Haki miliki ya pichaRoma MkatolikiImage caption
Msanii Roma mkatoliki adaiwa kupatikana katika kituo kimoja cha polisi Jijini Dar Es Salaam
Msanii Roma
Mkatoliki aliyedaiwa kutoweka na watu wasiojulikana nchini Tanzania sasa
amepatikana katika kituo cha polisi cha Oysterbay jijini Dar.
Habari
hizo zimethibtishwa na mmiliki wa studio za Tongwe ambapo msanii huyo
na wenzake wawili wanadaiwa kuchukuliwa na watu wasiojulikana siku ya
Jumatano jioni.
Hata
hivyo mmiliki huyo J Mada anasema kuwa hakuna maelezo ya kutosha
kuhusiana na wapi walipokuwa na ni akina nani aliokuwa wanawazuia.
Haki miliki ya pichaJamii ForumsImage caption
Mtandao wa jamii forums
Mtandao wa Jamii Forums unasema kuwa kupatikana kwao
kumefuatia wito mkubwa uliokuwa ukipaishwa na wasanii wenzake na
mashabiki kuhusu kuachiliwa huru, ndani na nje ya mitandao ya kijamii. Serikali yaomba usaidizi kumtafuta Roma Mkatoliki
Awali,
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Kamishina Simon Sirro
alisema bado walikuwa wakiendelea na upelelezi wa tukio la kupotea
(kutekwa) kwa msanii Roma Mkatoliki na wenzake.
Image caption
Price alipigwa risasi na mwanawe akiendesha gari
Mvulana wa umri wa miaka miwili amempiga risasi na kumuua mamake kimakosa katika mji wa Milwaukee, Marekani.
Mtoto huyo alipata bunduki hiyo sehemu ya nyuma ya gari.
Mwanamke
huyo, Patrice Price, 26, alikuwa akiendesha gari la mpenzi wake ambaye
ni mlinzi na ambaye alikuwa ameacha bunduki yake kwenye gari, babake
Andre Price amesema.
Polisi wa Milwaukee wanasema mwanamke huyo alipigwa risasi moja kutoka nyuma akiendesha gari mapema Jumanne asubuhi.
Mamake Price na mwanawe mwingine wa kiume mwenye umri wa mwaka mmoja walikuwa kwenye gari hilo wakati wa kutokea kwa kisa hicho.
Bw Price alisema ana binti mwingine mkubwa, lakini akasema Patrice alikuwa na bidii sana.
“Sasa hayupo nasi tena. Inaniuma sana,” Bw Price aliambia kituo cha habari cha WISN, Milwaukee.
Mwezi uliopita, mvulana wa umri wa miaka minne alimpiga risasi mamake Jamie Gilt katika jimbo la Florida katika hali sawa.
Bi Gilt alinusurika na majeraha.
Mtoto wa umri wa mwaka mmoja unusu amepatikana akiwa hai kwenye vifusi vya jengo lililoporomoka Ijumaa jijini Nairobi.
Jengo hilo la ghorofa sita liliporomoka katika mtaa wa Huruma baada ya mvua kubwa kunyesha.
Kwa mujibu wa gazeti la Daily Nation, msichana huyo alitolewa kwenye vifusi mwendo wa saa kumi usiku na kukimbizwa hospitalini.
Kamanda wa kitengo cha taifa cha kudhibiti majanga Pius Maasai anasema hali ya mtoto huyo ni thabiti, kwa mujibu wa gazeti hilo.
Watu 22 wamethibitishwa kufariki na wengine karibu 90 hawajulikani walipo.
Juhudi za uokoaji bado zinaendelea siku ya nne baada ya mkasa huo kutokea.
Kufikia sasa, watu 136 wameokolewa.
Polisi
wanasema wamiliki wa jumba hilo, ambalo maafisa wa baraza la jiji
wanasema halikufaa kuishi watu, wamekamatwa na wanazuiliwa na polisi.
Taarifa zinasema watafikishwa mahakamani baadaye Jumanne.
Wanafunzi
katika shule moja nchini Uingereza wameunda mipira ya kondomu
inayowaonya watumiaji wanapojamiana na mtu aliyeambukizwa maradhi ya
zinaa.
Kondomu hiyo inabadili rangi pindi inapokutana na majimaji ya mtu anayeugua maradhi ya zinaa.
Kondomu hiyo S.T.EYE inaweza kutambua maambukizi ya Chlamydia Kaswende na Kisonono.
Kulingana na wanafunzi hao kondomu hiyo inabadili rangi tofauti kulingana na bakteria iliyopo.
Uvumbuzi
huu ni wa Daanyaal Ali, 14, Muaz Nawaz, 13 na Chirag Shah, 14, ambao
ni wanafunzi katika shule ya Isaac Newton Academy iliyoko Ilford,
Essex, nchini Uingereza.
Kondomu hiyo S.T.EYE inaweza kutambua maambukizi ya Chlamydia Kaswende na Kisonono.
''tuliazimia kumpa onyo
mtumiaji wa mipira hii kuwa mpenzi wake yuko salama ama ni mgonjwa bila
ya wasiwasi wa kupimwa hospitalini''.
Wanafunzi hao tayari wametunukiwa, tuzo la ubunifu la ''the TeenTech'' .
Daanyall alisema kuwa "Walizindua kondomu hiyo ilikuifaidi kizazi kijacho''
''Kwa
hakika swala la usalama wa mpenzi wako ni swala la kibinafsi kwa hivyo
ni swala linalopaswa kupewa kipaombele haswa ikifahamika kuwa tunawajibu
wa kuchochea ngono salama bila ya kuwashurutisha wapenzi wetu kufika
hospitalini bila wao wenyewe kukusudia''
Wavumbuzi hao wanasema kuwa hiyo ni mojawepo ya njia salama ya kubaini usalama penzi lenyu
Wanafunzi hao waliwalitunukiwa pauni elfu moja pamoja na fursa ya kuzuru Kasri la Malkia wa Uingereza Buckingham Palace.
Muasisi wa kampuni ya ubunifu wa kiteknolojia, TeenTech, Bwana Maggie Philbin, alisema kuwa
"Ni
wajibu wetu kama jamii kuchochea ubunifu unaopatikana madarasani
kuchochewa na kupigwa msasa kwa minajili ya kuboresha maisha ya
mwanadamu''
Tayari
mtandao huo wa kijamii wa Facebook unakusanya taarifa kutoka katika
picha zako ili kubaini migao ya maoni kutoka kwa marafiki wako pale
wanapoweka mtandaoni picha.
Sasa inaonekana mitandao ya kijamii inachukua mkondo mwingine wa kuboreshwa zaidi.
Watafiti
kutoka katika idara ya upelelezi ya Facebook wamekuwa wakiifanyia kazi
teknolojia hiyo mpya ambayo nia kuu ni kumtambua mtu hata kama uso wake
hauonekani bayana kwenye picha.
Teknolojia hiyo iitwayo 'algorithm', inaangazia zaidi ya viungo mia moja vya mwanadamu.
Inatumika kwa pamoja katika kutambua uso wa mtu na pia mwili mzima wa binadamu.
Watafiti hao walitumia njia hiyo kwa kuzifanyia majaribio picha elfu 37 za watu ambazo zilitolewa kutoka kwa 'Flickr Commons'.
Wanasema kuwa njia hiyo ilitoa matokeo asilimia 83 ya watu 581 tofauti.
Matokeo hayo yaliwasilishwa mapema mwezi huu wa Juni katika kongamano la wakfu wa Computer Vision.
Kitengo
cha ujasusi nchini Marekani NSA kiliwachunguza marais wa Ufaransa
akiwemo Jacques Chirac,Nicolas Sarkozy na Francois Hollande mwaka
2006-12,kulingana na mtandao wa wikileaks.
Mtandao huo ulipata habari hizo kutoka kwa ripoti za kiintelijensia na stakhabadhi nyengine za kiufundi za NSA.
Afisa mmoja wa Ufaransa amesema kuwa upelelezi wa washirika haufai.
Rais wa Ufaransa Francois Hollande anatarajiwa kujadili swala hilo na maafisa wa usalama.
Marekani haijathibitisha ukweli wa stakhabadhi hizo
.
Wikileaks
Mwaka 2013 shirika la ujasusi la Marekani NSA lilishtumiwa kwa kumpeleleza kansela wa Ujerumani Angela Merkel.
Siku
ya jumanne,Wikileaks ilisema kuwa ilianza kuchapisha faili zilizo na
kichwa ''Espionage Elysee'' ikiwa ni kumbukumbu za ikulu ya rais wa
Ufaransa.
Imesema kuwa faili hizo za siri zilipatikana kupitia
upelelezi wa moja kwa moja wa mawasiliano uliofanywa na shirika hilo kwa
marais hao watatu wa Ufaransa pamoja na balozi wa Ufaransa nchini
Marekani.
Moja ya faili hizo ilioandikwa mwaka 2012,ni kuhusu rais
Hollande alivyokuwa akizungumza kuhusu kuondoka kwa Ugiriki katika
muungano wa Ulaya.
Nyengine ya mwaka 2011 inadai kuwa bwana
Sarkozy aliamua mazungumzo ya amani kati ya Israel na Palestina bila
kuhusisha Marekani.
Mwanzilishi wa Wikileaks Julian Assange
Faili nyengine ilioandikwa
mwaka 2010 inadai kwamba maafisa wa Ufaransa walijua kwamba Marekani
ilikuwa ikiwapeleleza na kwamba walipanga kutoa malalamishi yao.
Kulingana
na habari za mawasiliano yaliodukuliwa,balozi wa Ufaransa nchini
Marekani na mshauri wa rais Sarkozy walijadiliana kuhusu mpango wa
Sarkozy kutoa ghadhabu zake kuhusu kukataa kwa Marekani kutia saini
makubaliano ya ushirikiano wa kijasusi,ikiwa lengo ni kwa Marekani
kuendelea kuipeleleza Ufaransa.
Bondia wa Marekani Floyd Mayweather ameshinda pigano lililosubiri kwa wingi katika miongo kadhaa.
Mayweather amshinda Pacquiao
Bondia huyo ambaye hajashindwa alimshinda mpinzani wake raia wa Ufilipino Manny Pacquiao kwa wingi wa pointi.
Pacquiao akimpiga makonde mayweather
Mashabiki wengi waliojaa katika ukumbi wa MGM Grand Garden Arena mjini Las Vegas walimzoma mara kwa mara Mayweather.
Mayweather ashinda kwa wingi wa pointi
Kote duniani wateja millioni 3
walilipa kuliona pigano hilo ambalo ndio pigano lililovutia kitita
kikubwa cha fedha katika historia ya ndondi.
Mayweather
Tiketi nyingi za pigano hilo ziliuzwa katika bei ya makumi ya maelfu ya dola.