Monday, November 3, 2014

Warioba adhalilishwa mdahalo wa Katiba

Warioba adhalilishwa mdahalo wa Katiba

  • 2/11/2014
Waziri Mkuu mstaafu Joseph Warioba akisaidiwa kutolewa katika vurugu
Katika mazingira ya kutatanisha, siku ya Jumapili vurugu zimekatisha mdahalo uliokuwa ukiendelea kujadili mchakato wa katiba mpya ya Tanzania huku baadhi ya watu wakipigwa na kujeruhiwa.
Mdahalo huo uliokuwa ukitangazwa moja kwa moja kupitia redio na televisheni ulivurugika kutokana na kundi la vijana wapatao 20 kuanza kumzomea aliyekuwa mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, alipokuwa akiwasilisha mada yake.
Vijana hao ambao haijajulikana walitokea wapi au walikuwa na ajenda gani waliinua mabango ya kupinga msimamo wa waliokuwa wakiendesha mdahalo na kusema rasimu ya katiba iliyopendekezwa inakidhi mahitaji yote na kusema hakuna haja ya mdahalo.
Jaji Warioba ambaye ni Waziri Mkuu mstaafu wa Tanzania alifanikiwa kutoka nje ya ukumbi ulipokuwa ukifanyika mdahalo huo mjini Dar Es Salaam, lakini wapo watu waliojeruhiwa kutokana na kurushwa viti na vitu vingine.
BBC iliwasiliana na Jaji Warioba apate kueleza yaliyotokea na kama yuko salama baada ya vurugu hizo, lakini aliomba radhi kwa kusema hayupo tayari kulizungumzia swala hilo.
Kiongozi wa kitengo cha hamasa umoja wa vijana CCM (UVCCM), Paul Makonda, aliyekuwepo ukumbini alidaiwa kuhusika na vurugu. Lakini alipoulizwa na BBC kujibu tuhuma hizo Bw Makonda amekanusha kuhusika nazo huku akisema kwamba alihudhuria mdahalo kwasababu ulikuwa wazi kwa kila mtu.
Wakati wa vikao vya Bunge Maalum la Katiba mjini Dodoma, Makonda aliwahi kutoa kauli za kumkebehi Jaji Warioba ambaye tume yake iliandaa rasimu ya iliyokuwa ikijadiliwa na bunge hilo.
Hata hivyo Kamanda wa Polisi mkoa wa Kinondoni, Camillius Wambura, aliieleza BBC kuwa hana maelezo ya kutosha na kwamba atalizungumzia akipata taarifa rasmi ya kiofisi.
Tanzania ipo katika mchakato wa kupata katiba mpya. Rasimu iliyodaliwa na kupitishwa na bunge lililosusiwa na vyama vya upinzani inatarajiwa kupigiwa kura na wananchi mwezi Aprili, 2015.
Wachambuzi wa maswala ya kisiasa wameeleza wasi wasi kuwa endapo hakutakuwa na kuvumiliana hali ya kisiasa nchini humo inaweza kubadilika na kuleta ghasia ambazo zinaweza kuepukika.
  • Saa 9 zilizopita

Hedhi yawa fedheha kwa wanawake India

Hedhi yawa fedheha kwa wanawake India

  • 31 Oktoba 2014

Wanawake wakifua na kuoga nchini India

"Sitamwaacha binti yangu ateseke kama mimi ninavyoteseka nikiwa katika siku zangu. Familia yangu inafanya nijihisi najisi.
"Siruhusiwi kwenda jikoni, Siwezi kuingia hekaluni, Siwezi kukaa na wengine."
Kuna hisia ya dhamira katika sauti ya Manju Baluni mwenye umri wa miaka 32. Nilikutana naye katika kijiji cha Uttarakhand, jimbo lenye miinuko kaskazini mwa India.
Nchini India,kuna ukimya kuhusu suala la afya ya wanawake, hususan wawapo katika siku zao. Kuna mwiko uliojikita katika jamii hizi kuhusu suala la mwanamke awapo katika hedhi: wanawake si wasafi, wachafu, wagonjwa na wakati mwingine wamelaanika katika kipindi hicho.
'Wasiwasi na Mashaka'
Watu wanaamini kuwa wanawake wanaokuwa katika hedhi hawatakiwi kuoga na wana upungufu wa damu.
Uchunguzi wa hivi karibuni wa kampuni ya kutengeneza taulo maalum za kujisitiri kina mama wanapokuwa katika hedhi umeonyesha kuwa asilimia 75% ya wanawake wanaoishi mijini bado wananua taulo hizo zikiwa zimefungwa katika mifuko au gazeti ili kutoonyesha kilichomo ndani kwa sababu ya aibu inayohusishwa na hedhi.
 
Mwanamke akikunja taulo za kujihifadhi wakati wa siku zake nchini India
Na kamwe hawawaombi wanaume katika familia kuwanunulia taulo hizo maalum.
Nimekulia katika nyumba yenye wanawake wengi, lakini bado hatuwezi kujadili kwa uwazi suala hili ambalo ni la kawaida.
Wasichana wanajifunza kuficha nguo zao wanazotumia wawapo kwenye hedhi kwa wanaume baada ya kuzifua, anasema Rupa Jha. Mama yangu alitumia mashuka makuu kuu na kuzificha katika sanduku, tayari kwa kutumiwa na mabinti zake wanne.
Changamoto kubwa ni namna ya kukausha vipande hivyo vya nguo. Nina kumbukumbu za kuhisi wasiwasi na mashaka juu ya mchakato mzima.
Nilifundishwa mbinu nadada zangu wakubwa - namna ya kuficha nguo zenye madoa ya damu chini ya nguo nyingine bila ya mwanaume yeyote kugundua. Hatukuthubutu kuziacha peupe kwenye jua ili zikauke kabisa.
Nilihisi 'mchafu sana'
Matokeo ni kwamba kamwe hazikukauka vizuri, ziliacha harufu ya uvundo. Nguo hizo zisizo safi zilitumika tena na tena.
 
Wanawake wakisikiliza mwezeshaji kuhusu hali zao za usafi nchini India
Ukosefu wa maji ulifanya kazi ya ufuaji kuwa ngumu na isiyo na usafi. Hali hiyo haijabadilika sana tangu wakati huo kwa wanawake wengi wa Kihindi.
Uchunguzi mwingi uliofanyika siku za karibuni umeonyesha kuwa mila hizi zimesababisha madhara makubwa ya kiafya. Imeripotiwa kuwa mmoja kati ya wasichana watano nchini India anaacha masomo kutokana na kadhia ya hedhi.
Baadhi ya wasichana wanaacha kwenda shule wawapo katika kipindi cha hedhi. Margdarshi mwenye umri wa miaka kumi na mitano anaishi katika kijiji cha ndani cha Uttarakashi.
Anapenda kwenda shule japo inamaanisha safari ngumu akipita katika eneo lenye vilima vikali. Kamwe hajawahi kukosa masomo, isipokuwa kwa mwaka jana wakati ambapo nusura aache masomo baada ya kupata siku zake kwa mara ya kwanza.
"Tatizo kubwa kuliko yote ilikuwa namna ya kukabiliana na hali hiyo. Bado lipo. Najisikia kufedheheshwa, hasira na mchafu sana. Mwanzoni niliacha kwenda shule."
'Suala la kibinadamu'
Anataka kuwa daktari na anashangaa kwa nini wavulana katika darasa lake wakati wa somo la elimu ya viumbe(baolojia) wanacheka sana mwalimu anapoelezea njia ya hedhi.
"Nachukia. Natamani tungekuwa huru zaidi na kujisikia huru tunapozungumzia suala hili. Hali hii inatokea kwa kila mwanamke kwa hiyo kuna nini cha kuchekesha hapo?"
 
Mama nchini India
Anshu Gupta, mwanzilishi wa shirika lisilo la kiserikali, Goonj, anahisi kuwa tatizo hili limejikita katika ukweli kwamba linahusishwa na wanawake.
Nchini India wanawake wanatumia taulo za kujihifadhi wakati wawapo katika siku zao kwa kutumia nguo kuu kuu. "Si suala la wanawake pekee. Ni suala la kibinadamu lakini tumelibagua. Baadhi yetu tunataka kuondokana na utamaduni huu wa kuona aibu na kunyamaza. Tunahitaji kuvunja utamaduni huu."
Shirika hili linafanya kazi katika majimbo 21 kati ya 30.
Shirika hili pia linatengeneza taulo rahisi kutokana na nguo zilizochakatwa upya ili kuwasaidia asilimia 70% ya wanawake wa India ambao hawawezi kupata taulo salama na safi.
Muhimu zaidi, wanaanza kuzungumzia suala hili. Bila kuhisi kufedheheka.
Makala ya BBC ya BBC's 100 Women yamekuwa yakitangazwa katika mtandao, katika televisheni na radio ya Idhaa ya Dunia tangu Oktoba 27-29. Changia maoni yako katika mitandao ya kijamii ya Facebook na Twitter, ukitumia alama #100Women.

Taulo Kenya zina ukimwi',asema mhubiri

Taulo Kenya zina ukimwi',asema mhubiri

  • 22 Oktoba 2014
Kituo kimoja cha televisheni nchini Marekani kinachorusha kila siku kipindi cha mhubiri Pat Robertson kiliomba radhi Jumatatu kwa madai yake potofu kwamba wasafiri wanaokwenda Kenya wanaweza kupata maambukizi ya Ukimwi kwa njia ya taulo.
"Dr Robertson alikosea kusema juu ya uwezekanao wa kupata Ukimwi kwa njia ya mataulo," kimesema kituo cha Utangazaji cha Kikristo, CBN, katika mtandao wa Facebook.
"CBN imegundua mara moja kosa hili na kuondoa kauli hiyo kutoka kwa maktaba ya mtandao huo. CBN inaomba radhi kwa mkanganyiko wowote."
Mhubiri huyo mwenye umri wa miaka 84, mwinjilisti mkongwe ameonya katika kipindi chake cha "700 Club" cha Oktoba 16 kwamba wasafiri watalazimika kuchukua tahadhari ya hali ya juu ya kiafya wawapo nchini Kenya.
"Unaweza kupata Ukimwi nchini Kenya," Bwana Robertson aliwaambia watazamaji wake wanaokadiriwa kufikia milioni moja. "Watu wana ukimwi. Unatakiwa kuwa makini. Nina maana kuwa, mataulo yanaweza kuwa na virusi vya Ukimwi."
Virusi vya HIV vinapatikana tu katika damu ya mwili na huenezwa tu kutoka kwa mwathiriwa
Madai ya Bwana Robertson haraka yalishambuliwa na makundi yanayojihusisha na masuala ya ugonjwa wa Ukimwi.
Wamesema kuwa Ofisi ya serikali ya Marekani ya Masuala ya Afya ya kina Mama inasema virusi vya Ukimwi haviwezi kuambukiza kwa njia ya "kushirikiana vyombo vya chakula, mataulo na mashuka, simu au vyoo ."
'Hatari ya kutembelea Kenya'
Matamshi ya Bwana Robertson yamekuja kutokana na swali alilotumiwa kwa njia ya barua pepe na mtu asiyejulikana ambaye alielezea wasiwasi juu ya madhara ya kutembelea Kenya wakati wa mlipuko wa Ebola barani Afrika.
Alimhakikishia mtazamaji wa kipindi chake kuwa hakuna mgonjwa wa Ebola nchini Kenya akisema Kenya iko mbali na kitovu cha mlipuko wa Ebola, Afrika Magharibi.
Lakini Bwana Robertson alieleza hatari ya kuambukizwa magonjwa mengine nchini Kenya pamoja na Ukimwi.
Mbu wanaweza kusababisha madhara makubwa ya ugonjwa, amesema, akiongezea kwamba, "usafi akielezea kuwa tatizo lingine. Unakunywa maji, hayajachujwa, unaweza kupata ugonjwa wa matumbo"

Mazingira yahitaji hatua haraka

Mazingira yahitaji hatua haraka

  • 2 Novemba 2014
Jopo la Umoja wa Mataifa la wataalamu wa sayansi ya hali ya hewa, limeonya leo kuwa mabadiliko makubwa yanatokea katika hali ya hewa duniani na haitawezekana kurejesha hali ya zamani iwapo gesi zinazozidisha joto duniani, hazitaondoshwa kabisa ufikapo mwisho wa karne.
Ripoti iliyokubaliwa kwenye mkutano mjini Copenhagen, imechapishwa leo.
Dakta Peter Gleick ni mwana-sayansi wa mabadiliko ya hali ya hewa ambaye ameiona ripoti hiyo.
Aliiambia BBC, ushahidi wa kisayansi ni mzito sasa, kuwa binaadamu ndiye chanzo cha mabadiliko ya hali ya hewa:
"Bila ya shaka watu wasioamini kuwa wanaadamu ndio wanasababisha mabadiliko ya hali ya hewa, hawataki kusikiliza sayansi.
Kuna maswala magumu ya kisiasa yanahitaji kuamuliwa, lakini siyo ya kisayansi tena.
Ushahidi katika sayansi ni thabiti - kwamba hali ya hewa inabadilika; kwamba wanaadamu ndio wanayosababisha hayo.
Na kwamba ikiwa hatuchukui hatua sasa, basi totaona matokeo makubwa na hasara itakuwa kubwa kwa watu na dunia yenyewe."
Na Waziri wa Mashauri ya nchi za Nje wa Marekani, John Kerry, alisema wale wanaodharau sayansi kuhusu hali ya hewa iliomo kwenye ripoti hiyo, wanahatarisha maisha yetu, watoto na wajukuu wetu.

IS waua zaidi ya watu 300 Iraq

IS waua zaidi ya watu 300 Iraq

wapiganaji wa Islamic State
Maofisa wa serikali nchini Iraq wamesema wapiganaji wa Islamic State wameua watu zaidi ya 300 wa madhehebu ya Sunni ambao wamekuwa wakipigana na kundi hilo katika jimbo la Anbar.
Waziri wa Iraq wa masuala ya haki za binadamu amesema kuwa miili zaidi 50 ikiwemo ya wanawake na watoto ilikutwa ikielea katika visima.
Hata hivyo vyanzo kutoka jamii ya Al-Bu Nimr vimeerifu kuwa kumekuwa na mauaji kwa awamu tatu tangu alhamisi wiki iliyopita maeneo mbalimbali ya Iraq wakiwemo wale wanajitoa mhanga katika mabomu.
Mashambulizi zaidi yanatarajiwa kwa waumini wa dini ya Shia katika sherehe za za Ashura.