Wednesday, June 24, 2015

US iliwachunguza marais wa Ufaransa

US iliwachunguza marais wa Ufaransa


 
Marais wa Ufaransa
Kitengo cha ujasusi nchini Marekani NSA kiliwachunguza marais wa Ufaransa akiwemo Jacques Chirac,Nicolas Sarkozy na Francois Hollande mwaka 2006-12,kulingana na mtandao wa wikileaks.
Mtandao huo ulipata habari hizo kutoka kwa ripoti za kiintelijensia na stakhabadhi nyengine za kiufundi za NSA.
Afisa mmoja wa Ufaransa amesema kuwa upelelezi wa washirika haufai.
Rais wa Ufaransa Francois Hollande anatarajiwa kujadili swala hilo na maafisa wa usalama.
Marekani haijathibitisha ukweli wa stakhabadhi hizo
.null
Wikileaks
Mwaka 2013 shirika la ujasusi la Marekani NSA lilishtumiwa kwa kumpeleleza kansela wa Ujerumani Angela Merkel.
Siku ya jumanne,Wikileaks ilisema kuwa ilianza kuchapisha faili zilizo na kichwa ''Espionage Elysee'' ikiwa ni kumbukumbu za ikulu ya rais wa Ufaransa.
Imesema kuwa faili hizo za siri zilipatikana kupitia upelelezi wa moja kwa moja wa mawasiliano uliofanywa na shirika hilo kwa marais hao watatu wa Ufaransa pamoja na balozi wa Ufaransa nchini Marekani.
Moja ya faili hizo ilioandikwa mwaka 2012,ni kuhusu rais Hollande alivyokuwa akizungumza kuhusu kuondoka kwa Ugiriki katika muungano wa Ulaya.
Nyengine ya mwaka 2011 inadai kuwa bwana Sarkozy aliamua mazungumzo ya amani kati ya Israel na Palestina bila kuhusisha Marekani.
 null
Mwanzilishi wa Wikileaks Julian Assange
Faili nyengine ilioandikwa mwaka 2010 inadai kwamba maafisa wa Ufaransa walijua kwamba Marekani ilikuwa ikiwapeleleza na kwamba walipanga kutoa malalamishi yao.
Kulingana na habari za mawasiliano yaliodukuliwa,balozi wa Ufaransa nchini Marekani na mshauri wa rais Sarkozy walijadiliana kuhusu mpango wa Sarkozy kutoa ghadhabu zake kuhusu kukataa kwa Marekani kutia saini makubaliano ya ushirikiano wa kijasusi,ikiwa lengo ni kwa Marekani kuendelea kuipeleleza Ufaransa.

No comments:

Post a Comment