Fumbo la siku zote kwamba wanawake
ni wanene kuliko wanaume limepata ufumbuzi...ni wanene kwa wanahitaji
mwili wenye umbo zuri na makalio makubwa ili kupata watoto waliojaaliwa
werevu.
Taarifa hii ni kwa mujibu wa wanaakademia ambao wanasema
kuwa wanawake wenye makalio na mapaja makubwa na umbo zuri kutokana na
mafuta mfano kama
Kim Kardashian hupata watoto werevu.
Nini hasa kinawafanya
watoto wao kuwa werevu basi? Mafuta yanayopatikana katika sehemu za
mwili wa mwanamke huwa na manufaa makubwa sana kwa watoto hasa
wanapokuwa wananyonya, mafuta haya hupitia kwenye maziwa ya mama hadi
kwa mwili wa mtoto.
Profesa Will Lassek wa chuo kikuu cha
Pittsburgh University, Pennsylvania, aliyeongoza utafiti huo, anasema
mafuta yanayopatikana katika sehemu hizo za mwili, husaidia sana katika
kukuza ubongo wa matoto mchanga.
'Unahitaji mafuta mengi ya
mwilini ili kuwa na mfumo mzuri wa neva na mafuta katika sehemu hizi za
mwili yaani mapaja na makalio, huwa yina madini yajulikanayo kama DHA
(docosahexaenoic acid), ambayo ni muhimu sana katika kutengeza ubongo wa
binadamu.
Inaonekana kama wanawake wameweza kujua mbinu za kuhifadhi mafuta katika sehemu hizo za mwili hadi wanapopata mtoto.
Kwa
mda mrefu haijajulikana kwa nini wanawake wanakuwa wanene
sana.......mafuta ya mwili wao yakiwa ni asilimia 30 ya uzani wa mwili.
Professa
Lassek anasema kwamba mafuta hayo ni kiwango sawa na yale
yanayopatikana katika wanyama kama Dubu au Nyangumi wanapojiandaa kuzaa.
Wanasayansi
wanasema mafuta yanayopatikana katika mapaja na makalio ya wanawake
ndio yanayotumika kutengeza ubongo wa watoto wachanga.
Mafuta
mengi katika mwili wa mwanamke huisha mwilini pindi mama anapomnyonyesha
mtoto wake, kulingana na Profesa Lassek, aliyechapisha utafiti wake
katika kitabu chake kipya chenye kichwa ''Kwa nini wanawake wanahitaji
mafuta mwilini. ''
Wanawake wanaonyonyesha hupoteza kilo nusu ya mafuta mwilini kila mwezi.
Matokeo ya uchaguzi mkuu wa Zambia uliofanyika jana yatatangazwa kama ilivyopangwa awali.
Hata
hivyo kutangazwa kwa matokeo hayo kunakabiliwa na changamoto mbalimbali
kutokana na baadhi ya vituo vya kupigia kura kushindwa kupiga kura
jana, na hivyo kufanyika leo.
Vituo hamsini na moja vitapiga kura
hii leo na sababu kubwa ni mvua kubwa iliyo nyesha nchi yote ya Zambia
,hali mbaya ya hewa na kucheleweshwa kwa karatasi za kupigia kura ni
sababu zilizotajwa kusababisha wananchi wa Zambia kutopiga kura na leo
wapewe haki hiyo.
Hali mbaya ya hewa pia huenda ikasababisha hata
matokeo ya uchaguzi kutolewa kama ilivyosemwa awali,naye Rafael
Phiri,msemaji wa tume ya uchaguzi ya Zambia amethibitisha kuwa endapo
yatachelewa sana haitazidi tarehe ishirini na nne mwezi huu.
Rais
wa Marekani Barak Obama, amesema Marekani inafanya mabadiliko ya
kiuchumi na kijamii baada ya miaka mingi ya kujirudia kwa mdororo wa
uchumi na vita, huku uchumi ukiongeza ajira kwa kasi kubwa kuliko wakati
wowote tangu mwaka 1999.
Pia amesema Wamarekani wengi zaidi wana bima za afya kuliko wakati wowote kabla ya hapo.
Akihutubia
taifa kupitia baraza la Congress lenye wajumbe wengi kutoka chama cha
Republican, Rais Obama ametumia hotuba hiyo kutangaza mpango wa kujenga
uchumi wa kati kwa wananchi wote wa Marekani, ambapo wananchi wa kipato
cha chini watapata huduma za afya na elimu kwa gharama nafuu.
Rais
Obama ametangaza hatua za kusaidia familia za wafanyakazi kunufaika
kutokana na kukua kwa uchumi.Mkakati wa Bwana Obama anaouelezea kama
uchumi wa daraja la kati, unahusisha kupandisha kodi kwa matajiri.
Hotuba
ya Rais Obama ilibeba mapendekezo kuhusu kodi, vyuo vya jamii, huduma
za internet, usalama katika mtandao wa komputa na likizo ya ugonjwa.
Bwana Obama amesema hali ya kutoka katika mdororo wa uchumi imetoa fursa ya kuongezeka kwa kipato na fursa kwa kila mtu.
Amesema
uchumi wa daraja la kati ni wazo kwamba nchi hiyo inafanya vizuri
kabisa wakati kila mtu anapata haki katika mapato na kila mtu anatendewa
haki kama ilivyoanishwa katika sheria za nchi hiyo.
Waziri Mkuu mstaafu Joseph Warioba akisaidiwa kutolewa katika vurugu
Katika
mazingira ya kutatanisha, siku ya Jumapili vurugu zimekatisha mdahalo
uliokuwa ukiendelea kujadili mchakato wa katiba mpya ya Tanzania huku
baadhi ya watu wakipigwa na kujeruhiwa.
Mdahalo huo uliokuwa
ukitangazwa moja kwa moja kupitia redio na televisheni ulivurugika
kutokana na kundi la vijana wapatao 20 kuanza kumzomea aliyekuwa
mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba,
alipokuwa akiwasilisha mada yake.
Vijana hao ambao haijajulikana
walitokea wapi au walikuwa na ajenda gani waliinua mabango ya kupinga
msimamo wa waliokuwa wakiendesha mdahalo na kusema rasimu ya katiba
iliyopendekezwa inakidhi mahitaji yote na kusema hakuna haja ya mdahalo.
Jaji
Warioba ambaye ni Waziri Mkuu mstaafu wa Tanzania alifanikiwa kutoka
nje ya ukumbi ulipokuwa ukifanyika mdahalo huo mjini Dar Es Salaam,
lakini wapo watu waliojeruhiwa kutokana na kurushwa viti na vitu
vingine.
BBC iliwasiliana na Jaji Warioba apate kueleza
yaliyotokea na kama yuko salama baada ya vurugu hizo, lakini aliomba
radhi kwa kusema hayupo tayari kulizungumzia swala hilo.
Kiongozi
wa kitengo cha hamasa umoja wa vijana CCM (UVCCM), Paul Makonda,
aliyekuwepo ukumbini alidaiwa kuhusika na vurugu. Lakini alipoulizwa na
BBC kujibu tuhuma hizo Bw Makonda amekanusha kuhusika nazo huku akisema
kwamba alihudhuria mdahalo kwasababu ulikuwa wazi kwa kila mtu.
Wakati
wa vikao vya Bunge Maalum la Katiba mjini Dodoma, Makonda aliwahi kutoa
kauli za kumkebehi Jaji Warioba ambaye tume yake iliandaa rasimu ya
iliyokuwa ikijadiliwa na bunge hilo.
Hata hivyo Kamanda wa Polisi
mkoa wa Kinondoni, Camillius Wambura, aliieleza BBC kuwa hana maelezo ya
kutosha na kwamba atalizungumzia akipata taarifa rasmi ya kiofisi.
Tanzania
ipo katika mchakato wa kupata katiba mpya. Rasimu iliyodaliwa na
kupitishwa na bunge lililosusiwa na vyama vya upinzani inatarajiwa
kupigiwa kura na wananchi mwezi Aprili, 2015.
Wachambuzi wa
maswala ya kisiasa wameeleza wasi wasi kuwa endapo hakutakuwa na
kuvumiliana hali ya kisiasa nchini humo inaweza kubadilika na kuleta
ghasia ambazo zinaweza kuepukika.
Waziri Mkuu mstaafu Joseph Warioba akisaidiwa kutolewa katika vurugu
Katika
mazingira ya kutatanisha, siku ya Jumapili vurugu zimekatisha mdahalo
uliokuwa ukiendelea kujadili mchakato wa katiba mpya ya Tanzania huku
baadhi ya watu wakipigwa na kujeruhiwa.
Mdahalo huo uliokuwa
ukitangazwa moja kwa moja kupitia redio na televisheni ulivurugika
kutokana na kundi la vijana wapatao 20 kuanza kumzomea aliyekuwa
mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba,
alipokuwa akiwasilisha mada yake.
Vijana hao ambao haijajulikana
walitokea wapi au walikuwa na ajenda gani waliinua mabango ya kupinga
msimamo wa waliokuwa wakiendesha mdahalo na kusema rasimu ya katiba
iliyopendekezwa inakidhi mahitaji yote na kusema hakuna haja ya mdahalo.
Jaji
Warioba ambaye ni Waziri Mkuu mstaafu wa Tanzania alifanikiwa kutoka
nje ya ukumbi ulipokuwa ukifanyika mdahalo huo mjini Dar Es Salaam,
lakini wapo watu waliojeruhiwa kutokana na kurushwa viti na vitu
vingine.
BBC iliwasiliana na Jaji Warioba apate kueleza
yaliyotokea na kama yuko salama baada ya vurugu hizo, lakini aliomba
radhi kwa kusema hayupo tayari kulizungumzia swala hilo.
Kiongozi
wa kitengo cha hamasa umoja wa vijana CCM (UVCCM), Paul Makonda,
aliyekuwepo ukumbini alidaiwa kuhusika na vurugu. Lakini alipoulizwa na
BBC kujibu tuhuma hizo Bw Makonda amekanusha kuhusika nazo huku akisema
kwamba alihudhuria mdahalo kwasababu ulikuwa wazi kwa kila mtu.
Wakati
wa vikao vya Bunge Maalum la Katiba mjini Dodoma, Makonda aliwahi kutoa
kauli za kumkebehi Jaji Warioba ambaye tume yake iliandaa rasimu ya
iliyokuwa ikijadiliwa na bunge hilo.
Hata hivyo Kamanda wa Polisi
mkoa wa Kinondoni, Camillius Wambura, aliieleza BBC kuwa hana maelezo ya
kutosha na kwamba atalizungumzia akipata taarifa rasmi ya kiofisi.
Tanzania
ipo katika mchakato wa kupata katiba mpya. Rasimu iliyodaliwa na
kupitishwa na bunge lililosusiwa na vyama vya upinzani inatarajiwa
kupigiwa kura na wananchi mwezi Aprili, 2015.
Wachambuzi wa
maswala ya kisiasa wameeleza wasi wasi kuwa endapo hakutakuwa na
kuvumiliana hali ya kisiasa nchini humo inaweza kubadilika na kuleta
ghasia ambazo zinaweza kuepukika.
"Sitamwaacha binti yangu ateseke kama mimi ninavyoteseka nikiwa katika siku zangu. Familia yangu inafanya nijihisi najisi.
"Siruhusiwi kwenda jikoni, Siwezi kuingia hekaluni, Siwezi kukaa na wengine."
Kuna
hisia ya dhamira katika sauti ya Manju Baluni mwenye umri wa miaka 32.
Nilikutana naye katika kijiji cha Uttarakhand, jimbo lenye miinuko
kaskazini mwa India.
Nchini India,kuna ukimya kuhusu suala la afya
ya wanawake, hususan wawapo katika siku zao. Kuna mwiko uliojikita
katika jamii hizi kuhusu suala la mwanamke awapo katika hedhi: wanawake
si wasafi, wachafu, wagonjwa na wakati mwingine wamelaanika katika
kipindi hicho.
'Wasiwasi na Mashaka'
Watu wanaamini kuwa wanawake wanaokuwa katika hedhi hawatakiwi kuoga na wana upungufu wa damu.
Uchunguzi
wa hivi karibuni wa kampuni ya kutengeneza taulo maalum za kujisitiri
kina mama wanapokuwa katika hedhi umeonyesha kuwa asilimia 75% ya
wanawake wanaoishi mijini bado wananua taulo hizo zikiwa zimefungwa
katika mifuko au gazeti ili kutoonyesha kilichomo ndani kwa sababu ya
aibu inayohusishwa na hedhi.
Mwanamke akikunja taulo za kujihifadhi wakati wa siku zake nchini India
Na kamwe hawawaombi wanaume katika familia kuwanunulia taulo hizo maalum.
Nimekulia katika nyumba yenye wanawake wengi, lakini bado hatuwezi kujadili kwa uwazi suala hili ambalo ni la kawaida.
Wasichana
wanajifunza kuficha nguo zao wanazotumia wawapo kwenye hedhi kwa
wanaume baada ya kuzifua, anasema Rupa Jha. Mama yangu alitumia mashuka
makuu kuu na kuzificha katika sanduku, tayari kwa kutumiwa na mabinti
zake wanne.
Changamoto kubwa ni namna ya kukausha vipande hivyo
vya nguo. Nina kumbukumbu za kuhisi wasiwasi na mashaka juu ya mchakato
mzima.
Nilifundishwa mbinu nadada zangu wakubwa - namna ya kuficha
nguo zenye madoa ya damu chini ya nguo nyingine bila ya mwanaume yeyote
kugundua. Hatukuthubutu kuziacha peupe kwenye jua ili zikauke kabisa.
Nilihisi 'mchafu sana'
Matokeo ni kwamba kamwe hazikukauka vizuri, ziliacha harufu ya uvundo. Nguo hizo zisizo safi zilitumika tena na tena.
Wanawake wakisikiliza mwezeshaji kuhusu hali zao za usafi nchini India
Ukosefu wa maji ulifanya kazi
ya ufuaji kuwa ngumu na isiyo na usafi. Hali hiyo haijabadilika sana
tangu wakati huo kwa wanawake wengi wa Kihindi.
Uchunguzi mwingi
uliofanyika siku za karibuni umeonyesha kuwa mila hizi zimesababisha
madhara makubwa ya kiafya. Imeripotiwa kuwa mmoja kati ya wasichana
watano nchini India anaacha masomo kutokana na kadhia ya hedhi.
Baadhi
ya wasichana wanaacha kwenda shule wawapo katika kipindi cha hedhi.
Margdarshi mwenye umri wa miaka kumi na mitano anaishi katika kijiji cha
ndani cha Uttarakashi.
Anapenda kwenda shule japo inamaanisha
safari ngumu akipita katika eneo lenye vilima vikali. Kamwe hajawahi
kukosa masomo, isipokuwa kwa mwaka jana wakati ambapo nusura aache
masomo baada ya kupata siku zake kwa mara ya kwanza.
"Tatizo kubwa
kuliko yote ilikuwa namna ya kukabiliana na hali hiyo. Bado lipo.
Najisikia kufedheheshwa, hasira na mchafu sana. Mwanzoni niliacha kwenda
shule."
'Suala la kibinadamu'
Anataka kuwa daktari na
anashangaa kwa nini wavulana katika darasa lake wakati wa somo la elimu
ya viumbe(baolojia) wanacheka sana mwalimu anapoelezea njia ya hedhi.
"Nachukia.
Natamani tungekuwa huru zaidi na kujisikia huru tunapozungumzia suala
hili. Hali hii inatokea kwa kila mwanamke kwa hiyo kuna nini cha
kuchekesha hapo?"
Mama nchini India
Anshu Gupta, mwanzilishi wa
shirika lisilo la kiserikali, Goonj, anahisi kuwa tatizo hili limejikita
katika ukweli kwamba linahusishwa na wanawake.
Nchini India
wanawake wanatumia taulo za kujihifadhi wakati wawapo katika siku zao
kwa kutumia nguo kuu kuu. "Si suala la wanawake pekee. Ni suala la
kibinadamu lakini tumelibagua. Baadhi yetu tunataka kuondokana na
utamaduni huu wa kuona aibu na kunyamaza. Tunahitaji kuvunja utamaduni
huu."
Shirika hili linafanya kazi katika majimbo 21 kati ya 30.
Shirika
hili pia linatengeneza taulo rahisi kutokana na nguo zilizochakatwa
upya ili kuwasaidia asilimia 70% ya wanawake wa India ambao hawawezi
kupata taulo salama na safi.
Muhimu zaidi, wanaanza kuzungumzia suala hili. Bila kuhisi kufedheheka.
Makala
ya BBC ya BBC's 100 Women yamekuwa yakitangazwa katika mtandao, katika
televisheni na radio ya Idhaa ya Dunia tangu Oktoba 27-29. Changia maoni
yako katika mitandao ya kijamii ya Facebook na Twitter, ukitumia alama
#100Women.
Kituo
kimoja cha televisheni nchini Marekani kinachorusha kila siku kipindi
cha mhubiri Pat Robertson kiliomba radhi Jumatatu kwa madai yake potofu
kwamba wasafiri wanaokwenda Kenya wanaweza kupata maambukizi ya Ukimwi
kwa njia ya taulo.
"Dr Robertson alikosea kusema juu ya uwezekanao
wa kupata Ukimwi kwa njia ya mataulo," kimesema kituo cha Utangazaji
cha Kikristo, CBN, katika mtandao wa Facebook.
"CBN imegundua mara
moja kosa hili na kuondoa kauli hiyo kutoka kwa maktaba ya mtandao huo.
CBN inaomba radhi kwa mkanganyiko wowote."
Mhubiri huyo mwenye
umri wa miaka 84, mwinjilisti mkongwe ameonya katika kipindi chake cha
"700 Club" cha Oktoba 16 kwamba wasafiri watalazimika kuchukua tahadhari
ya hali ya juu ya kiafya wawapo nchini Kenya.
"Unaweza kupata
Ukimwi nchini Kenya," Bwana Robertson aliwaambia watazamaji wake
wanaokadiriwa kufikia milioni moja. "Watu wana ukimwi. Unatakiwa kuwa
makini. Nina maana kuwa, mataulo yanaweza kuwa na virusi vya Ukimwi."
Virusi vya HIV vinapatikana tu katika damu ya mwili na huenezwa tu kutoka kwa mwathiriwa
Madai ya Bwana Robertson haraka yalishambuliwa na makundi yanayojihusisha na masuala ya ugonjwa wa Ukimwi.
Wamesema
kuwa Ofisi ya serikali ya Marekani ya Masuala ya Afya ya kina Mama
inasema virusi vya Ukimwi haviwezi kuambukiza kwa njia ya "kushirikiana
vyombo vya chakula, mataulo na mashuka, simu au vyoo ."
'Hatari ya kutembelea Kenya'
Matamshi
ya Bwana Robertson yamekuja kutokana na swali alilotumiwa kwa njia ya
barua pepe na mtu asiyejulikana ambaye alielezea wasiwasi juu ya madhara
ya kutembelea Kenya wakati wa mlipuko wa Ebola barani Afrika.
Alimhakikishia
mtazamaji wa kipindi chake kuwa hakuna mgonjwa wa Ebola nchini Kenya
akisema Kenya iko mbali na kitovu cha mlipuko wa Ebola, Afrika
Magharibi.
Lakini Bwana Robertson alieleza hatari ya kuambukizwa magonjwa mengine nchini Kenya pamoja na Ukimwi.
Mbu
wanaweza kusababisha madhara makubwa ya ugonjwa, amesema, akiongezea
kwamba, "usafi akielezea kuwa tatizo lingine. Unakunywa maji,
hayajachujwa, unaweza kupata ugonjwa wa matumbo"
Jopo la Umoja wa Mataifa la wataalamu wa sayansi ya hali ya hewa,
limeonya leo kuwa mabadiliko makubwa yanatokea katika hali ya hewa
duniani na haitawezekana kurejesha hali ya zamani iwapo gesi
zinazozidisha joto duniani, hazitaondoshwa kabisa ufikapo mwisho wa
karne.
Ripoti iliyokubaliwa kwenye mkutano mjini Copenhagen, imechapishwa leo.
Dakta Peter Gleick ni mwana-sayansi wa mabadiliko ya hali ya hewa ambaye ameiona ripoti hiyo.
Aliiambia BBC, ushahidi wa kisayansi ni mzito sasa, kuwa binaadamu ndiye chanzo cha mabadiliko ya hali ya hewa:
"Bila ya shaka watu wasioamini kuwa wanaadamu ndio wanasababisha mabadiliko ya hali ya hewa, hawataki kusikiliza sayansi.
Kuna maswala magumu ya kisiasa yanahitaji kuamuliwa, lakini siyo ya kisayansi tena.
Ushahidi katika sayansi ni thabiti - kwamba hali ya hewa inabadilika; kwamba wanaadamu ndio wanayosababisha hayo.
Na kwamba ikiwa hatuchukui hatua sasa, basi totaona matokeo makubwa na hasara itakuwa kubwa kwa watu na dunia yenyewe."
Na
Waziri wa Mashauri ya nchi za Nje wa Marekani, John Kerry, alisema wale
wanaodharau sayansi kuhusu hali ya hewa iliomo kwenye ripoti hiyo,
wanahatarisha maisha yetu, watoto na wajukuu wetu.