Wednesday, June 24, 2015

Kondomu inayotambua maambukizi ya Zinaa

Kondomu inayotambua maambukizi ya Zinaa

 
Kondomu inayotambua maambukizi ya zinaa
Wanafunzi katika shule moja nchini Uingereza wameunda mipira ya kondomu inayowaonya watumiaji wanapojamiana na mtu aliyeambukizwa maradhi ya zinaa.
Kondomu hiyo inabadili rangi pindi inapokutana na majimaji ya mtu anayeugua maradhi ya zinaa.
Kondomu hiyo S.T.EYE inaweza kutambua maambukizi ya Chlamydia Kaswende na Kisonono.
Kulingana na wanafunzi hao kondomu hiyo inabadili rangi tofauti kulingana na bakteria iliyopo.
Uvumbuzi huu ni wa Daanyaal Ali, 14, Muaz Nawaz, 13 na Chirag Shah, 14, ambao ni wanafunzi katika shule ya Isaac Newton Academy iliyoko Ilford, Essex, nchini Uingereza.
 null
Kondomu hiyo S.T.EYE inaweza kutambua maambukizi ya Chlamydia Kaswende na Kisonono.
''tuliazimia kumpa onyo mtumiaji wa mipira hii kuwa mpenzi wake yuko salama ama ni mgonjwa bila ya wasiwasi wa kupimwa hospitalini''.
Wanafunzi hao tayari wametunukiwa, tuzo la ubunifu la ''the TeenTech'' .
Daanyall alisema kuwa "Walizindua kondomu hiyo ilikuifaidi kizazi kijacho''
''Kwa hakika swala la usalama wa mpenzi wako ni swala la kibinafsi kwa hivyo ni swala linalopaswa kupewa kipaombele haswa ikifahamika kuwa tunawajibu wa kuchochea ngono salama bila ya kuwashurutisha wapenzi wetu kufika hospitalini bila wao wenyewe kukusudia''
 null
Wavumbuzi hao wanasema kuwa hiyo ni mojawepo ya njia salama ya kubaini usalama penzi lenyu
Wanafunzi hao waliwalitunukiwa pauni elfu moja pamoja na fursa ya kuzuru Kasri la Malkia wa Uingereza Buckingham Palace.
Muasisi wa kampuni ya ubunifu wa kiteknolojia, TeenTech, Bwana Maggie Philbin, alisema kuwa
"Ni wajibu wetu kama jamii kuchochea ubunifu unaopatikana madarasani kuchochewa na kupigwa msasa kwa minajili ya kuboresha maisha ya mwanadamu''

Facebook kukutambua bila picha ya uso Dakika 49 zilizopita Mshirikishe mwenzako Facebook Tayari mtandao huo wa kijamii wa Facebook unakusanya taarifa kutoka katika picha zako ili kubaini migao ya maoni kutoka kwa marafiki wako pale wanapoweka mtandaoni picha. Sasa inaonekana mitandao ya kijamii inachukua mkondo mwingine wa kuboreshwa zaidi. Watafiti kutoka katika idara ya upelelezi ya Facebook wamekuwa wakiifanyia kazi teknolojia hiyo mpya ambayo nia kuu ni kumtambua mtu hata kama uso wake hauonekani bayana kwenye picha. Teknolojia hiyo iitwayo 'algorithm', inaangazia zaidi ya viungo mia moja vya mwanadamu. Inatumika kwa pamoja katika kutambua uso wa mtu na pia mwili mzima wa binadamu. Watafiti hao walitumia njia hiyo kwa kuzifanyia majaribio picha elfu 37 za watu ambazo zilitolewa kutoka kwa 'Flickr Commons'. Wanasema kuwa njia hiyo ilitoa matokeo asilimia 83 ya watu 581 tofauti. Matokeo hayo yaliwasilishwa mapema mwezi huu wa Juni katika kongamano la wakfu wa Computer Vision.

Facebook kukutambua bila picha ya uso


 
Facebook
Tayari mtandao huo wa kijamii wa Facebook unakusanya taarifa kutoka katika picha zako ili kubaini migao ya maoni kutoka kwa marafiki wako pale wanapoweka mtandaoni picha.
Sasa inaonekana mitandao ya kijamii inachukua mkondo mwingine wa kuboreshwa zaidi.
Watafiti kutoka katika idara ya upelelezi ya Facebook wamekuwa wakiifanyia kazi teknolojia hiyo mpya ambayo nia kuu ni kumtambua mtu hata kama uso wake hauonekani bayana kwenye picha.
Teknolojia hiyo iitwayo 'algorithm', inaangazia zaidi ya viungo mia moja vya mwanadamu.
Inatumika kwa pamoja katika kutambua uso wa mtu na pia mwili mzima wa binadamu.
Watafiti hao walitumia njia hiyo kwa kuzifanyia majaribio picha elfu 37 za watu ambazo zilitolewa kutoka kwa 'Flickr Commons'.
Wanasema kuwa njia hiyo ilitoa matokeo asilimia 83 ya watu 581 tofauti.
Matokeo hayo yaliwasilishwa mapema mwezi huu wa Juni katika kongamano la wakfu wa Computer Vision.

US iliwachunguza marais wa Ufaransa

US iliwachunguza marais wa Ufaransa


 
Marais wa Ufaransa
Kitengo cha ujasusi nchini Marekani NSA kiliwachunguza marais wa Ufaransa akiwemo Jacques Chirac,Nicolas Sarkozy na Francois Hollande mwaka 2006-12,kulingana na mtandao wa wikileaks.
Mtandao huo ulipata habari hizo kutoka kwa ripoti za kiintelijensia na stakhabadhi nyengine za kiufundi za NSA.
Afisa mmoja wa Ufaransa amesema kuwa upelelezi wa washirika haufai.
Rais wa Ufaransa Francois Hollande anatarajiwa kujadili swala hilo na maafisa wa usalama.
Marekani haijathibitisha ukweli wa stakhabadhi hizo
.null
Wikileaks
Mwaka 2013 shirika la ujasusi la Marekani NSA lilishtumiwa kwa kumpeleleza kansela wa Ujerumani Angela Merkel.
Siku ya jumanne,Wikileaks ilisema kuwa ilianza kuchapisha faili zilizo na kichwa ''Espionage Elysee'' ikiwa ni kumbukumbu za ikulu ya rais wa Ufaransa.
Imesema kuwa faili hizo za siri zilipatikana kupitia upelelezi wa moja kwa moja wa mawasiliano uliofanywa na shirika hilo kwa marais hao watatu wa Ufaransa pamoja na balozi wa Ufaransa nchini Marekani.
Moja ya faili hizo ilioandikwa mwaka 2012,ni kuhusu rais Hollande alivyokuwa akizungumza kuhusu kuondoka kwa Ugiriki katika muungano wa Ulaya.
Nyengine ya mwaka 2011 inadai kuwa bwana Sarkozy aliamua mazungumzo ya amani kati ya Israel na Palestina bila kuhusisha Marekani.
 null
Mwanzilishi wa Wikileaks Julian Assange
Faili nyengine ilioandikwa mwaka 2010 inadai kwamba maafisa wa Ufaransa walijua kwamba Marekani ilikuwa ikiwapeleleza na kwamba walipanga kutoa malalamishi yao.
Kulingana na habari za mawasiliano yaliodukuliwa,balozi wa Ufaransa nchini Marekani na mshauri wa rais Sarkozy walijadiliana kuhusu mpango wa Sarkozy kutoa ghadhabu zake kuhusu kukataa kwa Marekani kutia saini makubaliano ya ushirikiano wa kijasusi,ikiwa lengo ni kwa Marekani kuendelea kuipeleleza Ufaransa.

Monday, May 4, 2015

Floyd Mayweather amshinda Pacquiao

Floyd Mayweather amshinda Pacquiao

  • 3 Mei 2015
Pacquiao na Mayweather
Bondia wa Marekani Floyd Mayweather ameshinda pigano lililosubiri kwa wingi katika miongo kadhaa.
Mayweather amshinda Pacquiao
Bondia huyo ambaye hajashindwa alimshinda mpinzani wake raia wa Ufilipino Manny Pacquiao kwa wingi wa pointi.
Pacquiao akimpiga makonde mayweather
Mashabiki wengi waliojaa katika ukumbi wa MGM Grand Garden Arena mjini Las Vegas walimzoma mara kwa mara Mayweather.
Mayweather ashinda kwa wingi wa pointi
Kote duniani wateja millioni 3 walilipa kuliona pigano hilo ambalo ndio pigano lililovutia kitita kikubwa cha fedha katika historia ya ndondi.
Mayweather
Tiketi nyingi za pigano hilo ziliuzwa katika bei ya makumi ya maelfu ya dola.

Mkuu wa majeshi Burundi akemea wanasiasa

Mkuu wa majeshi Burundi akemea wanasiasa

  • 3 Mei 2015
Mkuu wa majeshi ya Burundi Meja Jenerali Prime Niyongabo
Mkuu wa majeshi nchini Burundi Meja Jenerali Prime Niyongabo ametoa wito kwa wanasiasa kutotumia jeshi la taifa kwa manufaa yao ya kisiasa.
Jenerali Niyongabo amekariri tangazo lililotolewa na waziri wa ulinzi Jumamosi kuwa jeshi la nchi hiyo litahakikisha kuwa mkataba wa Arusha umetekelezwa kikamilifu na kuwa jeshi hilo halitumiwi na mtu au chama chochote cha kisiasa.
Kuhusiana na maandamano yanayoendelea, mkuu huyo wa jeshi amesema kuwa maandamano hayo sio halali na wanaichi wanapaswa kutumia mbinu za sheria zilizopo kutatua mizozo yao.
Polisi wa kuzuia ghasia wakikabiliana na waandamanaji katika mitaa ya Bujumbura nchini Burundi
Wakati huo huo Meja Jenerali Niyongabo amesema jeshi hilo litasalia kuwa lenye nidhamu ya hali ya juu na tiifu kwa taifa la Burundi na wala sio kwa mwanasiasa yeyote.
Ameongeza kusema kufikia sasa jeshi limefanya kazi nzuri kuhakikisha kuwepo kwa usalama nchini Burundi na katika mataifa mengine wanakohudumu katika vikosi vya Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika.
Mkuu huyo wa majeshi amesema wanajeshi wataendelea kushirikiana na polisi kushika doria ili kuhakikisha amani na utulivu vinakuwepo nchini Burundi.
Huku hayo yakijitokeza muungano wa upinzani umesema kuwa maandamano yataendelea siku ya Jumatatu baada ya mapunziko ya siku mbili.
Upinzani umepinga hatua ya rais Pierre Nkurunziza ya kuwania muhula wa tatu kama rais.

Tuesday, January 20, 2015

Eti mafuta ya mwilini hukuza ubongo?



Eti mafuta ya mwilini hukuza ubongo?





Fumbo la siku zote kwamba wanawake ni wanene kuliko wanaume limepata ufumbuzi...ni wanene kwa wanahitaji mwili wenye umbo zuri na makalio makubwa ili kupata watoto waliojaaliwa werevu.
Taarifa hii ni kwa mujibu wa wanaakademia ambao wanasema kuwa wanawake wenye makalio na mapaja makubwa na umbo zuri kutokana na mafuta mfano kama Kim Kardashian hupata watoto werevu.
Nini hasa kinawafanya watoto wao kuwa werevu basi? Mafuta yanayopatikana katika sehemu za mwili wa mwanamke huwa na manufaa makubwa sana kwa watoto hasa wanapokuwa wananyonya, mafuta haya hupitia kwenye maziwa ya mama hadi kwa mwili wa mtoto.
Profesa Will Lassek wa chuo kikuu cha Pittsburgh University, Pennsylvania, aliyeongoza utafiti huo, anasema mafuta yanayopatikana katika sehemu hizo za mwili, husaidia sana katika kukuza ubongo wa matoto mchanga.



'Unahitaji mafuta mengi ya mwilini ili kuwa na mfumo mzuri wa neva na mafuta katika sehemu hizi za mwili yaani mapaja na makalio, huwa yina madini yajulikanayo kama DHA (docosahexaenoic acid), ambayo ni muhimu sana katika kutengeza ubongo wa binadamu.
Inaonekana kama wanawake wameweza kujua mbinu za kuhifadhi mafuta katika sehemu hizo za mwili hadi wanapopata mtoto.
Kwa mda mrefu haijajulikana kwa nini wanawake wanakuwa wanene sana.......mafuta ya mwili wao yakiwa ni asilimia 30 ya uzani wa mwili.
Professa Lassek anasema kwamba mafuta hayo ni kiwango sawa na yale yanayopatikana katika wanyama kama Dubu au Nyangumi wanapojiandaa kuzaa.
Wanasayansi wanasema mafuta yanayopatikana katika mapaja na makalio ya wanawake ndio yanayotumika kutengeza ubongo wa watoto wachanga.
Mafuta mengi katika mwili wa mwanamke huisha mwilini pindi mama anapomnyonyesha mtoto wake, kulingana na Profesa Lassek, aliyechapisha utafiti wake katika kitabu chake kipya chenye kichwa ''Kwa nini wanawake wanahitaji mafuta mwilini. ''
Wanawake wanaonyonyesha hupoteza kilo nusu ya mafuta mwilini kila mwezi.

Hali mbaya ya hewa yaikabili Zambia

Hali mbaya ya hewa yaikabili Zambia



Matokeo ya uchaguzi mkuu wa Zambia uliofanyika jana yatatangazwa kama ilivyopangwa awali.
Hata hivyo kutangazwa kwa matokeo hayo kunakabiliwa na changamoto mbalimbali kutokana na baadhi ya vituo vya kupigia kura kushindwa kupiga kura jana, na hivyo kufanyika leo.
Vituo hamsini na moja vitapiga kura hii leo na sababu kubwa ni mvua kubwa iliyo nyesha nchi yote ya Zambia ,hali mbaya ya hewa na kucheleweshwa kwa karatasi za kupigia kura ni sababu zilizotajwa kusababisha wananchi wa Zambia kutopiga kura na leo wapewe haki hiyo.
Hali mbaya ya hewa pia huenda ikasababisha hata matokeo ya uchaguzi kutolewa kama ilivyosemwa awali,naye Rafael Phiri,msemaji wa tume ya uchaguzi ya Zambia amethibitisha kuwa endapo yatachelewa sana haitazidi tarehe ishirini na nne mwezi huu.

Rais Obama ataka mgao sawa wa rasilimali

Rais Obama ataka mgao sawa wa rasilimali 

 
Rais Barack Obama wa Marekani
Rais wa Marekani Barak Obama, amesema Marekani inafanya mabadiliko ya kiuchumi na kijamii baada ya miaka mingi ya kujirudia kwa mdororo wa uchumi na vita, huku uchumi ukiongeza ajira kwa kasi kubwa kuliko wakati wowote tangu mwaka 1999.
Pia amesema Wamarekani wengi zaidi wana bima za afya kuliko wakati wowote kabla ya hapo.
Akihutubia taifa kupitia baraza la Congress lenye wajumbe wengi kutoka chama cha Republican, Rais Obama ametumia hotuba hiyo kutangaza mpango wa kujenga uchumi wa kati kwa wananchi wote wa Marekani, ambapo wananchi wa kipato cha chini watapata huduma za afya na elimu kwa gharama nafuu.
Rais Obama ametangaza hatua za kusaidia familia za wafanyakazi kunufaika kutokana na kukua kwa uchumi.Mkakati wa Bwana Obama anaouelezea kama uchumi wa daraja la kati, unahusisha kupandisha kodi kwa matajiri.
Hotuba ya Rais Obama ilibeba mapendekezo kuhusu kodi, vyuo vya jamii, huduma za internet, usalama katika mtandao wa komputa na likizo ya ugonjwa.
Bwana Obama amesema hali ya kutoka katika mdororo wa uchumi imetoa fursa ya kuongezeka kwa kipato na fursa kwa kila mtu.
Amesema uchumi wa daraja la kati ni wazo kwamba nchi hiyo inafanya vizuri kabisa wakati kila mtu anapata haki katika mapato na kila mtu anatendewa haki kama ilivyoanishwa katika sheria za nchi hiyo.