Wednesday, February 1, 2012

Nchi 25 zatia saini mkataba wa Euro

Nchi 25 zatia saini mkataba wa Euro

 31 Januari, 2012 - Saa 03:33 GMT
Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron
Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron
Nchi 25 kati ya 27 wanachama wa jumuiya ya ulaya zimetia saini mkataba ambao utachunguza zaidi matumaizi ya bajeti. Lakini jamhuri ya Czech na Uingereza hajizatia saini mkataba huo.
Mkataba huo mpya utasainiwa na nchi 25 mwezi Machi na baadaye lazima uidhinishwe.
Mkataba huo utaziwekea vikwazo nchi ambazo zitavunja sheria za matumizi ya fedha za jumuiya ya ulaya.
Nchi zilizotia saini mkataba huo pia zitahitajika kuongeza sheria kuhusu bajeti katika katiba zao.
Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron amesema kwamba angependa uchumi katika nchi za jumuiya ya ulaya kuimarika haraka iwezekanavyo lakini ameeleza wazi kwamba atachukua hatua ikiwa mkataba huo mpya wa kifedha utadhuru Uingereza.
Waziri mkuu huyo ameshtumiwa kwa kurudi nyuma katika utekelezaji wa ahadi ya kuzuia taasisi za jumuiya ya ulaya kutumika katika kufuatilia mkataba huo mpya.
Cameron amesema Uingereza itakuwa macho kuona kwamba mambo kama kuendesha shughuli za soko moja haziathiriwi.
Lakini amesema kwamba itakuwa vyema ikiwa nchi ambazo zinatumia sarafu ya Euro zitaweza kukumbana na madeni na ikiwa mkataba huu mpya utazisaidia kufanya hivyo.
Ujerumani inataka nchi zote zinazotumia sarafu ya Euro zitie saini mkataba huo, ambao utakua na sheria kali zaidi za bajeti, kabla iamue kama itatumia fedha zaidi kusaidia nchi hizo kupambana na mdororo wa uchumi.

No comments:

Post a Comment