Bondia wa Marekani Floyd Mayweather ameshinda pigano lililosubiri kwa wingi katika miongo kadhaa.
Bondia huyo ambaye hajashindwa alimshinda mpinzani wake raia wa Ufilipino Manny Pacquiao kwa wingi wa pointi.
Mashabiki wengi waliojaa katika ukumbi wa MGM Grand Garden Arena mjini Las Vegas walimzoma mara kwa mara Mayweather.
Kote duniani wateja millioni 3
walilipa kuliona pigano hilo ambalo ndio pigano lililovutia kitita
kikubwa cha fedha katika historia ya ndondi.
Tiketi nyingi za pigano hilo ziliuzwa katika bei ya makumi ya maelfu ya dola.
Mkuu
wa majeshi nchini Burundi Meja Jenerali Prime Niyongabo ametoa wito kwa
wanasiasa kutotumia jeshi la taifa kwa manufaa yao ya kisiasa.
Jenerali
Niyongabo amekariri tangazo lililotolewa na waziri wa ulinzi Jumamosi
kuwa jeshi la nchi hiyo litahakikisha kuwa mkataba wa Arusha
umetekelezwa kikamilifu na kuwa jeshi hilo halitumiwi na mtu au chama
chochote cha kisiasa.
Kuhusiana na maandamano yanayoendelea, mkuu
huyo wa jeshi amesema kuwa maandamano hayo sio halali na wanaichi
wanapaswa kutumia mbinu za sheria zilizopo kutatua mizozo yao.
Wakati huo huo Meja Jenerali
Niyongabo amesema jeshi hilo litasalia kuwa lenye nidhamu ya hali ya juu
na tiifu kwa taifa la Burundi na wala sio kwa mwanasiasa yeyote.
Ameongeza
kusema kufikia sasa jeshi limefanya kazi nzuri kuhakikisha kuwepo kwa
usalama nchini Burundi na katika mataifa mengine wanakohudumu katika
vikosi vya Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika.
Mkuu huyo wa
majeshi amesema wanajeshi wataendelea kushirikiana na polisi kushika
doria ili kuhakikisha amani na utulivu vinakuwepo nchini Burundi.
Huku
hayo yakijitokeza muungano wa upinzani umesema kuwa maandamano
yataendelea siku ya Jumatatu baada ya mapunziko ya siku mbili.
Upinzani umepinga hatua ya rais Pierre Nkurunziza ya kuwania muhula wa tatu kama rais.