Tuesday, January 20, 2015

Eti mafuta ya mwilini hukuza ubongo?



Eti mafuta ya mwilini hukuza ubongo?





Fumbo la siku zote kwamba wanawake ni wanene kuliko wanaume limepata ufumbuzi...ni wanene kwa wanahitaji mwili wenye umbo zuri na makalio makubwa ili kupata watoto waliojaaliwa werevu.
Taarifa hii ni kwa mujibu wa wanaakademia ambao wanasema kuwa wanawake wenye makalio na mapaja makubwa na umbo zuri kutokana na mafuta mfano kama Kim Kardashian hupata watoto werevu.
Nini hasa kinawafanya watoto wao kuwa werevu basi? Mafuta yanayopatikana katika sehemu za mwili wa mwanamke huwa na manufaa makubwa sana kwa watoto hasa wanapokuwa wananyonya, mafuta haya hupitia kwenye maziwa ya mama hadi kwa mwili wa mtoto.
Profesa Will Lassek wa chuo kikuu cha Pittsburgh University, Pennsylvania, aliyeongoza utafiti huo, anasema mafuta yanayopatikana katika sehemu hizo za mwili, husaidia sana katika kukuza ubongo wa matoto mchanga.



'Unahitaji mafuta mengi ya mwilini ili kuwa na mfumo mzuri wa neva na mafuta katika sehemu hizi za mwili yaani mapaja na makalio, huwa yina madini yajulikanayo kama DHA (docosahexaenoic acid), ambayo ni muhimu sana katika kutengeza ubongo wa binadamu.
Inaonekana kama wanawake wameweza kujua mbinu za kuhifadhi mafuta katika sehemu hizo za mwili hadi wanapopata mtoto.
Kwa mda mrefu haijajulikana kwa nini wanawake wanakuwa wanene sana.......mafuta ya mwili wao yakiwa ni asilimia 30 ya uzani wa mwili.
Professa Lassek anasema kwamba mafuta hayo ni kiwango sawa na yale yanayopatikana katika wanyama kama Dubu au Nyangumi wanapojiandaa kuzaa.
Wanasayansi wanasema mafuta yanayopatikana katika mapaja na makalio ya wanawake ndio yanayotumika kutengeza ubongo wa watoto wachanga.
Mafuta mengi katika mwili wa mwanamke huisha mwilini pindi mama anapomnyonyesha mtoto wake, kulingana na Profesa Lassek, aliyechapisha utafiti wake katika kitabu chake kipya chenye kichwa ''Kwa nini wanawake wanahitaji mafuta mwilini. ''
Wanawake wanaonyonyesha hupoteza kilo nusu ya mafuta mwilini kila mwezi.

Hali mbaya ya hewa yaikabili Zambia

Hali mbaya ya hewa yaikabili Zambia



Matokeo ya uchaguzi mkuu wa Zambia uliofanyika jana yatatangazwa kama ilivyopangwa awali.
Hata hivyo kutangazwa kwa matokeo hayo kunakabiliwa na changamoto mbalimbali kutokana na baadhi ya vituo vya kupigia kura kushindwa kupiga kura jana, na hivyo kufanyika leo.
Vituo hamsini na moja vitapiga kura hii leo na sababu kubwa ni mvua kubwa iliyo nyesha nchi yote ya Zambia ,hali mbaya ya hewa na kucheleweshwa kwa karatasi za kupigia kura ni sababu zilizotajwa kusababisha wananchi wa Zambia kutopiga kura na leo wapewe haki hiyo.
Hali mbaya ya hewa pia huenda ikasababisha hata matokeo ya uchaguzi kutolewa kama ilivyosemwa awali,naye Rafael Phiri,msemaji wa tume ya uchaguzi ya Zambia amethibitisha kuwa endapo yatachelewa sana haitazidi tarehe ishirini na nne mwezi huu.

Rais Obama ataka mgao sawa wa rasilimali

Rais Obama ataka mgao sawa wa rasilimali 

 
Rais Barack Obama wa Marekani
Rais wa Marekani Barak Obama, amesema Marekani inafanya mabadiliko ya kiuchumi na kijamii baada ya miaka mingi ya kujirudia kwa mdororo wa uchumi na vita, huku uchumi ukiongeza ajira kwa kasi kubwa kuliko wakati wowote tangu mwaka 1999.
Pia amesema Wamarekani wengi zaidi wana bima za afya kuliko wakati wowote kabla ya hapo.
Akihutubia taifa kupitia baraza la Congress lenye wajumbe wengi kutoka chama cha Republican, Rais Obama ametumia hotuba hiyo kutangaza mpango wa kujenga uchumi wa kati kwa wananchi wote wa Marekani, ambapo wananchi wa kipato cha chini watapata huduma za afya na elimu kwa gharama nafuu.
Rais Obama ametangaza hatua za kusaidia familia za wafanyakazi kunufaika kutokana na kukua kwa uchumi.Mkakati wa Bwana Obama anaouelezea kama uchumi wa daraja la kati, unahusisha kupandisha kodi kwa matajiri.
Hotuba ya Rais Obama ilibeba mapendekezo kuhusu kodi, vyuo vya jamii, huduma za internet, usalama katika mtandao wa komputa na likizo ya ugonjwa.
Bwana Obama amesema hali ya kutoka katika mdororo wa uchumi imetoa fursa ya kuongezeka kwa kipato na fursa kwa kila mtu.
Amesema uchumi wa daraja la kati ni wazo kwamba nchi hiyo inafanya vizuri kabisa wakati kila mtu anapata haki katika mapato na kila mtu anatendewa haki kama ilivyoanishwa katika sheria za nchi hiyo.