunguzi kama washukiwa wakuu.
Hadi wakati huo kulikuepo mfululizo wa mapungufu ya polisi kwa kushindwa kukusanya ushahidi wa kutosha mbara mbili, wa kwanza uliowasilishwa na wazazi wake Stephen Lawrence, Doreen na Neville Lawrence.
Lakini katika kuichunguza kesi hio kwa mda wa miaka minne, wataalamu wengine wa kupeleleza ushahidi waliweza kugundua ushahidi ulioweza kuwaunganisha washukiwa na mauwaji - ushahidi ambao ulia mikononi mwa polisi kwa kipindi kirefu.
Ushahidi huo wa alama za damu, nyuzi za nguo na unywele wa marehemu - vilipatikana kwenye nguo za washukiwa zilizotekwa tangu mwaka 1993.
Wataalamu wa upelelezi wa ushahidi walifanikiwa kugundua ushahidi huo kwa kutumia mitambo ya kisasa ambayo wakati ule havikuwepo.
Dobson, mwenye umri wa miaka 36, na Norris,akiwa na umri wa miaka 35, walikanusha madai ya kuua. Walidai kua damu hio ilichanganyika na nguo zao kutokana na kuchanganywa na ushahidi kupitia kipindi cha miaka mingi.
Wapelelezi walitumia mda kuchunguza jinsi ushahidi huo ulivyozungushwa na jinsi ulivyohifadhiwa kuondoa shaka ya uwezekano wa kuchanganywa kama walivyodai watuhumiwa.
Gary Dobson alikamatwa na kufungwa jela mnamo mwaka 2010 kwa kushiriki biashara ya kuuza mihadarati. Yeye ni miongoni mwa kundi dogo la wanaume waliohusishwa na uhalifu mmoja baada ya Mahakama ya rufaa kuzima ombi lake la rufani mnamo mwaka 1996.
Katika mahojiano marefu na BBC, Mamake Stephen Lawrence, Doreen alisema: "siwezi kuwasamehe vijana waliomuua mwanangu Stephen. Wao hawadhani kama wametenda uovu wa aina yoyote.
Hukumu inatazamiwa sku ya jumatano..

WikiLeaks suspect to get prison upgrade


USA - 
Article published the Wednesday 20 April 2011 - Latest update : Friday 16 December 2011

WikiLeaks suspect to get prison upgrade

Bradley Manning has been in prison since July 2010.
Bradley Manning has been in prison since July 2010.
AFP/Reuters/RFI

By RFI
The US army officer who allegedly passed classified documents to whistle-blowing website WikiLeaks is being transferred to a new prison, the Pentagon announced on Tuesday. Rights groups have criticised the treatment he received in his current jail in Quantico, Virginia.

Army intelligence officer Bradley Manning, who is still awaiting trial for his role in the WikiLeaks affair, will be sent to the Fort Leavenworth prison in Kansas. There he will be allowed contact with other detainees and visitors.
Dossier: AfPak news and analysis
He has been held at Quantico since July 2010. Campaign group Amnesty International criticised the “harsh and punitive” conditions he was kept in, including solitary confinement and being forced to sleep naked.
Quantico is designed for short-term incarceration. “It is rare if not unprecedented that
Like secrets? Find out about the Hidden Paris
somebody is there for as long as nine or 10 months,” admitted Jeh Johnson, the general counsel of the Department of Defense.
Johnson nonetheless insists that Manning’s treatment at Quantico complied with all “legal and regulatory standards”.