Tuesday, January 3, 2012

Bunge halijamalizana na Luhanjo, Jairo

Habari Kuu

article thumbnailWabunge D'salaam Wamvaa Magufuli
WAMTAKA AOMBE RADHI KWA KUTOA LUGHA CHAFUKeneth Goliama na Zaina Malongo
KAULI ya Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli kwamba watakaoshindwa kulipa nauli mpya ya Sh200 kuvuka Kigamboni ni vyema wakapiga mbizi kuvuka bahari, imewakera wabunge wa Mkoa wa  [ ... ]
(Comments 96)
Habari
Bunge halijamalizana na Luhanjo, Jairo
Fredy AzzahLICHA ya aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, David Jairo kung’atuka kwenye nafasi (Comments 10)
+ Full Story
IGP apangua askari kikosi cha silaha
Moto wazidi kuwaka NCCR Mageuzi
Balozi Mhina wa CCM afariki dunia
Madiwani Chadema Arusha warejea mahakamani
Tucta: JK wawajibishe mawaziri wazembe
Maswi: Nitasimamia kutekeleza ahadi tulizotoa Bungeni
Biashara
Ripoti ya uchunguzi kuhusu UDA kutolewa...
Patricia KimelemetaRIPOTI kuhusu sakata la kubinafishwa isivyo halali kwa Shirika la Usafiri la Dar es Salaam (UDA) inatarajiwa kutolewa kabla ya mwisho wa (Comments 1)
+ Full Story
Kampuni yatoa mkopo wa pembejeo za kilimo
Muheza watakiwa kutunza mazingira
Wasomi Dodoma, Singida watakiwa kusaidia ajira
Wakulima wapatiwa matrekta ya 160milioni
Ulanga wapewa Sh43 milioni
Vijana wambana Zitto wakitaka ajira
Michezo
Azam yaua, Simba leo
Jackson Odoyo, ZanzibarTIMU ya Azam imeanza vyema michuano ya Kombe la Mapinduzi kwa kuisambaratisha Kikwajuni kwa mabao 3-1 katika mchezo uliofanyika katika (Comments 1)
+ Full Story
Mashabiki wakelwa Papic kulea magoigoi Yanga
Nyoso:Msibweteke
Wachezaji waishusha daraja Toto
Man City kujiuliza kwa Liverpool leo
Matumla amfunga mdomo Cheka
Chipukizi tenisi hao Burundi
Makala
Profesa Nawe: Utamaduni wa kujisomea ...
SEKTA ndogo ya maktaba nchini inapiga hatua licha ya kuwapo kwa mwamko mdogo wa Watanzania kupenda kusoma vitabu na machapisho mbalimbali.Mkurugenzi Mkuu (Comments 0)
+ Full Story
Usajili shule nyingi za sekondari za kata haukufuata masharti na taratibu
Walimu Kapunga watembea kilometa 52 kwenda, kurudi shule
Dk Muganda: Changamoto za elimu; nchini zinahitaji tafiti za kina
Mwaka mpya na umachinga katika elimu ya watoto wetu
Unayajua madhara ya kuwa mtoro shuleni?
2011 umetuachia aibu kubwa katika michezo kim

Al- Mahmoundi kurudishwa Libya

Wabunge D'salaam Wamvaa Magufuli

Wabunge D'salaam Wamvaa Magufuli  Send to a friend
Monday, 02 January 2012 22:23
0digg
Abiria wakishuka kutoka katika kivuko cha Mv Magogoni kinachofanya kazi kati eneo la Magogoni na Kigamboni. Serikali imepandisha nauli ya kivuko hicho kuanzia juzi kutoka sh100 hadi 200, nauli iyodumu kwa zaidi ya miaka 14 iliyopita ambayo abiria wanaotumia kivuko hicho wanalalamikia ongezo hilo. Picha na Venance Nestory
WAMTAKA AOMBE RADHI KWA KUTOA LUGHA CHAFUKeneth Goliama na Zaina Malongo
KAULI ya Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli kwamba watakaoshindwa kulipa nauli mpya ya Sh200 kuvuka Kigamboni ni vyema wakapiga mbizi kuvuka bahari, imewakera wabunge wa Mkoa wa Dar es Salaam ambao sasa wanamtaka aombe radhi.

Juzi, Dk Magufuli akiwa katika ziara eneo la Kivukoni alijaribu kuzungumza na wananchi wa Kigamboni kuhusu ongezeko hilo la nauli lakini badala ya wananchi hao kumsikiliza, walizomea ndipo alipowaambia kuwa watakaoshindwa ni vyema wakapiga mbizi baharini, kuzunguka Kongowe kuingia katikati ya jiji au warudi kijijini wakalime.jana, wabunge hao licha ya kumtaka Dk Magufuli aombe radhi, wameitaka Serikali kusitisha mara moja amri ya ongezeko hilo la nauli katika kivuko hicho kutokana na uamuzi huo kufikiwa bila ya kuwashirikisha wananchi.

Akitoa tamko kwa niaba ya wenzake, Mwenyekiti wa Wabunge wa Mkoa wa Dar es Salaam, Abbas Mtemvu alisema tatizo lililopo katika kivuko hicho ni ubadhirifu mkubwa ambao umekuwa ukijitokeza na si nauli ndogo.Alisema ubadhirifu huo umesababisha makusanyo ya ushuru kuwa Sh9 milioni badala ya Sh18 milioni kwa mwezi na kuhoji fedha nyingine zinakokwenda.
Alisema  kitendo kilichofanywa na Waziri Magufuli ni cha kuidhalilisha Serikali kutokana na kutokuwa na ushirikiano na viongozi wengine na kufanya kazi kwa hasira.“Kwa hakika, Magufuli ametutukana kutokana na tabia yake ya kufanya kazi kwa hasira.

Tunamtahadharisha sisi ni wazaliwa wa Dar es salaam na ndiyo tunaujua huu mji. Hatutaki kuongea tu kama yeye, kinachotakiwa ni kusitisha ubabe wake maana  hapa siyo Chato (Jimbo ambalo Dk Magufuli ni mbunge wake),” alisema Mtevu.Mtevu alisema lazima Magufuli ajue nauli hizo hazikufuata sheria ya upandishaji kwa maana hata Sumatra (Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nchi Kavu na Majini), haijui kinachoendelea huku akisema kauli yake kwamba kupandisha nauli kunatokana na vituo vingine kupandisha ni ya kukurupuka inayotaka kuichonganisha Serikali na wananchi.

Alisema  jiji la Dar es Salaam linachukua watu wengi kutoka Kigamboni  hivyo, kupandisha nauli ni kuwaonea wananchi wanaoishi huko na ikifanya hivyo, Serikali itakuwa haijadhamiria kuwasaidia wananchi, bali kuwakomoa.Mtevu alisema kinachofanywa na Waziri Magufuli ni hasira na si uongozi bora akidai kwamba kila kitu anachoibua kinaleta mgongano katika Serikali huku akimsihi kuacha kukurupuka katika kutekeleza Ilani ya CCM.“Kitendo cha kuongeza nauli ni kuwaongezea neema watu wachache. Zoezi hilo lisitishwe mara moja na kuleta amani.
Alisema kama Serikali imeshindwa kusimamia mapato ya vivuko viwili vya Mv Kigamboni na Mv Alina, vikabidhiwe kwa wabunge kwa wiki mbili ili kukusanya mapato.
Alisema Serikali inapaswa kujua kwamba, CCM ndicho kilichopandisha nauli kutokana na jimbo hilo kusimamiwa na chama hicho na kuongeza kwamba hatua hiyo itawaathiri zaidi ya watu milioni 2.5.
Baadhi ya wabunge waliohudhuria mkutano huo mbali na Mtemvu ni pamoja na John Mnyika (Ubungo), Mussa Azzan Zungu (Ilala), Dk Faustine Ndugulile (Kigamboni, Zarina Madabida, Angela Kairuki na Philipa Mtulano (Viti Maalumu).
Akizungumzia madai ya wabunge hao, Msemaji Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Martin Ntemo alisema msimamo wa Serikali kuhusu suala hilo ni ule uliotolewa na Serikali kupitia kwa Dk Magufuli wa kupandisha nauli tofauti na madai kwamba Waziri Mkuu, Mizengo Pinda aliwahi kutoa agizo la kusitishwa kwa ongezeko hilo... “Hadi sasa kauli inayosimama ni ya Waziri (Magufuli).”
Kilio cha Dk NdugulileDk Ndugulile alisema hali ya hewa imechafuka katika jimbo lake kutokana na kuwatangazia wananchi kuwa Waziri Mkuu  amesitisha ongezeko hilo baada ya kupigiwa simu na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadik.Hata hivyo, Sadik alikaririwa na vyombo vya habari jana akikanusha kupokea maagizo hayo na kwamba alichoagiza ni kumtaka katibu mkuu katika ofisi yake kuwasiliana na mwenzake wa Ujenzi juu ya suala hilo kwa manufaa ya wananchi wa Kigamboni.
Dk Ndungulile alisema ongezeko hilo linagusa watu wanyonge   kwa zaidi ya asilimia 800 akiwataja kuwa ni  waendesha baiskeli za miguu mitatu (Maguta), baiskeli za kawaida, pikipiki na Bajaji  wakati wenye magari ya kifahari  hawajapandishiwa kiasi kikubwa cha nauli.Alisema haiingii akilini kuona guta likipaswa kulipiwa Sh1,800 kutoka Sh200 wakati gari dogo litalipa Sh1,300 kutoka Sh800... “Bei hizo ni za kumkomoa nani?”
Alisema tangu achaguliwe kuwa ubunge, amekuwa akimwandikia barua Waziri wa Ujenzi kuhusu kero mbalimbali za kivuko hicho lakini hakuna alichojibu zaidi ya kujitokeza jana (juzi) na kutangaza nauli mpya.“Wakati naingia katika nafasi ya uongozi wa ubunge Jimbo la Kigamboni nilitaka kupata taarifa ya mapato ya uendeshaji wa  kivuko ambapo nilipata taarifa ya makusanyo ya Sh8 milioni hadi 13milioni.

Baada ya kupokea taarifa hizo nilifanya uchunguzi wangu ambao baadaye nilibaini kuwa Serikali inapata kiasi cha Sh5 milioni kama mapato ya kivuko hicho huku kiasi cha Sh3 milioni kikiwa hakijulikani kinakwenda wapi,” alisema. Dk Ndugulile alisema kama Serikali ingeweza kudhibiti hali hiyo, leo hii kusingekuwa na ongezeko hilo la nauli kutoka Sh100 hadi 200 kwa waenda kwa miguu huku magari yenye ujazo tofauti wakitakiwa kulipa kiasi cha Sh1,300 hadi 1,500.Zungu: Kilio cha wajasiriamali
Kwa upande wake, Zungu alisema gharama hizo zimewaathiri kwa kiasi kikubwa wajasiriamali kuliko wenye fedha. Alisema nauli zilizowekwa hazikufuata sheria kutokana na kutoshirikisha wananchi wala kiongozi yoyote na kuhoji ulizi gani shirikishi unaohubiriwa.“Naomba tujiulize kikao cha kuongeza nauli kilifanyika wapi,  maana huu ni mzigo ambao wananchi hawatakiwi kubebeshwa,” alisema.Madabida kwa upande wake alisema ongezeko hilo litawaathiri zaidi kina mama wanaofanya biashara ndogondogo kwa kutumia kivuko hicho.Alisema Magufuli anataka kuwachonganisha wananchi na wabunge kutokana kauli zake

Mafuta yapanda bei sana Nigeria 2 Januari, 2012 - Saa 14:07 GMT

Mafuta yapanda bei sana Nigeria

 2 Januari, 2012 - Saa 14:07 GMT
Bei ya mafuta nchini Nigeria imepanda zaidi ya mara dufu baada ya serikali kuamua kuacha kufidia bei ya mafuta.
Wachuuzi wa petroli nchini Nigeria
Vyama vya wafanyakazi vimetoa wito kwa watu kujitayarisha kwa migomo na maandamano.
Serikali inadai kuwa kuondosha fidia hiyo inayoigharimu dola bilioni 6 kila mwaka, inamaanisha kuwa itakuwa na fedha kutumia kwenye miradi ya kupunguza umaskini.
Lakini Wanigeria wengi hawaamini kuwa wataona manufaa yoyote katika hatua za kupunguza ufukara.
Mwanaharakati wa wafanyakazi, John Odah, aliiambia BBC kwamba Nigeria haifai kuagizia petroli kutoka nchi za nje, na serikali inafaa kushughulikia kujenga mitambo ya kusafisha mafuta nchini.
"Nafikiri serikali haikuweza kujibu hoja kwamba nchi inayotoa mafuta kama sisi, haifai kuagiza petroli kutoka nje.
Kwa hivo serikali inafaa kuupa umbele mradi wa kuwa na vinu vya kutosha vya kusafisha mafuta nchini mwetu.
Lakini hatuoni kuwa serikali inaelekea huko."

Iran yajaribu makombora zaidi BAHARI YA HORMUZ


Iran yajaribu makombora zaidi

 2 Januari, 2012 - Saa 17:12 GMT
Iran inasema imefanikiwa katika majaribio ya makombora mawili zaidi, na inaonekana inataka kuonesha nguvu zake za kijeshi, siku ya mwisho ya mazoezi ya jeshi lake la wanamaji karibu na mlango wa bahari wa Hormuz.
Manuwari ya Iran ikifyatua kombora karibu na Hormuz
Kamanda wa jeshi la wanamaji la Iran, Mahmoud Mousavi, alisema kombora la kushambulia meli, lilotengenezwa Iran, liliipiga lengo; na kombora aina nyengine lilojaribiwa lilikuwa bora zaidi kushinda la awali.
Mwandishi wa BBC anasema Iran inataka kuonesha kuwa inaweza kudhibiti njia ya bahari ya Hormuz, ambapo ndipo meli nyingi zinazosafirisha mafuta zinapopita.
Anasema inatoa ujumbe kwa Mataifa ay Magharibi kwamba inaweza kutengeneza makombora yake yenyewe, juu ya kuwa imewekewa vikwazo kwa sababu ya mradi wake wa nuklia.

Youssou N'dour atangaza kuwania urais


Youssou N'dour atangaza kuwania urais

 3 Januari, 2012 - Saa 02:07 GMT
Mwanamuziki wa Senegal Youssou N'dour
Mwanamuziki wa Senegal Youssou N'dour
Mwanamuziki mashuhuri nchini Senegal na mwanaharakati wa kisiasa,Youssou N'dour, ametangaza kuwa atawania kiti cha urais katika uchaguzi wa mwezi Februari nchini humo.
Mwanamuziki huyo amesema kuwa anaitikia wito wa kumtaka agombee kiti hicho dhidi ya rais wa sasa Abdoulaye Wade, ambaye anapania kuwania kiti hicho kwa muhula wa tatu.
Youssou N'dour amehusika na maswala ya kibinadamu kwa siku nyingi na pia ni balozi wa shirika la umoja wa matataifa kuhusu maswala ya watoto (UNICEF).
Mwandishi wa BBC mjini Dakar, Thomas Fessy, anasema hatua ya bwana Youssou N'dour kutangaza kuwa atawania kiti cha urais, haijawashangaza wengi. Hii ni kufuatia tangazo alilotoa mwisho wa mwaka uliopita kuwa atajitosa katika ulingo wa kisiasa.
Katika hotuba iliyopeperushwa kupitia kituo chake cha redio na televisheni, mwanamuziki huyo amesema atapunguza matuzi ya serikali na kuahidi kuzalisha chakula na umeme kwa wote iwapo atachaguliwa kuwa rais wa Senegal.

''kuwa rais ni kazi sio taaluma''

Youssou N'dour anakubali kuwa yeye sio msomi lakini anaelezea wadhifa wa rais kama ''kazi na sio taaluma''.
Youssou N'dour alikuwa rafiki wa karibu wa rais Abdoulaye Wade, lakini baada ya Wade kutangaza nia ya kuwania kiti cha urais kwa muhula wa tatu, aligeuka na kuwa mpinzani wake mkuu.
Lakini haitakuwa kazi rahisi kwa Bw. Youssou Ndour kuwabadili maelfu ya wafuasi wake wa muziki kumpigia kura.
Aidha, Youssou N'dour amewahi kuwashutumu viongozi wa nchi za Afrika kuhusu jinsi walivyoshughulikia janga la njaa nchini Somalia.