Tuesday, May 3, 2016

Mtoto mchanga atolewa kwenye vifusi Nairobi

Mtoto mchanga atolewa kwenye vifusi Nairobi

  • 3 Mei 2016. chanzo , bbcswahili
Jengo
Mtoto wa umri wa mwaka mmoja unusu amepatikana akiwa hai kwenye vifusi vya jengo lililoporomoka Ijumaa jijini Nairobi.
Jengo hilo la ghorofa sita liliporomoka katika mtaa wa Huruma baada ya mvua kubwa kunyesha.
Kwa mujibu wa gazeti la Daily Nation, msichana huyo alitolewa kwenye vifusi mwendo wa saa kumi usiku na kukimbizwa hospitalini.
Kamanda wa kitengo cha taifa cha kudhibiti majanga Pius Maasai anasema hali ya mtoto huyo ni thabiti, kwa mujibu wa gazeti hilo.
Watu 22 wamethibitishwa kufariki na wengine karibu 90 hawajulikani walipo.
Juhudi za uokoaji bado zinaendelea siku ya nne baada ya mkasa huo kutokea.
Kufikia sasa, watu 136 wameokolewa.
Polisi wanasema wamiliki wa jumba hilo, ambalo maafisa wa baraza la jiji wanasema halikufaa kuishi watu, wamekamatwa na wanazuiliwa na polisi.
Taarifa zinasema watafikishwa mahakamani baadaye Jumanne.

No comments:

Post a Comment