Mazungumzo kuhusu Sudan Kusini yaanza
3 Januari, 2014 - Saa 10:27 GMT
Mazungumzo ya kupatanisha pande
mbili zinazozozana kwenye mgogoro wa Sudan Kusini na kusitisha vita,
yameanza mjini Addis Ababa Ethiopia.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka katika wizara ya
mambo ya nje nchini Ethiopia, wajumbe kutoka kanda ya Afrika Mashariki
wananuia kusuluhisha mgogoro huo wa kisiasa ambao umekuwa ukitokota kwa
takriban wiki tatu.Waakilishi kutoka pande zinazozozana wanakutana na wajumbe wa kikanda wanaoendesha mazungumzo hayo ingawa haijulikani ikiwa vingozi wa Sudan Kusini wenyewe watakutana ana kwa ana.
Mamia ya maelfu ya raia wa nchi hiyo wameachwa bila makao kufuatia mapigano hayo kati ya majeshi ya Rais Salva Kiir na yale ya hasimu wake ambaye alikuwa makamu wake wa Rais Riek Machar
Wakati huo huo, ubalozi wa Marekani, katika mji mkuu wa Sudan Kusini,Juba unaendelea na shughuli ya kuwahamisha wafanyakazi wake wote nchini humo kutokana na mzozo unaoendelea.
Umoja wa Mataifa umesema kuwa hautarajii raia wa Marekani wanaofanya kazi na shirika lake lolote kuondoka.
Waasi wakiongozwa na makamu wa rais wa zamani Riek Machar wamekuwa wakipambana na wanajeshi wa serikali tangu mwezi uliopita.
No comments:
Post a Comment