Roma Mkatoliki na wenzake wapatikana Tanzania
Msanii Roma
Mkatoliki aliyedaiwa kutoweka na watu wasiojulikana nchini Tanzania sasa
amepatikana katika kituo cha polisi cha Oysterbay jijini Dar.
Habari
hizo zimethibtishwa na mmiliki wa studio za Tongwe ambapo msanii huyo
na wenzake wawili wanadaiwa kuchukuliwa na watu wasiojulikana siku ya
Jumatano jioni.Hata hivyo mmiliki huyo J Mada anasema kuwa hakuna maelezo ya kutosha kuhusiana na wapi walipokuwa na ni akina nani aliokuwa wanawazuia.
Serikali yaomba usaidizi kumtafuta Roma Mkatoliki
Awali, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Kamishina Simon Sirro alisema bado walikuwa wakiendelea na upelelezi wa tukio la kupotea (kutekwa) kwa msanii Roma Mkatoliki na wenzake.